Wizara ya fedha na uchumi imetoa siku 7
kwa mkurugenzi wa mfuko wa pensheni kwa wastaafu PSPF, iwe imelipa mafao ya wastaafu wanayodai
shirika hilo.
Naibu waziri wa fedha Dk. Ashantu
Kijachi amesema kuwa serikali
imeshalilipa shirika hilo jumla shilingi bilioni 154, kati ya bilioni 177
walizokuwa wakidai serikali, akisisitiza kuwa kama fedha hizo zimelipwa hakuna
sababu ya wastaafu kuendelea kutaabika na mafao yao, kuwa haiwezekani kwasababu
wanaotakiwa kupewa kipaumbele na hilo ni jasho lao.
Amesema kuwa serikali imejiridhisha
baada ya kupokea malalamiko kuwa hundi zao zimeandikwa tangu mwezi januari,
ilhali haijulikani zinakopotelea.
Mkurugenzi mkuu wa PSPF Bwana Adam
Mahingu, amesema kuwa wananchama wake
wengi ni watumishi wa serikali, na serikali imekuwa ikitakiwa kuleta michango, ingawa serikali ilikuwa haijalipa fedha za miezi saba lakini wiki hii shirika hilo limeandaa hundi za wastaafu 444, waliostaafu kwa kipindi cha kuanzia mwezi wa nne hadi wa kumi, pamoja na wanaodai mirathi 142.

Kumekuwa na mkanganyiko wa fedha za
wastaafu, ambazo zinaonesha kuwa zimeshatoka serikalini, ambapo naibu waziri
amesema kuwa katika miezi ya 11 na 12 mwaka huu, serikali imelipa bilioni 70 za
kufunga mwaka, hivyo haikutegemea kuona malalamiko ya wastaafu na hili
halikubaliki katika serikali ya awamu ya 5.
Na Mwanaharakati.