.Haioneshi marekebisho ya mikoa mipya,
.Wachapishaji wauzaji kukamatwa,
.Yasema hakuna mgogoro na Malawi.
katika baadhi ya maeneo.
Mkurugenzi wa habari maelezo
ambaye ni msemaji wa serikali ASSAH MWAMBENE, amesema kuwa serikali ilizindua
ramani mpya na sahihi, ambayo inaonesha uwepo wa mikoa mipya ya SIMIYU, GEITA
na MANYARA, pamoja na kuonesha mipaka ya eneo la ziwa Nyasa na Tanganyika.
Amesema kuwa siku za karibuni baadhi
ya vyombo vya habari yakiwamo magazeti ya Mzalendo, Citizen, Mwananchi na
Wajibika yalitumia ramani isiyosahihi katika taarifa zake, na serikali inaweza
kuvichukulia hatua kwa mujibu wa sheria wakati wowote.
Wakati huo huo, amezungumzia
mgogoro wa ziwa Nyasa kati ya Tanzania na
Malawi, kuwa ukubwa wa Tanzania ni pamoja na eneo la ziwa Nyasa, kwani Malawi ina eneo lake katika ziwa hilo na
hakuna mkanganyiko tena kwani Tanzania inahudumia eneo lake na Malawi la kwake
kwasababu nchi zilikwisha kaa pamoja na kutoa maelezo na shughuli zinaendelea
kawaida.
Itakumbukwa kuwa ramani ya Tanzania,
afrika na dunia imekuwa ikiuzwa kiholela na wafanyabaisha mbalimbali nchini,
jambo ambalo serikali imewataka kufuata taratibu za upatikanaji wa ramani iliyo
sahihi kwenye mamlaka husika, kama wanataka kuendelea na biashara hiyo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment