. Pia aliweka miundombinu kadhaa,
. Uzio wahitajika kudhibiti wanafunzi,
. Wanafunzi watumika kuvua samaki.
Ni
miaka mitano sasa tangu shule ya sekondari Lutunga kuanzishwa, ambapo ufaulu wa kwanza wa kidato cha nne mwaka jana 2014 wanafunzi wanne walichaguliwa kujiunga kidato
cha tano, kati ya wahitimu 48.
Mwandishi
wa mtandao huu ametembelea shule hiyo na kutajiwa changamoto, ya
ukosefu wa
uzio, upungufu wa nyumba za walimu, uhaba wa huduma ya maji, na mahitaji ya
huduma ya umeme, kama alivyofafanua Madam Hawa….
Kwa
mujibu wa uongozi ndani ya kata Kahororo manispaa ya Bukoba, shule hiyo
ilanzishwa baada ya mbunge anayemaliza muda wake Balozi Khamis Kagasheki, kununua kiwanja ili wajenge shule hiyo, kwa wakaazi baada ya
kupendekezwa kwa eneo husika, na kuchangia ujenzi wa shule hiyo, ambayo hadi
sasa ina madarasa 4 ikiwa bado na uhitaji wa madarsa 4 ili kukamilisha mikondo
miwili inayotakiwa kuwa katika shule hiyo na kukidhi mahitaji ya wanafunzi zaidi
160 waliopo shuleni hapo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment