MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 19 May 2013

KUTOKA IKULU


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WARSHA YA WAZI KUJADILI MATOKEO YA UCHAMBUZI WA KINA WA MAENEO YA KIPAUMBELE YA KITAIFA
Katibu Mkuu Kiongozi atakuwa na Press Conference kesho, Jumatatu 20, Mei, 2013 saa 3 asubuhi katika Ukumbi wa mikutano wa mawasiliano – IKULU.
Tunaomba wahariri mtutumie majina ya waandishi na wapiga picha watakaokuja kuhudhuria shughuli hii. Press Conrefence hii itahusu miradi na program zitakazotekelezwa na Serikali kwa kipindi cha miaka mitatu (2013/14 hadi 2015/16) katika maeneo ya Kipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16)”. Miradi hiyo inatokana na uchambuzi wa kina uliofanywa na wataalamu wa kitanzania kwa kutumia mfumo mpya wa labs.
Huu ni mfumo mpya ambao Serikali imeuanzisha ili kuhakikisha ushirikishwaji mpana wa wadau na wananchi kwa ujumla katika utekelezeaji wa miradi ya kipaumbele ya kitaifa.
Tafadhali tunaomba mzingatie muda na karibuni sana

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
 19 Mei, 2013
 

MWANA HARAKATI

MCHUNGAJI MSIGWA; MBUNGE IRINGA MJINI AKAMATWA NA POLISI JUU YA MACHINGA KURUDISHWA WALIPOONDOLEWA.





Yamepigwa mabomu ya machozi baada ya Msigwa kufika eneo walipokuwa wafanyabiashara hao, na kuanza kusukuma gari lake, lakini mwanzoni walimlinda na polisi wakapata wakati mgumu kumkamata.  

Ikumbukwe kuwa hawa wamachinga wamepewa eneo maalumu la kufanyia biashara zao la Kitanzini na Mlandege, kwa sababu hapo wanapotaka kufanyia biashara sasa ni padogo na ni kero kwa wanachi kwani ni stendi kuu ya mabasi na pia kuna zile mashine kubwa tatu za kukoboa mpunga ambazo huwa zinajaa watu wengi na pia ni barabara ambayo ina muingiliano mkubwa.



MWANA HARAKATI

Monday, 6 May 2013

RAIS AKATIZA ZIARA YAKE NCHI ZA NJE.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.

Rais Kikwete aliyekuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, amelazimika kukatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.

Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika  eneo la Ahmadi mjini Kuwait. Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.

MWANA HARAKATI

MAFURIKO BUKOBA......

Mkuu wa wilaya ya Bukoba bi ZIPORAH PANGANI, ametoa taadhari kuwa watu watakaoendelea kukaa kwenye makazi yao selikari inawatoa kwa nguvu kwani wameshaambiwa wahame maeneo ya mabondeni hawataki.

Wakati huo wakazi wa Kyabitembe na Nshambya wameshindwa kuvuka kupitia Rwamishenye baada ya daraja walilokuwa wakitumia kusombwa na maji ya mvua zilizonyesha usiku kucha na kupelekea
Wananchi wa eneo hilo manispaa ya Bukoba, waishi kwa wasiwasi baada yam to kanoni unawaunganisha na kata ya rwamishenye, kujaa maji wakati hakuna daraja mbadala la kuvukia kufuata huduma muhimu.

Wakizungumza na harakati kwa nyakati tofauti, wananchi wameskitishwa na njia iliyowekwa kama daraja la kuvukia huku ikionekana itadondoka dakika yoyote ilihali ikiwa tishio kwa watoto na kulazimu wazazi kusubiria taarifa yoyote kuhusu watoto waliokwenda shule.

Wamesema kuwa wakati mwingine watoto wanashindwa kwenda shule wakihofia kudumbukia majini na kusababisha kukwamisha upatikanaji wa elimu.

Mto kanoni katika eneo hilo, unatenganisha kyabitembe n6a6 r6wamis6hen6y6e, ambapo hu6tum6ik6a na wananchi hasa wanafunzi wa shule za rwamishasha, na omumwani na maeneo mengine kama sokoni.
.
Biashara zimesimama ghafla katika mji huo wa Bukoba na taarifa za serikali zinaendelea kutolewa kupitia redio za mjini Bukoba.


MWANA HARAKATI

ARUSHA BOMU ILIKUWA HIVI



Taarifa zilizopo ni kwamba tukio limetokea kwenye saa tano asubuhi kwenye Kanisa Katoliki Olasiti Arusha ambapo lilikua linazinduliwa na mgeni rasmi ambae ni balozi wa Papa hapa Tanzania.
Inasemekana chanzo ni bomu la kurushwa na mtu ambae aliwasili kanisani hapo na kurusha hilo bomu muda mfupi tu baadae ambapo walioumia wamekimbizwa hospitali ya Mount Meru.




Taarifa za karibuni kabisa zinaeleza kuwa mtu mmoja amekufa kwenye mripuko uliotokea katika ufunguzi wa kanisa la Katoliki la Olasiti, kwenye kitongoje cha Arusha, Tanzania.
Watu kama 50 wamejeruhiwa.

Makamo wa rais wa Tanzania, Dr. Mohamed Gharib Bilal amewasili Arusha kwenda kupeleka pole ya serikali kwa viongozi wa kanisa na majeruhi.
Dr. Bilal alisema serikali ya Tanzania itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa inawapata watu waliohusika na mripuko huo.

Mtu mmoja amekamatwa lakini haikuelezwa ni nani au kama amehusika na kundi
MWANA HARAKATI