MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 29 September 2014

NEWS ALERT!!! ASKOFU BAGONZA; WALIMU WAZUNGU KUNUSURU SAYANSI KARAGWE.

 Akizungumza mbele ya mgeni rasmi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bukoba mjini CCM Balozi Khamis Kagasheki, katika mahafali ya tano ya kidato cha nne katika shule inayomilikiwa na KKKT ya Bweranyange, askofu Bagonza amemwomba mbunge huyo kumsaidia kukamilisha usajili wao ili wasikwame kufundisha katika shule za kanisa hilo kunusuru wanafunzi wa sayansi.

Amesema kuwa alienda Sri Lanka kufanya mazungumzo, na kukubaliana na walimu kadhaa ambao kwa mujibu wake anataka kubadilisha mawazo na mtazamo wa elimu ya tanzania kupitia walimu kutoka nje, huku akisema kuwa walimu wa ndani waache kushinikiza mishaara mikubwa, kisa wanafundisha sayansi.

Katika mhafali hayo, wanafunzi 67 wa kike wamehitimu kidato cha nne, huku shule hiyo ikikabiliwa na mapungufu ya kompyuta, huduma ya maji na umeme, ambavyo mh. Kagasheki amesema ankwenda kuzungumza na rafiki zake, ili kuona jinsi ya kusaidia vitu hivyo, huku akiomba apewe bajeti yake.
Balozi Kagasheki, akifanyiwa utabiri na mwanafunzi kutaja na ni kitu gani ameshika mkononi wakati wa mchezo wa kuigiza..

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Balozi Kagasheki akikabidhi cheti kwa moja ya mwanafunzi muhitim.

Askofu Bagonza kushoto, akiongozana na Balozi Kagasheki katika ukaguzi wa mazingira ya shule hiyo ya wanafunzi wa kike,ambapo hatahivyo balozi ameoneshwa maabara ya shule hiyo inavyofanya kazi.
Na Mwanaharakati.

BREAKING NEWS!!!MJI WA BUKOBA HATARINI KUKUMBWA NA MAFURIKO.

 Mvua zilizonyesha jana katika mji huo na viunga vingine mkoani Kagera, imesababisha nyumba kadhaa kuzingirwa na maji, ambapo sababu kubwa inachangiwa na kuziba kwa mitaro, mito, pamoja na ujenzi holela, hasa katika kujenga kado kando ya mto Kanoni, unaokatiza katika mji huo.
Ni eneo la Miembeni, mkabala na ukumbi wa Disco Linas.

Ni mkabala na CRADB, chini ya Baa ya Oxygen katikati ya mji.

Hapa ni katika paking ya bank CRDB
Kituo cha mfuta Camel barabara ya Kashozi nacho ndani ya maji.

Daraja katika barabara ya Kashozi liko eneo la Migera.
Na Mwanaharakati.

NEWS ALERT!!! TIZEBA ELIMU LAZIMA IZINGATIWE



NAIBU  waziri  wa mawasiliano na uchukuzi  Dk  Charles Tizeba  ambaye  pia  ni mbunge wa jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema mkoani Mwanza amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwa kuwa elimu ndiyo urithi pekee.
Dk  Tizeba  ametoa  wito  huo  juzi katika  kata  ya  Nyehunge  wakati akikabidhi msaada wa vitabu elfu moja vya somo la Hisabati kwa walimu wakuu wa shule kumi na nane za sekondari katika jimbo la Buchosa.

Amesema  kuwa  lengo  la  kugawa  vitabu  hivyo  katika  shule  hizo  ni kuasaidia tatizo la upungufu wa vitabu mashuleni na kuwawezeasha wanafunzi kujisomea vizuri na hatimaye waweze kufanya vizuri katika mitiahani ya ya taifa.
 .
Dk  Tizeba  aliongeza  kuwa  vitabu    hivyo  vya  somo  la  hisabati ni kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili na kwamba vimegharimu shilingi milioni 9.

 Aidha  amewataka  walimu  wakuu  wa  shule  za  sekendari  jimboni  humo kuakikisha vitabu hivyo vinatunzwa kwa uangalifu mkubwa na umakini zaid.

 Mwalimu  mkuu  wa  shule  ya  sekondar Nyehunge  Rubhari
Benesta akisoma  risala  fupi  kwa  mbunge  wa jimbo  hilo
alisema   kuwa  wanafunzi  wa  shule  za  sekondari  katika  jimbo
wanaotoka  mbali  na  maeneo  ya  shule hizo wanaishi  katika
mazingira magumu ya upangaji kutokana na shule kutokuwa na hostel.
 
Naye afisa  elimu  vifaa na  takwimu  shule za  msingi
Wilayani  sengerem  Pius  Lwamimi  akishukuru  kwa  niaba ya  ofisa elimu idala ya sekondari Wilayani sengelema ameongeza DK Tizeba kwa msaada wa vitabu hivyo na kuwaomba wengine kuiga mfano huo.


Na Mwanaharakati.

KINACHOJIRI BUNGE LA KATIBA.

Mwenyekiti wa kamati uya uandishi ya Bunge hilo maalumu Mh ANDREW CHENGE, amesema kuwa marekebisho ya jalada la marekebisho ya rasimu ya katiba mpya hivyo anawakilisha kwa wajumbe tayari kuanza utaratibu wa upigaji kura.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba, Andrew Chenge  akisoma marekebisho katika jarada la rasimu, bungeni mjini Dodoma,  Septemba 27, 2014.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akiteta na Mjumbe wa Bunge hilo, Kingunge Ngombale Mwiru, bungeni mjini Dodoma Septemba .

Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu akiongoza kikao cha Bunge hilo Septemba.

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema  (kulia) na Hamad  Rashid (kushoto) wakiteta bungeni mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, John Momose Cheyo akichangia  bungeni mjini Dodoma

Na Mwanaharakati.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU 29 SEP 2014






Na Mwanaharakati.

BREAKING NEWS!!! BALOZI KAGASHEKI, KATIBA ISIWAGAWE WATANZANIA.



Na Mwanaharakati.

Friday, 26 September 2014

NEWS ALERT!!! MCHUNGAJI ATUMIA SADAKA KUSAIDIA UJENZI WA MAABARA BUKOBA

Mchungaji James

Hatahivyo mashirika, Taasisi na watu binafisi mkoani Kagera wameombwa kuendelea kuchangia katika miradi mbalimbali ya Maendeleo .


Wito huo umetolewa na mmoja wa wadau wa maendeleo manispaa ya Bukoba, MCHUNGAJI KING JAMES wa kanisa la ukombozi manispaa ya Bukoba wakati wa hafla ya kukabidhi mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara unaondelea kwa sasa.

Mchungaji JEMES  amesema kuwa amewiwa kutoa mchango huo, katika shule za manispaa zinazoendelea na ujenzi huo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha elimu hususan masomo ya sayansi.

Kulia ni mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi ZIPORAH PANGAN

Kutoka kushoto ni mkurugenzi manispaa, naibu meya Ngalinda, mchungaji James, mwenyekiti wa ccm wilaya, na afisa tarafa Abdon Khawa.



Ameongeza kuwa juhudi za serikali pekee hazitoshi katika kuwaletea wananchi maendeleo bali ni kushirikiana na wadau wote.

Akisoma risala wakati wa kupokea msaada huo mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba, ADOH MAPUNDA amesema kuwa msaada huo, umetolewa kwa wakati muafaka na kutaka msaada huo kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
 

Na Mwanaharakati.