MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday 28 June 2017

AUDIO; TAKUKURU YASHIKILIA WANNE KWA KUTOZA PESA UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KAGERA



Mtendaji wa kata ya Bakoba katika manispaa ya Bukoba na wengine watatu, wanashikiliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani Kagera, kwa kuwatoza wananchi shilingi elfu tano katika uandikishaji wa vitambulisho vya taifa.

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, mkuu wa Takukuru mkoani Kagera Joseph Mwaiswelo, amesema kuwa  pamoja na kukamatwa kwa mtendaji huyo, pia inawashikiria watu watatu na wanaendelea kuhojiwa.


Amemtaja mtendaji huyo kuwa Marco Mgoe, huku akisisitiza kuwa majina ya wengine yanahifadhiwa kwa sababu za uchunguzi, na kuwa wanatuhumiwa kwa kutoza wananchi shilingi elfu tano kwa ajili ya kupewa fomu za vitambulisho vya taifa wakati wa uandikishaji unaoendelea.

Amesema kuwa katika uandikishaji huo, fomu zinatolewa bure na serikali, hivyo wananchi wasidanganyike kutozwa pesa bila ufafanuzi wa kazi yake.
Mwaiswelo amesema kuwa wanaendelea na kuwahoji watuhumiwa, na ikiwa upelelezi utakamilika watu hao watafikishwa mahakamani.
 

Na Mwanaharakati.

No comments: