MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 5 October 2015

TAARIFA KUHUSU DR. ABDALAH KIGODA



Taarifa kwa Vyombo vya Habari;

Tumepata taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara amefariki dunia nchini India alikokuwa anatibiwa.

Tunapenda kutoa taarifa Rasmi kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Dkt. Kigoda bado yupo nchini India Katika Hospitali ya Apollo katika Jiji la New Delhi anakoendelea kupatiwa matibabu.

Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015 na tangu kipindi hicho amend eleza kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo.

Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari nu Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa serikali.

Imetolewa na Assah Mwambene,Msemaji Mkuu wa serikali, na mtandao huu umeipata kwa mdau wa habari Yona Fares Maro.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: