Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif
Rashidi akiwasha moja ya kati ya magari manne.
|
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif
Rashidi (kulia) akipokea ufunguo wa moja ya gari kutoka kwa mwakilishi wa
shirika la GLRA nchini Burchard Rwamtoga (kushoto) |
|
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif
Rashidi (kulia) akimkabidhi Mratibu wa huduma za kifua kikuu na ukoma mkoa wa
Kigoma Dkt. Deus Leonard (kushoto) moja kati ya magari manne yaliyokabidhiwa kwa Serikali. |
Mikoa ambayo imenufaika na msaada huo ni
pamoja na Tanga, Kigoma, na Mikoa ya Kanda Maalum ya Ilala na Kinondoni.
Akipokea msaada huo leo (Jumanne Agosti
26, 2014) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashidi (Mb) aliwataka
Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia kikamilifu matumizi ya vyombo hivyo vya
usafiri kwa kuvilinda na kuvitumia kulingana na malengo yaliyokusudiwa.
Dkt. Seif alisema kuwa vifaa hivyo
vimegawiwa kulingana na mgawanyo wa mikoa iliyoanishwa na Serikali katika Mpango
wa Taifa wa kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma.
Dkt. Seif alisema Mpango wa Taifa wa
kudhibiti kifua kikuu na ukoma umekuwa na mafanikio ambapo imeendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa wote
wa kifua kikuu na ukoma bila malipo katika hospitali na vituo vya huduma za
afya vya serikali na binafsi nchini.
Aidha, Dkt. Seif amesema kuwa Tanzania
imevuka malengo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kuponyesha asilimia 85 ya
wagonjwa wote wa kifua kikuu wanaoanza matibabu kila mwaka.
“Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania
imefikia viwango vya asilimia 88 ya kuwahudumia na kuwaponyesha wagonjwa hao
ambayo ni zaidi ya kiwango cha WHO” alisema Dkt Seif.
Dkt. Seif amesema kuwa kwa upande wa
ugonjwa wa ukoma, Serikali inaendelea kufanya kampeni katika mikoa ya Dar es
salaam, Dodoma, Kagera, Lindi, Morogoro, Mwanza, Pwani, Rukwa, Shinyanga,
Tabora na Tanga katika kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujikinga na ugonjwa
huo.
Kwa mujibu wa Dkt. Seif alisema wagonjwa
wapya wa ukoma waliogunduliwa mpaka sasa na kupatiwa tiba ni 23,667, na
Serikali tayari imetoa jozi 35,000 ya viatu maalumu kwa wagonjwa hao.
“Mpaka sasa tumeweza kufikia malengo ya
kimataifa ya kutokomeza ukoma kwa kuwa chini ya mgonjwa mmoja katika watu
10,000 na kufanya ugonjwa wa ukoma kuwa si tatizo kubwa la kiafya kwa jamii
nchini” alisema Dkt Rashid.
Naye mwakilishi wa shirika lisilo la
kiserikali la GLRA nchini Burchard Rwamtoga
aliusifu kwa ushirikiano uliodumu kwa miaka 37 baina ya Shirika hilo na
Serikali ya Tanzania katika mapambano ya magonjwa ya ukoma na kifua kikuu.
Aidha, Rwamtoga aliongeza kuwa Shirika la
GLRA hutoa wastani wa Tsh. Bilioni 1.3 kila mwaka kwa Serikali na kati ya fedha hizo kiasi cha Tsh.milioni
600 hutumika kwa ajili ya manunuzi ya vifaa vya usafirishaji ikiwemo magari, na
pikipiki kwa waratibu wa kifua kikuu na ukoma.
GLRA mbali na kutoa fedha kwa Serikali
pia tunaratibu mpango wa kuwajengea
uwezo wa kiutendaji waratibu wa mikoa ikiwemo kutoa mafunzo nje ya nchi kupitia
kituo cha ALERT kilichopo nchini Ethiopia, ambacho hujisihusha na mafunzo ya upasuaji
na kutoa visaidizi ikiwamo miguu bandia na baiskeli kwa wagonjwa.
Kwa upande wake Mratibu wa huduma za kifua
kikuu na ukoma mkoa wa Ilala Dkt. Mbarouk Seif ameishukuru Serikali kuupatia
mkoa huowake gari la wagonjwa na kuahidi kuwa Ofisi yake itahakikisha gari hilo
linawafikia na kuwahudumia wagonjwa kwa wakati.
Shirika la GLRA ilianza kusaidia wagonjwa
wa ukoma nchini mwaka 1959 na kupata usajili mwaka 1977 ambapo lilianza
kushirikiana na Mpango wa Kudhibiti kifua kikuu na ukoma (NTLP) nchini uliopo
chini ya Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamii.
Na Mwanaharakati.