MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 21 July 2015

WAGOMBEA UBUNGE MANISPAA BUKOBA KUUNGANA

. Ni CCM katika kampeini katika kata,
. Mikutano kuanza 23 hadi 30 julai 2015.
Wakati wa kuelekea katika uchaguzi mkuu, mchakato wa kupata wagombea katika majimbo na kata unaendelea ambapo walioomba nafasi ya ubunge katika manispaa ya Bukoba, wanaanza mchakato wa kutembelea kata zote 14 kuomba kura kwa wajumbe kwa kujielezea na jinsi gani watatekeleza ilani ya CCM kwa atakayechaguliwa.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu ofisi kwake, katibu wa CCM wilaya ndugu Abdul Kambuga, amesema kuwa kwa mujibu wa utaratibu wa chama, inabidi watangaza nia wote waongozane kufanya mikutano kila kata, ambapo kama kuna mgombea anayetaka kwenda na gari yake binafsi anaomba kufanya hivyo ingawa ni lazima awe kwenye msafara mmoja.
Jumla ya wabunge waliotangaza nia ya kugombea jimbo la Bukoba mjini ni 8 baada ya mmoja kushindwa kurejesha fomu, na kufanya idadi ya watu 9 waliochukua fomu kutotimia.

Na Mwanaharakati.

No comments: