Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Kizilamuyaga
kata Kimwani wilayani Muleba, ameuawa
kwa kushambuliwa na kitu chenye ncha kali.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao
huu kwa njia ya simu, mwenyekiti wa kijiji cha Kizilanuyaga Bw. Adrian Philipo,
amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Ester Anaseti
mwenye umri wa miaka 30, ambaye anasadikiwa kuuawa na mtu anayesadikiwa kuwa
shemeji yake ambaye jina lake limehifadhiwa, usiku wa kuamkia jana jumapili.
Kamanda wa polisi mkoani Kagera Agustine Olomi, amesema hajapokea taarifa za mauaji hayo na ameahidi kutoa taarifa kamili baada ya kupokea undani wa tukio hilo, kutoka kwa mkuu wa polisi wa wilaya ya Muleba.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment