MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 5 October 2015

NORTH MARA SASA KUWAJALI WANYONGE TANZANIA- SOMA KILICHOJIRI



Ni baada ya kukamilisha na kuzindua shule ya Sekondari JK Nyerere pamoja na nyumba za walimu, kwa gharama ya shilingi bilioni 1.7 wilayani Tarime.

Ujenzi wa shule hiyo iliyopo kijiji cha Nyamwaga  kinachopakana na mgodi huo umeenda sambamba na ununuzi wa samani za ofisi za walimu, madarasa na maabara.

Meneja wa Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,  Jimmy Ijumba amesema shule hiyo imejengwa kwa awamu  ambapo kwasasa zimekamilika awamu mbili ambazo wigo wake ni madarasa nane, nyumba za walimu sita zenye vyumba vya kulala vitatu, stoo, jiko, bafu, tanki la maji pamoja na uzio, jengo la utawala, maktaba, maabara mbili, vyoo vya walimu na wanafunzi vyenye  matundu 33.

Aidha Mgodi huo umenunua kompyuta za wanafunzi na walimu, photocopier machine, printer, projector na scanner kwa ajili ya shule hiyo.

Alifafanua kwamba ujenzi wa shule hiyo umekuwa ukitekelezwa kwa awamu kutokana na shule kuwa mpya kwani ina kidato cha kwanza na cha pili na kama majengo yote yangejengwa kwa wakati mmoja yangekosa matumizi.

“Awamu ya tatu ya ujenzi wa shule hii utatekelezwa mwakani kwa kuhusisha madarasa manne, bwalo la chakula na chumba cha kupumzikia wagonjwa”, alisema Ijumba.

Kwa upande wake Mama Kikwete aliipongeza kampuni ya ACACIA  kwa kuchangia jitihada za Serikali za kuboresha elimu kwa watoto na kusema kuwa mfano huo unapaswa kuigwa na makampuni mengine hapa nchini.

Alisema njia pekee ya kupambana na ujinga, maradhi na umasikini ni kuwapeleka watoto shule kwani wao ndiyo tegemeo la wazazi, nguvu kazi na rasilimali ya taifa. 

Wakielimishwa watakuwa wanawatengenezea njia ya kujikomboa katika Nyanja za kijamii na kiuchumi na watakuwa msaada mkubwa kwa wazazi wao pindi watakapokuwa wazee.

Mradi wa ujenzi wa shule ya JK Nyerere ni moja kati ya miradi ya kijamii katika kijiji cha Nyamwaga inayotekelezwa kwa ufadhili  wa mgodi kama ilivyoainishwa kwenye mkataba wa manufaa ya vijiji (VBIA) uliosainiwa kati ya mgodi na kijiji mwezi Februari 2012.
Miradi mingine ni ya sekta ya maji, afya, elimu, barabara za jamii, umeme na uchumi.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: