Nicolaus Mac (None Association Movement) KWA MATANGAZO YA REDIO NA TV WASILIANA NASI KWA +255767814844- nicolausngaiza@gmail.com.
Saturday, 25 July 2015
MCHAKATO WA KURA ZA MAONI CHADEMA MANISPAA YA BUKOBA
Ni katika ukumbi wa Rumuli manispaa ya Bukoba ambapo wagombea wamemaliza kujieleza na upigaji kura unaendelea sasa.
Na Mwanaharakati.
ASKOFU KILAINI APIGA MSUMALI VYAMA VYA SIASA
.
Asema wawaletee wagombea wanaopendwa,
.
Watumiao udini, siasa na ukabila hawafai,
.
Hatosita kusema kama mambo yanakwenda vibaya.
Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Bukoba Dr Method
Kilaini, ameiambia sautiyamnyonge kuwa, kiongozi anayetakiwa na jamii ndiye anayepaswa
kuchaguliwa na chama kwani wao ndiyo wapiga kura hivyo wasikoseshwe haki
wanayoipendekeza kuwaongoza.
Hatahivyo ametaja sifa za kiongozi kuwa lazima wananchi wamuulize amewafanyia nini kabla, atafanya nini lakini akasema kuwa
wananchi wanakosa elimu ya kutambua kiongozi bora, hivyo sautiyamnyonge ni moja
ya chombo cha kuwasaidia watu hao
Kumekuwa na desturi za kusambaza kauli za ubaguzi na
kusema udini katika siasa, jambo ambalo amesema haiwezekani wakaendelea kutumia
majukwaa kutukana, akisistiza kuwa angeweza angemwapisha mmojammoja ili
akikiuka alaniwe.
Vyama vya siasa kote nchini, vinaendelea na mchakato wa
kuwapata wagombea wa nafasi ya udiwani, ubunge na urais, huku kukiwa katika
mchakato wa kuomba ridhaa kupitia vyama vyao, ili apatikane kiongozi mmoja kila
kata na jimbo kama ambavyo amepatikana mmoja kwenye nafasi ya urais kupitia
CCM.
Katika manispaa ya Bukoba, wagombea ubunge ni wanane,
ambapo wajumbe wa kata kupitia chama hicho, wamemwambia mbunge anayemaliza muda
wake, kuwa asiangaike kuomba kura, na chama kingempitisha bila kupingwa ili aendelee
kuleta mazuri anayowafanyia.
Na Mwanaharakati.
Friday, 24 July 2015
KIFO CHA JACKIE CHAN
Kumetolewa taarifa kuhusu muigizaji maarufu wa kijapani Jackie Chan kuwa amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo mjini Kong Kong nchini China.
Taarifa inasema kuwa muigizaji huyo alijizolea umaarufu mkubwa katika filamu zake nyingi zikiwemo za kivita na kuchekesha.
Tutakuletea taarifakamili.
Na Mwanaharakati.
Taarifa inasema kuwa muigizaji huyo alijizolea umaarufu mkubwa katika filamu zake nyingi zikiwemo za kivita na kuchekesha.
Tutakuletea taarifakamili.
Na Mwanaharakati.
Thursday, 23 July 2015
KAULI YA AMANI YAWASTUA WANA CCM BUKOBA, MWENYEKITI ANUSURU MKUTANO WA MAONI.
. Kuhusu rushwa taasisi za serikali,
. Baadhi wastukia uhalali wamgombea,
. Ashindwa kubainisha sekta alizotaja
kuhusika.
![]() |
| Mwenyekiti wa mtaa uswahili Bw Udd Miiluko akituliza wajumbe baada ya kutaka Amani apishe mkutano kwa kuwadanganya. |
Katika mkutano wa kwanza wa waomba
ridhaa ya kugombea ubunge ndani ya CCM manispaa ya Bukoba, wagombea ubunge
wakisimama mbele ya adhara ya kata bilele kuwaomba wanaCCM kumpitisha mmoja
kuwania nafasi ya ubunge kupitia chama hicho, ambapo mmoja wa wagombea asema
serikali imejaa rushwa katika setka nne muhimu hapa nchini.
Mtia nia huyo Dr Anatoly Aman kati ya watia nia nane wa
manispaa ya Bukoba, ameshindwa kuendelea baada ya kuulizwa swali kama alivyosema kuwapo taasisi nne za wala rushwa, mmoja wa wajumbe alitaka azitaje kwa majina ndipo yeye akasema yafuatayo na kuzua taaruki kwa wajumbe wa CCM kata
bilele………......................
Sambamba na hilo, amesema kuwa ataleta
maendeleo ya ajabu kwa kujenga soko la kisasa, huku akisema kuwa ameleta
muwekezaji na ameanza kuweka taa za barabarani katika manispaa ya Bukoba.
Kwa upande wake Mjuni Kataraiya,
aliyewahi kuwa mbunge katika jimbo hili 1995- 2000, amejittetea kuwa hakuuza
jimbo bali alishindwa tu katika uchaguzi, hivyo anawaomba wananchi ili alete
maendeeo kwa kipindi alichokaa bila nafasi hiyo amejifunza mengi.
Na Mwanaharakati.
Wednesday, 22 July 2015
HII NDIYO AJALI YA BUS DODOMA WATU 20 WAFARIKI
Ni katika ajali iliyohusisha bus LA SIMIYU EXPRESS iliyokuwa ikitokea Mwanza kwenda Dar es salaam, ambayo imepasuka tairi na kupinduka na watu 20 kufariki papo hapo huku wengine40 wakijeruhiwa.
Taarifa za awali zinasema kuwa bado baadhi ya miili ya marehemu imenasa kwenye gari hilo kwani imeharibika vibaya.
Endelea kufuatilia hapa
Na Mwanaharakati.
Taarifa za awali zinasema kuwa bado baadhi ya miili ya marehemu imenasa kwenye gari hilo kwani imeharibika vibaya.
Endelea kufuatilia hapa
Na Mwanaharakati.
Tuesday, 21 July 2015
WAGOMBEA UBUNGE MANISPAA BUKOBA KUUNGANA
. Ni CCM katika kampeini katika kata,
. Mikutano kuanza 23 hadi 30 julai 2015.
Wakati wa kuelekea katika uchaguzi mkuu, mchakato wa kupata wagombea katika majimbo na kata unaendelea ambapo walioomba nafasi ya ubunge katika manispaa ya Bukoba, wanaanza mchakato wa kutembelea kata zote 14 kuomba kura kwa wajumbe kwa kujielezea na jinsi gani watatekeleza ilani ya CCM kwa atakayechaguliwa.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu ofisi kwake, katibu wa CCM wilaya ndugu Abdul Kambuga, amesema kuwa kwa mujibu wa utaratibu wa chama, inabidi watangaza nia wote waongozane kufanya mikutano kila kata, ambapo kama kuna mgombea anayetaka kwenda na gari yake binafsi anaomba kufanya hivyo ingawa ni lazima awe kwenye msafara mmoja.
Jumla ya wabunge waliotangaza nia ya kugombea jimbo la Bukoba mjini ni 8 baada ya mmoja kushindwa kurejesha fomu, na kufanya idadi ya watu 9 waliochukua fomu kutotimia.

MBUNGE NA DIWANI WAVURUGANA UCHAGUZI MWENYEKITI BUKOBA VIJIJINI
. Wananchi watahabika na barabara,
. Akana kupewa hela mbunge,
. Wasema apewe nafasi nyingine.
Hatahivyo inadaiwa kuwa mbunge huyo amesikika akisema kuwa barabara hiyo imeshindwa kukamilika baada ya diwani wa kata hiyo SYLVAND LUGALAMULA kukataa pesa za ukarabati wake.
Sambamba na tatizo la barabara, wakaazi wa vijiji vya Nyakibimbili, Kitahya Bugengere na Bundaza, wanakabiliwa na huduma ya matibabu huku wakijengewa kliniki na shirika la kiraia WORLDVISION, ambayo hatahivyo haina wahudumua.
Kandayaziwa blog, bado inaendelea kumtafuta mbunge wa jimbo anayemaliza muda wake katika jimbo la Bukoba mjini kupata maelezo yake kuhusu hilo.
Na Mwanaharakati.
. Akana kupewa hela mbunge,
. Wasema apewe nafasi nyingine.
Ni katika kata ya Nyakibimbili wilayani Bukoba vijijini
kaskazini magaharibi mwa mkoa wa Kagera, katika jimbo analogombea Jasson
Rweikiza, huku wananchi wakimuuliza ataomba vipi kura zao ilhali alishindwa
kukamilisha barabara inayowafanya kukosa huduma muhimu za matibabu na
kusafirisha bidhaa zao za kilimo kupata masoko.
Hatahivyo inadaiwa kuwa mbunge huyo amesikika akisema kuwa barabara hiyo imeshindwa kukamilika baada ya diwani wa kata hiyo SYLVAND LUGALAMULA kukataa pesa za ukarabati wake.
Katika mahojiano maalumu na kandayaziwa blog, diwani wa kata
hiyo aliyemaliza muda wake Bwana Sylivand Lugalamula amefafanua kuwa anahisi
mbunge huyo amechukia baada ya kushiriki kampeini za kumchagua mwenyekiti wa
halmashauri.
Sambamba na tatizo la barabara, wakaazi wa vijiji vya Nyakibimbili, Kitahya Bugengere na Bundaza, wanakabiliwa na huduma ya matibabu huku wakijengewa kliniki na shirika la kiraia WORLDVISION, ambayo hatahivyo haina wahudumua.
Kandayaziwa blog, bado inaendelea kumtafuta mbunge wa jimbo anayemaliza muda wake katika jimbo la Bukoba mjini kupata maelezo yake kuhusu hilo.
Na Mwanaharakati.
Subscribe to:
Posts (Atom)