. Mmoja ashikiliwa kwa mauaji.
Taarifa
ya polisi mkoani Kagera juu ya tukio hilo na la mauaji, inasema kuwa
wanaendelea kuwatafuta watu watatu kwa tuhuma za kutelekeza begi
lililokuwa na silaha za kivita.
Kamanda
wa polisi mkoa humo Agustino Olomi , mesema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 1
mwezi Septemba mwaka huu karibu na kituo
kidogo cha polisi Kalenge wilayani Biharamlo, baada ya kupata taarifa kutoka
kwa raia wema waliokuwa wakisafiri
kutoka Kibondo Kwenda Kahama kuwa kwenye gari lao kuna watu watatu wanawatilia
mashaka.
Amebainisha
kuwa,watu hao baada ya kutelekeza begi hilo wametokomea polini na jeshi la
polisi linaendelea kuwasaka ili kuwabaini.
Hatahivyo
polisi mkoani Kagera inamshikilia
mwendesha pikipiki mmoja baada ya kumgonga mtembea kwa miguu na kufariki dunia.
Mtuhumiwa
huyo ametajwa na polisi kuwa ni Siliakus Almachius mwenye umri wa miaka 22 na
aliyefariki ni Anacreti Anastazi mwenye umri wa miaka 40 mzaliwa wa Karagwe.
Kamanada
Olomi amesema kuwa,baada ya ajali hiyo kutokea,mwendesha pikipiki huyo
alitoroka lakini baadae polisi walimpata, na kuwa mtuhumiwa huyo muda wowote atafikishwa
mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment