. Akana kupewa hela mbunge,
. Wasema apewe nafasi nyingine.
Ni katika kata ya Nyakibimbili wilayani Bukoba vijijini
kaskazini magaharibi mwa mkoa wa Kagera, katika jimbo analogombea Jasson
Rweikiza, huku wananchi wakimuuliza ataomba vipi kura zao ilhali alishindwa
kukamilisha barabara inayowafanya kukosa huduma muhimu za matibabu na
kusafirisha bidhaa zao za kilimo kupata masoko.
Hatahivyo inadaiwa kuwa mbunge huyo amesikika akisema kuwa barabara hiyo imeshindwa kukamilika baada ya diwani wa kata hiyo SYLVAND LUGALAMULA kukataa pesa za ukarabati wake.
Katika mahojiano maalumu na kandayaziwa blog, diwani wa kata
hiyo aliyemaliza muda wake Bwana Sylivand Lugalamula amefafanua kuwa anahisi
mbunge huyo amechukia baada ya kushiriki kampeini za kumchagua mwenyekiti wa
halmashauri.
Sambamba na tatizo la barabara, wakaazi wa vijiji vya Nyakibimbili, Kitahya Bugengere na Bundaza, wanakabiliwa na huduma ya matibabu huku wakijengewa kliniki na shirika la kiraia WORLDVISION, ambayo hatahivyo haina wahudumua.
Kandayaziwa blog, bado inaendelea kumtafuta mbunge wa jimbo anayemaliza muda wake katika jimbo la Bukoba mjini kupata maelezo yake kuhusu hilo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment