MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 29 December 2014

HALI YA WASIWASI KUTOKEA UKAME MKOANI MOROGORO

Hali hiyoinajitokeza baada ya msimu wa mvua kubadilika kwa kupungua kiwango cha mvua, huku  milima yenye kuwa na unyevunyevu na baridi huku mawingu yakiwa karibu na milima hiyo, sasa vikitoweka, na jotokuongezeka.
Picha ikionesha mojaya eneo lililo bondeni, nje kidogo ya mji huo katika eneo la Nanenane ambapo miaka ya nyuma hapa palikuwa na maji na unyevu wa mara kwa mara.


 Hatahivyo baadhi ya mazao kama matunda ambayo yalikuwa yakipatikana kutokea upande wa pili wa milima inayoonekana kwenye picha chini Mgeta, sasa yanapatikana kwa shida na gharama iko juu, ambapo wakaazi wake wanasema tatizo uongozi umeshindwa kusimamiamatumizi ya maeneo na kusababisha baadhi ya wananchi kuvamilia milima hiyona kufanya shughuli za kilimo.
Taswira mji wa Morogoro eneo la soko la sabasaba na milima ikionekana kwa mbali kuwa miti imekatwa kwa kiasi kikubwa na mawingu ambayo yalikuwa yakitanda hayapo kabisa.

Na Mwanaharakati.

TAARIFA YA KAKA KUONA ALIYEZUA TAFLANI NA ATIMAYE MVUA KUNYESHA DAR ES SALAAM



Huyu ndiye Kakakuona aliyeonekana leo maeneo ya Kigamboni jijini Dar, 
Ambapo wananchi walimwekea maji, kisu, unga na pesa,huku taarifa za wanancnhi zikisema kuwa alijikunjua na kunywa maji mengi sana, akafuata unga na pesa, lakini wala akuelekea vilipokuwa panga na kisu. 

Watabiri wa mambo wanasema tutarajie mema mwakani.
 

Na Mwanaharakati.

Thursday, 25 December 2014

BREAKING NEWS!!! SAKATA LA MELI MV VICTORIA UBADHILIFU WABAINIKA UONGOZI WATIMULIWA WENGINE WAWEKWA KIPORO



Kutokana na meli ya Mv Victoria kukwama safari zake mara kwa mara na kuzua mjadala na hasara kwa abiria na wafanyabiashara, waziri wa uchukuzi HARISON MWAKYEMBE atimua uongozi mzima bandarini hapo na kuteua wapya.
Waliofukuzwa kazi ni Meneja mkuu Projest Kaija, na nafasi yake imechukuliwa na Fabian Mayenga.
Kaimu mhasibu mkuu Tito W.Mwambagi, nafasi yake kuchukuliwa na Beatus R. Rugalabamu, kaimu meneja masoko biashara, ameondolewa Cpt Obeid Nkongoki nafasi yake inachukuliwa na Cpt Winton Mwasa.

Aliyefukuzwa mwingine ni kaimu meneja wa tawi Mwanza Beatus T. Mghamba na kuingia Bwana Philemoni Bagambilana, Kaimu tawi Kigoma ameondolewa Bwana Abel Giliard na nafasi yake kuchukuliwa na Anthony Stephen, huku kaimu mwanasheria na menejautumishi anakuwa Fabian Mayenga baada ya kuondolewa Josephat Mshumbusi .

Meli hiyo imesimamishwa kutoa huduma ili ifanyiwe ukarabati wa kina, baada ya kubainika kuwa uongozi uliokuwapo ulikuwa ukiweka spare fake, na kusababisha adha kubwa kwa watumiaji.

Waliopewa onyo sima kwenye picha hii chini.
 
Uongozi mpya umeanza kazi tangu tarehe 18 Dec 2014.
 

Na Mwanaharakati.

Tuesday, 23 December 2014

KITISHO CHA USALAMA, POLISI AUAWA

Askari mmoja ameuawa na mwingine akiwa mahututi baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi kaskazini mwa Kenya.
Askari hao wa Kenya wanadaiwa kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la Al Shabaab.
Askari hao wa jeshi la polisi kikosi cha ziada walikutwa na kisa hicho mjini Wajir kaskazini mwa Kenya usiku wa kuamkia leo.
Na Mwanaharakati.

SOMA ALICHOSEMA PROF ANNA TIBAIJUKA KUPITIA MWANAE



Monday, 22 December 2014

BREAKING NEWS!!! RAIS KIKWETE AMTAKA WAZIRI TIBAIJUKA JIUZULU

Rais Kikwete ameeleza kuwa kupitia mazungumzo yake na waziri huyo, ameshamwambia apishe nafasi hiyo ili rais aweze kuchagua mwingine.
Na Mwanaharakati.

BREAKING NEWS!!! MTUHUMIWA WA EPA JOHNSON LUKAZA ASHINDA KESI, AACHILIWA HURU




Hukumu hiyo Imetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Edson Mkasimongwa aliyekuwa alisaidia na Hakimu Mkazi Pamela Mazengo.

Lukazaambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) alikuwa akitetewa na Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Mkasimogwa alisema Kesi hiyo ya Mwaka 2008 , Mahakama  imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili Na kupitia vielelezo
mbalimbali, Mahakama yake Imefikia uamuzi wa kuwaachiria huru
washitakiwa wote Wawili kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuleta
ushahidi thabiti ambao ungeishawishi Mahakama hiyo iwakute na hatia
washitakiwa Hao.


Na Mwanaharakati.

ALICHOSEMA CAG ALIYECHUNGUZA ESCROW HIKI HAPA



Hayo amesema leo jijini Dar es Salaam katika kupokea tuzo ya uadilifu kutoka kwa Kampuni ya Dream  Success Enterprises kutokana na kutambua umuhimu wa utendaji wake wa kazi.

Alisema kuwa mihimili mitatu isipojua mipaka yake itawaweka wananchi washindwe kujua uwepo wa mihimili hiyo na kufanya nchi ishindwe kutawalika kutokaka na mihimili hiyo kuwa na mianya ya kutoafikiana katika utendaji..

Utouh alisema kuna vitu hataweza kusahau katika ofisi ya CAG moja ni fedha zilizochotwa katika akaunti za nje (EPA) pamoja na ripoti ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini, David Jairo ambapo wabunge walishindwa kujua uhalali wa fedha zilizochangishwa  na Jairo na hakuna sheria yeyote iliyovunjwa.

“Tuzo hii nimepata lakini nimepita  katika kipindi ambacho jina la ufasadi limeweza kuzaliwa kutokana  na uchotaji wa fedha za EPA na kufanikisha zingine kuweza kurudi, nchi zingine huwa zinashindwa kabisa kurudisha fedha za namna hiyo”alisema Utouh.
 

Na Mwanaharakati.