Kwa mujibu wa chanzo ambacho ni ndugu wa karibu
wa familia hiyo, siku moja baada ya msiba, mtoto huyo alitangaza kuwa gari hilo
ni lake na akaanza kutafuta madalali wa kuliuza gari hilo lakini akakwamishwa
na kukosekana kwa kadi ya gari.
“Yaani hawa watoto wa marehemu sijui wana nini jamani, hata arobaini ya baba
yao bado wameanza kushikana mashati, hii ni hatari sana. Huyo mmoja ndiyo
anajitapa kabisa kuwa gari ni la kwake na ameshaanza kutafuta mteja,” kilisema
chanzo chetu kwa masharti ya kutotajwa gazetini.
Mtoto wa marehemu, Mariam Gurumo ambaye alipoulizwa
kuhusu ishu hiyo, alisema: “Aliyekupa hizo taarifa ni muongo, hakuna ishu kama
hiyo. Kwanza bado tunaomboleza kifo cha baba yetu. Sasa tuuze gari na nyumba
ili iweje? Siyo kweli.
“Ni kweli kuna kesi ya nyumba ipo mahakamani lakini siyo nyumba hiyo
unayoisema. Unajua sisi watoto wa Gurumo tunataka kudhulumiwa nyumba iliyoachwa
na marehemu mama yetu iliyopo Ilala.
“Unajua huyu mjane wa marehemu, hakubahatika kupata mtoto, sisi mama yetu ni
marehemu na tulizaliwa wanne, mimi (Mariam), Mwalimu, Mwazani na Omary.
“Abdallah yeye ana mama mwingine lakini ni ndugu yetu wa damu. Kabla mama
hajafa, Gurumo alimjengea nyumba Ilala.
“Sasa mama yetu alipokufa, mdogo wake (jina tunalihifadhi) akawa anataka
kuiuza, hivi jana tu (Ijumaa) tumetoka mahakamani. Tumefungua kesi pale yenye
jalada namba RB/IL/112/2013 kuzuia nyumba kuuzwa. Tunashukuru mahakama
imeingilia kati vinginevyo tungedhulumiwa.
Naomba watu wasichanganye, nyumba yenye matatizo ni ya Ilala. Kuhusu gari, kwa
sasa bado hatujaamua chochote mpaka arobaini ipite,” alisema Mariam.
|
Mariam
Gurumo |
“Ni kweli
nyumba inauzwa. Hilo lilikuwa ni agizo la mume wangu kabla hajafariki,
aliniambia ni bora aiuze kabla hajafa kwani anawajua wanaye watanisumbua sana
pindi akifa.
“Tulianza kutafuta wateja miezi minne kabla Gurumo hajafa, bahati mbaya
ametangulia kabla hatujakamilisha hiyo kazi. Yeye alikuwa na lengo zuri la
kutaka atugawie kila mmoja chake ili akifa yasitokee haya yanayotaka kutokea.
“Unajua hii nyumba tumejenga na mume wangu, mimi nilikuwa mfanyabiashara na
tulisaidiana kabla hata hawa watoto hawajazaliwa lakini nashangaa wanataka
kunigeuka eti mimi sihusiki.”
“Naomba
serikali iingilie kati kwenye hili suala, nyumba wala gari viziuzwe kwanza.
Jamani hata eda sijamaliza mambo yameanza kuwa hivi.
Hao watoto wenyewe tangu tumzike baba yao hawajakanyaga hata hapa nyumbani
kunijulia hali, sijui wanafikiria nini kuhusu mimi, naomba mnisaidie nimalize
eda salama na mali zikiuzwa, basi na mimi nipewe staahili yangu,” alisema mjane
huyo kwa huzuni.
Na Mwanaharakati.