BUKOBA
Kwaya ya Tumain Jipya ya kanisa la Lutheran Kashura lililopo
ndani ya manispaa ya Bukoba imeezindua album yake jana kwa mara ya kwanza tangu ilipoanzishwa mwaka 2012 ikiwa
na wanakwaya kumi na wanne.
Kufikia jana kyaya hiyo ilikuwa tayari na wanakwaya 29,na
wamefanikiwa kurecord album yao kwa gharama ya Tsh millioni 6,ambapo katika
uzinduzi huo wamebainisha changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni uhaba wa fedha
kwa ajili ya kununua vifaa vya kuendeleza kwaya yao ambayo ni kiasi cha
shilingi milioni nane laki moja na elfu hamsini.
Akizindua Album hiyo meya wa manispaa ya Bukoba Chief
Kalumna,amewapongeza kwa kujitoa kuubili injili kupitia nyimbo ikiwa ni
sambamba na kuwawezesha zaidi ya laki nne huku akiongoza alambee kwa wadau na
washirika katika kuwezesha kwaya hiyo.
Kupitia alambee hiyo wamefanikiwa kupata fedha taslimu
Tsh.milioni mbili laki mbili na elfu tatu na ahadi ya shilingi millioni mbili
na elfu ishirini na tisa.
No comments:
Post a Comment