MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 28 January 2014

MMOJA AFUMWA AKILA URODA NA KUKU

Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo ametiwa mbaroni na maafisa wa polisi mjini kisumu baada ya kudaiwa kushiriki kitendo kisicho cha kawaida na kuku. Inadaiwa mwanamume huyo amekuwa na mazoea ya kutekeleza kitendo hicho. Ni tukio lililotokea mwishoni mwa mwaka jana mjini Kisumu. 

MWANA HARAKATI

ALIVYOKUFA MCD WA TWANGA PEPETA




Sudi Mohamed, 'MCD' (pichani, juu na chini) ambaye ni mpinga tumba maarufu nchini Tanzania amefariki dunia usiku huu akiwa Moshi ambako alikwenda kwa ajili ya matiabu zaidi yapata miezi mitatu iliyopita. Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa Bendi ya Twanga Pepeta, Meneja Hassani, MCD alipelekewa nauli ya kurudi jijini Dar esalaam leo ili arejee kesho lakini mauti yakamfika usiku mida ya saa tano na nusu. MCD amewahi kupiga katika bendi kadhaa za muziki wa dansi ikiwemo Mashujaa Band na African Stars ambako alirejea tena. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi - ameen!

MWANA HARAKATI

AL SIS KUGOMBEA URAIS MISRI




Viongozi wa kijeshi nchini Misri wamekubaliana Mkuu wa jeshi ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi Abdel Fattah Al Sisi kuwania Urais katika Uchaguzi unaotarajiwa miezi michache ijayo.
Field-Marshal al-Sisi anatarajiwa kujiuzulu kutoka jeshini na kutangaza azma yake ya kuwania urais siku chache zijazo.
Waandishi wa habari wamesema mwanajeshi huyo anapigiwa upatu kushinda kwa urahisi katika uchaguzi unaotarajiwa hapo Aprili ambapo hana upinzani mkubwa.
Al Sisi anaaminika kuchangia pakubwa katika kumuondoa madarakani Rais Mohammed Mosri mwaka jana kufuatia maandamano makubwa dhidi yake.

Mikutano ya hadhara ilifanyika wikendi hii huku kukiwa na wito wa kumtaka Bw. Al Sisi kuwania Urais.
Binafsi Al Sisi hajatangaza kugombea lakini kumekua na taarifa kwamba alikua akijitayarisha kujitosa katika kinyang'anyiro cha kuongoza Misri.
Maelfu ya raia walikusanyika katika medani ya Tahiri hapo Jumamosi na kumtaka mkuu wa jeshi kuwania Urais.

Hapo Jumapili Kaimu Rais Adly Mansur alitangaza kwamba uchaguzi wa Rais utafanyika kabla ya kuwachagua wabunge. Wadadisi waliona tangazo hilo kama kumpa nafasi Al Sisi kugombea Urais. Wafuasi wake wamesema Misri inahitaji kiongozi mkali kama yeye.

Kwa sasa dalili zote ni kwamba Mkuu huyo wa jeshi atashinda kwa urahisi. Hata hivyo wapinzani wake wanaonya huenda Misri ikarejea katika utawala wa kiimla ambao uliondolewa na maandamano ya raia miaka mitatu iliyopita.

MWANA HARAKATI

TAKRIBANI WATU 583 WAMEATHIRIKA NA MAFURIKO YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA KATIKA KATA YA MPUNGUZI MKOANI DODOMA NA KUSABABISHA NYUMBA 146 KUANGUKA .




Diwani wa kata ya  mpunguzi mh john Matonya ameseama pamoja na idadi hiyo ya nyumba zilizo anguka bado nyingine zinaendelea kuanguka .
Aidha mh matonya amesema miundombinu mibovu ndio chanzo cha mafuriko hayo kutokana na kujengwa bila kiwango kizuri.
Hata hivyo mh matonya ameomba miundombinu iboreshwe ili kuondoa adha ya mafuriko wakati mvua zinaponyesha.

WAMILIKI WA MITANDAO YA SIMU   ZA MKONONI  TANZANIA  WAMEELEZA SABABU ZINAZOPELEKEA  WAO KUSHINDWA  KUWEKA  MINARA  YA SIMU KATIKA  MAENEO YA VIJIJINI

Hayo yamejiri mara baada ya wakazi wa kijiji cha solowu wilayani  chamwino kulalamikia ukosefu wa  mawasiliano ya mitandao ya simu  kwa  muda mrefu .

Mfanyakazi wa  mtandao wa  zantel Bw  Brayan Donard amesema   ukosefu wa miundombinu  vijijini ndo sababu kubwa   inayowapelekea wao kushindwa  kuwafikia  wakazi wa  maeneo hayo.

Aidha Bwana Brayani ameongezea kuwa  wana malengo ya kuwafika watanzania wote ila kwa sasa wameanza na wakazi wa Dodoma mjini  na wanaelekea  vijijini.

Sanjari na hayo  amewataka wakazi  wa maeneo ambayo  yamekuwa  yana matatizo ya mtandao  wawe  wavumilivu   kwani wanawakumbuka na muda ukifika watawafikia

DIWANI WA KATA YA CHILONWA WILAYANI CHAMWINO AMEITAKA SERIKALI KUJENGA DARAJA LA CHILONWA LILILOSABABISHA  WATU WATATU KUPOTEZA MAISHA KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
Mh Yaledi Sinon  amesema tangu kutokea kwa tukio hilo mpaka sasa hakuna harakati zinazofanyika baada ya meneja wa mkoa kuahidi kutafuta jitihada za matengenezo.

Aidha mh  Sinoni amesema tangu kutokea tukio hilo  mpaka hivi sasa hakuna kiongozi yeyote aliefika  hapo kwa ajili ya kutatua kero hiyo.

Hata hivyo ameomba madereva kuwa makini katika daraja hilo kutokana na kuendelea kunyesha kwa mvua na kuwataka makandarasi kutengeneza daraja hilo.

ZAIDI YA MAGARI 1,000 YAMEKWAMA KWENYE BARABARA KUU YA MWANZA  KWENDA  DAR ES SALAAM KATIKA KATA YA MIGUWA, WILAYANI NZEGA, KUTOKANA UTEKAJI WA MALORI ULIOFANYWA HIVI KARIBUNI.

Madereva wamegoma kuondoa magari yao baada ya kukasirishwa na kitendo cha polisi wa Nzega kushindwa kuwasaidia wakati walipotekwa.

Kutokana na tukio hilo,madereva wamegoma kuondoa magari yao na kusababisha mabasi ya abiria na malori ya mizigo kukwama wakati abiria wapatao 3,000 wakitaabika kwa kukosa chakula na maji.

Aidha Madereva hao wameapa kutoondoa magari hayo hadi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa watakapofika kwenye eneo hilo ili kusikiliza kilio chao.

Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nzega, Emmanuel Mihayo amesema watu wamejeruhiwa vibaya kwenye utekaji huo kwa kukatwa masikio na kutobolewa macho.

WATU WANNE WAMEPOTEZA MAISHA KWA KUSOMBWA NA MAJI MKOANI  HAPA , KUTOKANA NA MVUA ZINAZO ENDELEA KUNYESHA NCHINI.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime amesema watu hao wanatoka maeneo tofauti lakini vifo vyao vimetokea kwenye mito inayotiririsha maji kwa msimu.

Katika  tukio la hivi karibuni mkazi mmoja wa kijiji cha Mpinga mwenye umri wa miaka 55 amefariki baada ya kutumbukia kwenye mto Mpinga ambao ni wa msimu.

Kamanda Misime amesema tukio jingine limetokea  mwanzoni mwa wiki iliyopita, ambapo  watu wanne walitumbukia na gari waliyokuwa wakisafiria  katika mto Chinyasungwi, kijiji cha Mahampa, Wilayani  Chamwino na watatu kati yao walikufa huku mmoja akiokolewa.
 

MWANA HARAKATI

KIFO CHA MZEE DUDE


Msanii wa kundi la Futuhi Mzee Dude amefariki dunia Leo mida ya saa kumi na moja jion.
Habari zinasema kuwa alizidiwa jana Jumapili na kukimbizwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza 

MWANA HARAKATI

Monday, 27 January 2014

NI CHADEMA NDANI YA BEYA LEO

 


Chini; Wananchi wa mji wa Njombe na vitongoji wakiwa katika mkutano wa hadhara wa Operesehni M4C Pamoja Daima, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika mjini Njombe jana.



Picha chini ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Cadema), Dk. Willibrod Slaa akimnadi mgombea udiwani katika Kata ya Njombe Mjini kupitia chama hicho, Agrey Mtamba, wakati wa mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Njombe jana.

MWANA HARAKATI