Watumishi katika ngazi za serikali za mitaa wametakiwa kuwa makini na kutunza vizuri kumbukumbu za mapokezi na matumizi ya fedha za umma zinazopelekwa na serikali kwenye vituo vyao vya kazi ambapo kuanzia julai mosi mwaka huu fedha zitapelekwa moja kwa moja kuliko ilivyokuwa zamani ambapo zilikuwa zinapitishwa katika halmashauri ndo zipelekwe vituo husika.
Wito huo umetolewa na mkurugenzi mtendaji wa manisapaa ya
Bukoba Erasto Mfugale katika ufunguzi wa
mafunzo kwa maafisa elimu kata na wakuu wa vituo vya afya katika halmashauri za
wilaya hiyo ambapo amesema mfumo huo utakuwa unafanana kwa nchi nzima na hivyo
utasaidia kuondoa upotevu wa kumbukumbu za kiuhasibu zilizokuwepo hapo awali.
Aidha amewasihi watumishi hao kuhakikisha wanatekeleza
majukumu yao kwa umakini,na kutumia elimu watakayoipata ndani ya semina hiyo
kwa wenzao na hatimaye watakuwa wamelisaidia taifa kusonga mbele kimaendeleo.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment