BUKOBA
Kufuatia vitendo vya uhalifu vinavyoendelea katika maeneo
mbalimbali nchini Tanzania,mkoa wa Kagera umefanikiwa kufungua majalada ya
mauaji zaidi ya 140 kwa mwaka 2016 kitendo kinachodhihirisha utendaji mzuri wa
watumishi wa mahakama
Wakili wa serikali mkuu mfawidhi wa ofisi ya mwanasheria
mkuu wa serikali mkoa wa Kagera Hashimu Ngole amesema kuwa alipoingia mkoani
Kagera mwaka 2015 alikuta kesi za tangu 2008 hazijafunguliwa majalada,kitendo
kilichompelekea kuweka mikakati na mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Kagera ili
kuhakikisha kesi zinafanyiwa upelelezi na zinafunguliwa kwa uharaka.
Aidha amesema “mwaka
jana 2016 ofisi yangu ilifanikiwa kufungua majalada ya mauaji kwenye mahakama
kuu kufikia zaidi ya 140,na hii ni record katika nchi ambapo sio kitu rahisi kukipata”
Pia amezitaja changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni pamoja
na malipo ya mashahidi wao kitendo kinachowakatisha tama baadhi ya mashahidi
huku akisema kuwa kiutaratibu na kisheria wanaotakiwa kulipa gharama hizo ni
mahakama.
MWISHO
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment