Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kamizirente kata Rwamishenye
manispaa ya Bukoba maisha yao yapo matatani kutokana ubovu wa miundombinu
hususani eneo ilipofungwa Transfoma ya kusambaza umeme ndani ya mtaa huo.
Barabara ya mtaa huo imeharibiwa na mvua,hali iliyosababisha
kuwepo kwa shimo kubwa ambalo linmawapa wasiwasi wakazi wa maeneo hayo na
watumiaji wa barabara hiyo kwani mtu akianguka ghafla ndani ya shimo hilo
asilimia za kunusurika ni chache.
Kufuatia hali hiyo majirani wameiomba serikali kuchukua
hatua za haraka kufukia shimo hilo ili kuweka maisha yao katika hali ya usalama,kwani
lipo eneo ambalo linatumiwa na watu
wengi wakiwemo wanaofuata maji katika mto wa Kamizilente.
JIONEE PICHA MBALIMBALI ZA SHIMO HILO…………………………….......................
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment