MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 16 August 2015

HATARI; HII NDIYO KAZI YA SHERIA YA MTANDAO NA UTANGAZAJI



Serikali imevitaka vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu kutoa wasemaji wa mwenendo wa siasa katika kipindi chote cha uchaguzi.

Mkurugenzi wa idara ya utangazaji Tanzania, amesema hayo wakati wa kuchambua kanuni za utangazaji katika vyombo vya habari wakati wa uchaguzi wa vyama vya siasa hapa nchini, kwenye semina ya siku moja iliyowashirikisha wakurugenzi, wahariri na waandaaji vipindi wa redio na tv kanda ya ziwa.

Amesema kuwa kutokana na kupitishwa kwa sheria kuhusu vyombo vya habari na utangazaji, ni lazima hata vyama vifuate utaratibu elekezi, ili kutoa fursa pande zote kushiriki kikamilifu huku akisisitiza kuwa hakuna chama cha siasa au chombo cha habari kitakachoonewa kama sheria na taratibu zilizowekwa zitafuatwa.
Kwaupande wake afisa mkuu wa utangazaji Tanzania Andrew Kisaka, amesema kuwa hakuna tatizo la mtangazaji au mwandishi kufanya mawasiliano na chama cha siasa au mwanasiasa kwa lengo la kupata habari, ingawaje mwandishi atakayeshiriki kugombea atatakiwa aombe likizo au kuacha kazi kwa muda wote wa uchaguzi
Amesema kuwa wanasiasa watakaotakiwa kuhojiwa na vyombo vya habari, watatakiwa kukubali ili kusaidia chombo husika kufanya kipindi chenye uwiano sawa, kwani atakapokataa haitaondoa chama kingine au mwanasiasa mwingine kuhojiwa ingawa lazima vyama viwili au zaidi vishiriki kipindi hicho.
 
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, imetoa semina hiyo kwa vyombo vya habari kanda ya ziwa, kwa dhamira ya kudhibiti mawasiliano, kusisitiza kufuata sheria itakayoanza kutumika tarehe 1 mwezi wa 9/2015. 

Na Mwanaharakati.

No comments: