Nicolaus Mac (None Association Movement) KWA MATANGAZO YA REDIO NA TV WASILIANA NASI KWA +255767814844- nicolausngaiza@gmail.com.
Friday, 12 May 2017
SAFARI ZIMEKWAMA BUKOBA BAADA YA BARABARA YA BUKOBA DAR ES SALAAM KUMEGUKA
Wakala wa barabara nchini TANROADS mkoani Kagera, umepeleka mkandarasi katika barabara kuu ya Bukoba kwenda Muleba iliyomeguka na kushindwa kupitika, ili kuanza kazi ya ujenzi maramoja.
Akizungumza na mwandishi wa kituo hiki katika eneo la Bulila kijiji Kanazi kata Kemondo Bukoba vijijini, meneja wa TANROADS mkoani humo mhandisi Andrew Kasamwa, amesema kuwa wamechukua hatua za awali kuwaelekeza watumiaji kupitia barabara ya Kanazi kutokea Kanyinya, huku mkandarasi akianza kazi ya ukarabati kwa kuweka daraja kwenye eneo lililoharibika.
Amemtaja mkandarasi aliyekabidhiwa kazi hiyo kuwa wa kampuni ya ABEMULO, na kuwa wamemtaka akamilishe kazi hiyo haraka, kutokana na umuhimu wa barabara hiyo kuu kama kiunganishi cha mkoa wa Kagera na mikoa mingine nchini.
Badhi ya wananchi wa eneo hilo, wamesema kuwa Calvat iliyosombwa na maji ya mvua iliyonyesha kuanzia usiku wa kumakia leo, ilikuwa imeanza kuwa na nyufa, huku mtendaji wa kata hiyo Silianus Sostenes akisema kuwa tatizo kubwa limetokana na uchafu uliokuwa umeziba na kusababisha maji yaanze kupita pembeni.
Gharama za matengenezo ya eneo hilo zitatolewa baada ya tathmini kamili kufanywa na kamati ya ujenzi na vikosi vya ulinzi na usalama.
Na Mwanaharakati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment