MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 29 November 2011

Maadhimisho miaka 50 ya uhuru mkoani kagera yapambwa na wanafunzi. Maonesho hayo yalianzia maandamano katika kata ya rwamishenye yakiongozwa na wanafunzi wenyewe ambapo kufikia kona ya kyakairabwa darajani walikutana na trafik (askari wa usalama barabarani) wakaanza kuwapanga ni jinsi gani wataingia uwanjani kyakairabwa.

Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa kagera katika maadhimisho hayo lakini kwa hakika yalihudhuliwa na wanafunzi kwa wingi ambapo watu wazima wachache sana waliojitokeza walizungumza nami wakadai hawana maslahi na hawaoni cha kuwakusanya kutokana na kwamba serikali madarakani ndiyo inafaida ma maadhimisho si wananchi hivyo hakuna haja ya kuudhulia.

Meya wa manispaa ya Bukoba Bwana ANATOL AMAN alihijiwa nami moja kwamoja akakiri uchache wa wa raia hao lakini akatoa sababu kuwa wamekosekana kwasababu ni siku za kazi na kutokana na uchumi wananchoi wapo kwenye shughuli za utafutaji.

Wanafunzi wenyewe walisema wamelazimishwa na walimu na katika shule ya Buhembe Sec School waliandakwa majina ambaye hakufika atapewa adhabu.


Wednesday, 23 November 2011

 Wanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi ZAMZAM mjini BUKOBA wakivua samaki katika mto wenye maji machafu wa KANONI karibu kabisa na ofisi za Manispaa, muda wa saa tano asubuhi ambapo walitakiwa kuwa darasani.
 Ni jambo la kusikitisha kuona wazazi na walezi wakiwakuta watu hawa katika mazingira yanamna hiyo lakini hakuna anayekemea jambo hilo, je walimu hawajiulizi kwamba wanafunzi hawa wako wapi katika muda wa kuwa darasani?
 Huyu siyo kwamba amepumzika, ni mtu ambaye kafa baada ya kipigo kutoka kwa raia kwa mujibu wa vyanzo vyetu. Jamaa aliyefahamika kwa jina moja tu la NURU na inasemekana alikuwa akiishi katika vichaka vya NYAKANYASI mjini Bukoba, amekutwa amekufa karibu kabisa na daraja linalotenganisha mtaa wa nyakanyasi na USWAHILINI mjini Bukoba.
Miongoni mwa waliskia purkushani za usiku wakti wananchi wakitoa kichapo, wanasema waliskia sauti zikisema kama ndizi lakini hawakujua kulichoendelea.
Pembeni ni mizigo ya nguo inayosadikiwa kuwa ni ya wizi. Kumekuwa na matukio ya mauaji mjini bukoba ambapo m,apema mwezi uliopita mwanamke mmoja aliyefahmika kwa jina moja la NYANGOMA alikutwa amekufa katika mtaa wa BUYEKERA kata BAKOBA mjini BUKOBA wakti huo akiwa amevuliwa nguo yake ya ndani (chupi) na imetupwa pembeni

Friday, 11 November 2011

ABIRIA WAKIRUDI KWENYE BASI BAADA YA KUCHIMBA DAWA MENEO YA CHATO.

Kuchimba dawa unapokuwa unasafiri katika basi kwa masafa marefu ni muhimu kwa ajili ya afya ya mwanadamu kwani safari zingine ni ndefu kutoka dar hadi bukoba au bukoba-dar, lakini ni kwamba uchimbaji huo wa dwa hauzingatii usafi wa mazingira.

Wanaposimamisha magari kwa ajili ya uchimbaji huo wa dawa pia umwaga uchafu wote unaokuwa ndani ya gari, si vibaya kufanya hivyo lakini jamani kumekuwa na kumwaga taka hizo maeneo yasiyofaa kama maeneo ya mitaro ya kusafisha maji ambayo inatakiwa kuwa safi muda wote
Ni mwezeshaji wa mfuko wa waandishi habari tanzania(TMF) Bwana JAPHET SANGA akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa DODOMA.

Amesisitiza waandishi kukamilisha kazi wanazoombea pesa kutoka TMF ili kuhimarisha uhaminifu katika mfuko huo ili utakapofunguliwa muhula mwingine mwaka 2012 waweze kupata ruzuku kwa urahisi.

TMF mwaka kesho 2012 inampango wa kurekebisha taratibu tofauti na za sasa ili kumwezesha mwandishi kupata ruzuku kwa haraka baada ya kuomba na wakti huo bwana SANGA akishauri kuwa kuanzia hapo TMF itakuwa na uataratibu wa kutomwonea mtu huruma ya kumpa pesa kama ataonekana kutokujali kazi yake ipasavyo.

Kuanzia mwishoni mwa novemba TMF itafunga muhula na kutoatoa ruzuku hadi mwezi march 2011.
NI WAANDISHI HABARI WAKIMSIKILIZA MWALIMU MWEZESHAJI(MENTOR) ALIYEVALIA KOFIA NA KOTI YA DRAFTI, MHARIRI  NDIMALA TEGAMBWAGE. 


BASI LINAPOSIMAMA AJILI YA KUCHIMBA DAWA.

Ni katika barabar ya Tabora Dar Wilayani IRAMBA katika maeneo ya MISIGIRI ambapo inaonekana kila mara gari hili pichani usimama hapa hili abiria wachimbe dawa lakini cha ajabu pamoja na uchimbaji huo wa dawa, wenye gari umwaga uchafu kama makopo ya soda na mifuko mbalimbali katika mtaro huu inavyooneka. Sasa je ukujaa mtaro huu itakuwaje?

Friday, 4 November 2011

AFISA MAWASILIANO TACAIDS Bw RICHARD J. NGAIZA na MENEJA MAHUSIANO TACAIDS GRORY MZIRAY.

Waandishi habari wametakiwa kushirikisha jamii wanayoihudumia ili kushiriki mawazo na kujua matatizo yao kwa urahisi.

Hayo yamesemwa na meneja mahusiano wa TACAIDS Bi GRORY MZIRAY katika semina ya siku mbili kwa waandishi habari kanda ya ziwa kuhusu maandalizi ya vipindi vinavyohusu ugonjwa wa UKIMWI.

Amesema ugonjwa wa UKIMWI unaendelea kuwepo kwasababu ya wapenzi kuzoeana kwa muda mfupi, jambo linalopelekea kuacha kutumia kinga  baada ya kuwa pamoja katika mapenzi.

Naye Afisa mawasiliano TACAIDS Bwana RICHARD JOSEPH NGAIZA, amesema chombo cha habari cha ndani kinaifikia zaidi jamii ya eneo hilo kutokana na maelewano mazuri ya lugha inayotumika katika maeneo husika.

Semina hiyo ambayo inahitimishwa leo jijini Mwanza imeandaliwa na TACAIDS kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi habari wa vyombo vya ndani (Community Radio) katika kanda ya ziwa ili kuwawezesha kuandaa vipindi kwa ufasaha na ujumbe uweze kufika kwa jamii kwa haraka zaidi.