. Kulikuwa na mtandao wa watu 10,
. Asema wanaoondoka ndani yake
waondoke,
. Asema utajiri usitumike kukandamiza
wanyonge.
Ni mwenyekiti wa taasisi ya mwalimu Nyerere alipozungumza na
watanzania kupitia mdahalo ulioandaliwa na taasisi hiyo, kwakusema kuwa mtandao
huo uliokuwa umejikita ndani ya CCM, ulikuwa ukiweka masharti ndani ya chama
hicho kuwa usizungumziwe kuhusu utajiri wake.
Amesema kuwa utajiri siyo tatizo tatizo ni jinsi utajiri huo unavyotumika, kwa kuwatupia wananchi kama kuku, jambo ambalo Mwalimu Nyerere alisema ni lazima heshima ijengwe kwenye chama na asiyetaka anaweza kuondoka.
Kwaupande wake Profesa Balegu, amesema kuwa hawezi kutoa tuhuma kwa mtu yeyote, huku akisistiza kuwa unaweza kufanya kazi kwenye taasisi yenye uadilifu nawe ukawa mwadilifu au ikawa kinyume chake.
Humphrey Polepole, amesema kuwa Nyerere asitafsriwe vibaya kwa kusema kuwa alitaka mabadiliko
kwani mwenyewe alitaka mageuzi ambayo yanajumuisha mambo mengi na yenye kuwaletea wananchi maendeleo na uwajibikaji bora, wala siyo mabadiliko ya vyama kama wengi wanavyoimba.
kwani mwenyewe alitaka mageuzi ambayo yanajumuisha mambo mengi na yenye kuwaletea wananchi maendeleo na uwajibikaji bora, wala siyo mabadiliko ya vyama kama wengi wanavyoimba.
Naye Bwana Muhammad Yusuph Mshamba, amesema kuwa sheria ni lazima ifuatwe katika mchakato huu
wa uchaguzi mkuu, kwani wakisea huku ya ICC haitahepukika kwasababu Tanzania ni mwanachama wa mahakama hiyo ya kimataifa ya makosa ya jinai.
Katibu wa CCM Tanzania bara Bwana Philip Mangula, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ndogo ya maadili ndani ya chama hicho, amesema kuwa yeye kama mmoja wa wajumbe wa umoja wa vyama 22 vya siasa nchini, walikubaliana kwa pamoja kuhakikisha wanatuza maadili ya vyama vyao hivyo atashangaa kuona ukiukwaji unaendelea katika vyama.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment