Waziri wa maliasili na utalii Prof.Jumanne Magembe leo
amefanya ziara yake ya siku moja mkoani Kagera kwa lengo la kueleza msimamo wa
serikali juu ya wanaoingiza mifugo katika hifadhi za mistu na mapori ya akiba.
Akiwa wilayani Biharamulo Prof.Magembe amesema kuwa hawataruhusu
tena mifugo kurudi ndani ya hifadhi,na watahakikisha ndani ya wiki mbili au
tatu wanapitisha ndege zenye rubani na ambazo hazina rubani ili kuhakikisha
hakuna mtu anayeingiza mifugo ndani ya hifadhi hizo.
Aidha amesema kuwa wakikuta mtu ameingia kwenye
hifadhi,watamuondoa pamoja na msimamizi wa eneo hilo na familia yake yote ili mbegu mbaya isibaki katika kuhifadhi
wanyamapori.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment