MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 9 October 2015

TAARIFA YA KIFO CHA MGOMBEA UBUNGE ARUSHA

Aliyekuwa mgombea ubunge wa (ACT) Ndg. Estomih J. Mallah

Ni taarifa iliyoufikia mtandao huu kuhusu mgombea huyo wa Arusha mjini kupitia ACT, inasema kuwa  Ndugu Estomih Malla amefariki dunia katika hospitali ya KCMC Moshi.
Ndugu Malla alipelekwa KCMC jana mchana kutokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha mjini baada ya kulazwa hapo kwa siku mbili kwa sababu ya kupata tatizo la shinikizo la juu la damu.

Hali hiyo ilimtokea siku ya tarehe 6/10/2015 baada ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni, ambapo alilalamika kusikia kizunguzungu na baadae kukimbizwa hospital ya St Thomas ambapo madaktari wa pale walisema ndugu Malla anasumbuliwa na uchovu na hivyo anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu. 

Awali alikuwa Naibu Meya wa Jiji la Arusha na diwani wa kata ya Kimandolu, kupitia CHADEMA, ambapo alifukuzwa na chama hicho baada ya kuvunja ukimya na kumtaka aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa na viongozi wenzake kuacha kuwadanganya wananchi wa Arusha na Watanzania kuhusu sakata la umeya wa Arusha kwa madai kuwa hakuna tena njia ya kumtengua nafasi hiyo meya wa CCM, Gaudance Lyimo aliyepo madarakani. 

Na Mwanaharakati.

No comments: