. Baadhi ya wajumbe wazomewa,
. Waliokosa majibu ya wananchi
watimuliwa,
. Upigaji kura jumamosi tarehe 1.
Ni katika mikutano 12 ya kampeini za kuomba kura kwa watia
nia ya ubunge manispaa ya Bukoba, ambapo wamezunguka kwa pamoja kata 14 za
manispaa hiyo, huku baadhi ya wagombea wakizomewa, na wengine kuulizwa maswali
kuhusu walichofanya awali na wengine kuhusu dhuluma walizosimamia huku majibu
yakikosekana.
Jumla ya watia nia hao ni 8 ambapo kila mgombea amekumbana
na maswali, kuzomewa au kushnagiliwa, kulingana na anavyofahamika katika kazi
yake, na aliyeongoza kuzomewa na kukimbia mikutano alikuwa Anatory Aman, huku
Mjuni Kataraiya akizomewa baada ya kujibu swali kuwa anglau alitoa lift, baada
ya kuulizwa anachoweza kukumbukwa wakati akiwa mbunge.
George Lubaiyuka amejieleza kuwa amekuwa akifanya kazi za elimu kwa muda mrefu na sasa ni afisa elimu wilayani Misenyi, ameulizwa swali na kijana wa kata Ashai jinsi anavyoweza kusaidia kuondoa mkanganyiko katika ngazi ya ubunge ilhali kwenye sekta ya ualimu imekuwa ngumu huku walimu wakibainika kulalamika na yeye akiwa afisa elimu.
Anatory Amani aliwahi kuwa Meya na amesema kuwa yuko tayari kuwaletea maendeleo, lakini ameulizwa
swali na mmoja wa wajumbe kuwa ameongoza kuwa na kesi nyingi mahakamani huku akikataa maridhiano kama inavyoshauriwa kwenye chama chao, akipata nafasi ya ubunge hataongeza migogoro na hata kufarakanisha bunge?
amesema hana malalamiko na mchakato, ameshukuru wananchi kumpendekeza kuendelea kugombea lakini akitaja miradi mbalimbali aliyofanya huku kubwa akiwaomba wananchi wasiendeleze migogoro kuwa haki yao itapatikana kwa mujibu wa taratibu za nchi.
Bi Eriet ameomba kuwasaidia wananchi kwani akina mama wana huruma huku akisema kuwa mama
mwenye mimba hajui atajifungua mtoto gani, naye hajajua atafanya nini juu ya wananchi lakini wamchague ataleta maendeleo.
Mzee Joseph Kaijage, anasema yeye ni Born here here die here here, hivyo wampe kura hata ikitokea mambo yameharibika hawezi kuwakimbia wananchi watakaa na kutatua pamoja.
Yeye amezaliwa hapaha hapa na atafia hapa hapa hivyo matatizo ya wananchi anayajua na yuko tayari kuyatatua, lakini hawezi kuyatatua bila nguvu ya wananchi hivyo wamuunge mkono kumpa kura.
Bi Selestine Lwezaura, yeye ni mmoja wa akina mama aliyefanya kazi maeneo mbalimbali, hivyo amesema
kazi ya ubunge anaweza kuifanya kusaidia jamii kama wengine au kuzidi wengine, hivyo anaomba ridhaa ya wananchi ili apeperushe bendera na atajitahidi kuwainua akina mama.
Philbert Katabazi (Nyerere) anasema kuwa yeye amependekezwa katika ngazi mbalimbali za uongozi wa
CCM hivyo naye ameamua kujiotokeza kuomba nafasi, kwani wanaopendekeza mara kwa mara wanahittaji kuona naye akijitutumua.
Mjuni Kataraiya akiwa ni mwenye kuomba tena nafasi ya ubunge, akiwa na kumbukumbu ya kuongoza jimbo la Bukoba mjini kama Mbunge mwaka 1995-2000, ambapo anasema alikosea kidogo akafungwa goli.
Alipoulizwa ni nini wananchi wawiwe kumrudisha akasema anglau nilitoa lifti kwa wale waliokuwa watu wazima wakati huo.
Na Mwanaharakati.