MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 17 August 2015

BREAKING NEWS!!! RED CROSS WAJIONDOA KUTOA HUDUMA KAGERA

. Mkoa wajipanga,
. Damu hatarini kukosekana.


Kutokana na hali hiyo, serikali ya mkoa inaangalia namna ya kukabiliana na damu kwa matumizi ya wagonjwa katika hospitali, baada ya RED CROSS ukijitoa.

Akizungumza na mwandishi wa kituo hiki, mkuu wa mkoa wa Kagera Bwana John Mongela, amesema kuwa kujiondoa kwao kunatokana na kumalizika kwa mkataba kati ya serikali na shirika la msalaba mwekundu(RED CROSS), ambayo ameelezea kuwa ni jambo zito na linahitaji nguvu za pamoja kwasababu ya unyeti wake hivyo inapaswa kufanyiwa haraka
Amesema kuwa wamefanya kazi hiyo kwa kipindi kirefu katika program mbalimbali tofauti na suala la damu salama, hivyo viongozi na wananchi, ni wakati kukaa pamoja katika kukabiliana na hali hii.

Taarifa ya shirika la msabalaba mwekundu Tanzania kwa ufadhili wa serikali ya Marekani CDC, ambao umekuwa ukikusanya damu kutoka wilaya zote na kupelkwa mwanza kwa upimaji na kuhakikisha inavifikia vituo vyote vya usambazaji, limetoa taarifa kuwa  ufadhili wake kwa TRCS umefikia ukomo October mwaka huu na RED CROSS kusitisha huduma zake mkoani Kagera.

Kuondoka kwa red cross kunaipa jukumu serikali kujipanga na kuratibu huduma hiyo bila ufadhili, na inashauriwa kuwatumia watalaamu ambao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kupitia ufadhili ili wasaidie kwa utalamu wao kupitia bajeti ya serikali kila mwaka.

Na Mwanaharakati.

No comments: