Nicolaus Mac (None Association Movement) KWA MATANGAZO YA REDIO NA TV WASILIANA NASI KWA +255767814844- nicolausngaiza@gmail.com.
Saturday, 10 June 2017
157 WAHUKUMIWA KWA KUKWEPA KODI YA ARDHI NCHINI
Ofisi ya Kamishna wa ardhi Kanda ya Mgharibi, imewafikisha wadaiwa sugu wa kodi za ardhi 157 katika Mahakama za ardhi za mikoa ya Tabora na Kigoma, baada ya kushindwa kulipa kodi hizo kwa wakati, ili kuipa Mahakama jukumu la kutoa uamuzi wa kukamata mali zao na kuzipiga mnada.
Ni wakazi wa mikoa miwili ya Tabora na Kigoma, walijikuta wakiangukia mikononi mwa Mahakama hiyo mkoani hapa, ili kulipa deni la pango la ardhi ambalo hawajalipa kwa muda mrefu.
Kaimu Kamishna wa Ardhi kanda ya Magharibi Bw. Idrissa Kayera amesema kuwa Wakazi hao waliokuwa wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni 800 ambapo baada ya kufikishwa mahakamani wameweza kulipa kiasi cha shilingi milioni 645 sawa na asilimia 84 (84%) ya deni.
Baada ya hatua hiyo kukamilika, zoezi hilo litahamia katika Halmashauri nyingine Ishirini na saba zilizopo Kanda ya Magharibi, ambapo mikoa ya Shinyanga na Katavi, itafuata baada ya kutajwa kuwepo na wakwepaji kodi wengi.
Wakati zoezi hilo likiendelea baadhi ya watu waliofikishwa Mahakamani hapo, wakaelezea masikitiko yao kwa Serikali kuwapa muda mfupi wa kulipa madeni hayo ambao ni notisi ya siku kumi na nne zilizowekwa kisheria kwa mdaiwa kulipa deni lake kabla hatua za kisheria kufuatia.
Na Mwanaharakati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment