Taarifa kutoka Karagwe mkoani Kagera,
zinasema kuwa mvua zilizonyesha Agosti
30 na 31 mwaka
huu katika kata
ya Bugene zimesababisha
maafa katika kijiji
cha Kishao baada
ya migomba kuangushwa
na upepo mkali
na kuna baadhi
ya nyumba nazo
zimebomolewa na mvua
hizo.
Afisa Mtendaji wa Kata
Bugene Bw. Deus Ntinchwa amesema kuwa
maafa yaliyosababishwa na
mvua hizo, zilizoanza kunyesha
majira ya saa kumi na moja jioni, na kusema kuwa jumla migomba
iliyoanguka ni 58,365,nyumba zilizoezuliwa paa ni 15,na zilizoharibika sehemu ndogondogo
ni 9,na mihogo iliyoharibika ni1661.
Kutokana na mahafa hayo, wananchi
wametakiwa kupanda mazao
kwa wakati na
kutakiwa kuchukua tahadhari
juu ya watoto
wao kipindi hiki
cha mvua za
vuli zilizoanza kwa kasi kubwa.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment