Chanamoto ya uhaba wa maji imeendelea katika maeneo mbalimbali
mkoani Kagera hali iliyosababishwa na baadhi ya vyanzo vya maji kukauka na
kupelekea wananchi kutegemea chanzo kimoja.
Hali hiyo imewakuta pia baadhi ya wananchi wa wilaya Muleba
kata ya Nshamba ambao wanahudumiwa na mto wa {Nyina Eshamba}ambao wamesema kuwa
wanatumia zaidi ya kilometa tano kufuata
maji ikiwa ni sambamba na mto huo kuwa na watu wengi kitendo kinachopelekea
kutumia muda mrefu katika maeneo hayo na shughuli nyingine kukwama.
Aidha wamesema kuwa wanakabiliwa pia na changamoto ya uchakavu wa mabomba ya mto
huo wanaoutegemea kitendo kinachosababisha wananchi kupata maji machafu.
Sanjali na hayo wameiomba serikali kupitia uongozi wao
kuwasaidia juu ya changamoto hizo wanazokumbana nazo kwani ni sehemu mojawapo
inayopelekea kukwama kwa kwa shughuli za maendeleo katika Taifa letu.
PICHA 4; SHUGHULI YA KUCHOTA MAJI IKIENDELEA {NYINA ESHAMBA}
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment