Ni katika ukumbi wa Ikulu ambapo Ernest Mangu ambaye uteuzi wake umetenguliwa, yupo katika orodha ya viongozi wa polisi walioudhuria katika hafla hiyo, tayari kushuudia mteule akiwa kiapo...
Kiapo hicho kinajiri siku moja baada ya rais Joseph Magufuli kumteua jana jumapili kushika nafasi hiyo na kueleza kuwa Ernest Magu atapangiwa nafasi nyingine.
Jana mei 28/2017 Rais Magufuli alifanya mabadiliko kwenye jeshi la polisi nchini kwa kutengua uteuzi wa aliyekua mkuu wa jeshi hilo, Ernest Mangu, nafasi ambayo alitumikia tangau awamu ya nne chini aliyekuwa rais wakati huo Jakaya Mrisho Kikwete.
IGP Sirro alikuwa kamishna wa polisi na kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam, aliwahi kuwa kamanda wa polisi mkoani Mwanza kama alivyo Ernest Mangu aliyewahi kupitia mkoani humo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment