MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 25 July 2015

MCHAKATO WA KURA ZA MAONI CHADEMA MANISPAA YA BUKOBA

Ni katika ukumbi wa Rumuli manispaa ya Bukoba ambapo wagombea wamemaliza kujieleza na upigaji kura unaendelea sasa.

Na Mwanaharakati.

ASKOFU KILAINI APIGA MSUMALI VYAMA VYA SIASA



. Asema wawaletee wagombea wanaopendwa,
. Watumiao udini, siasa na ukabila hawafai,
. Hatosita kusema kama mambo yanakwenda vibaya.

Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Bukoba Dr Method Kilaini, ameiambia sautiyamnyonge kuwa, kiongozi anayetakiwa na jamii ndiye anayepaswa kuchaguliwa na chama kwani wao ndiyo wapiga kura hivyo wasikoseshwe haki wanayoipendekeza kuwaongoza.

Hatahivyo ametaja sifa za kiongozi kuwa lazima wananchi wamuulize amewafanyia nini kabla, atafanya nini lakini akasema kuwa wananchi wanakosa elimu ya kutambua kiongozi bora, hivyo sautiyamnyonge ni moja ya chombo cha kuwasaidia watu hao
Kumekuwa na desturi za kusambaza kauli za ubaguzi na kusema udini katika siasa, jambo ambalo amesema haiwezekani wakaendelea kutumia majukwaa kutukana, akisistiza kuwa angeweza angemwapisha mmojammoja ili akikiuka alaniwe.

Vyama vya siasa kote nchini, vinaendelea na mchakato wa kuwapata wagombea wa nafasi ya udiwani, ubunge na urais, huku kukiwa katika mchakato wa kuomba ridhaa kupitia vyama vyao, ili apatikane kiongozi mmoja kila kata na jimbo kama ambavyo amepatikana mmoja kwenye nafasi ya urais kupitia CCM.

Katika manispaa ya Bukoba, wagombea ubunge ni wanane, ambapo wajumbe wa kata kupitia chama hicho, wamemwambia mbunge anayemaliza muda wake, kuwa asiangaike kuomba kura, na chama kingempitisha bila kupingwa ili aendelee kuleta mazuri anayowafanyia. 

Na Mwanaharakati.

Friday, 24 July 2015

KIFO CHA JACKIE CHAN

Kumetolewa taarifa kuhusu muigizaji maarufu wa kijapani Jackie Chan kuwa amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo mjini Kong Kong nchini China.

Taarifa inasema kuwa muigizaji huyo alijizolea umaarufu mkubwa katika filamu zake nyingi zikiwemo za kivita na kuchekesha.

Tutakuletea taarifakamili.
Na Mwanaharakati.

Thursday, 23 July 2015

KAULI YA AMANI YAWASTUA WANA CCM BUKOBA, MWENYEKITI ANUSURU MKUTANO WA MAONI.



. Kuhusu rushwa taasisi za serikali,
. Baadhi wastukia uhalali wamgombea,
. Ashindwa kubainisha sekta alizotaja kuhusika.
Mwenyekiti wa mtaa uswahili Bw Udd Miiluko akituliza wajumbe baada ya kutaka Amani apishe mkutano kwa kuwadanganya.




Katika mkutano wa kwanza wa waomba ridhaa ya kugombea ubunge ndani ya CCM manispaa ya Bukoba, wagombea ubunge wakisimama mbele ya adhara ya kata bilele kuwaomba wanaCCM kumpitisha mmoja kuwania nafasi ya ubunge kupitia chama hicho, ambapo mmoja wa wagombea asema serikali imejaa rushwa katika setka nne muhimu hapa nchini.

Mtia nia huyo Dr Anatoly Aman kati ya watia nia nane wa manispaa ya Bukoba, ameshindwa kuendelea baada ya kuulizwa swali kama alivyosema kuwapo taasisi nne za wala rushwa, mmoja wa wajumbe alitaka azitaje kwa majina ndipo yeye akasema yafuatayo na kuzua taaruki kwa wajumbe wa CCM kata bilele………......................

Sambamba na hilo, amesema kuwa ataleta maendeleo ya ajabu kwa kujenga soko la kisasa, huku akisema kuwa ameleta muwekezaji na ameanza kuweka taa za barabarani katika manispaa ya Bukoba.

Katika mkusanyiko huo wa wajumbe,ewaomba ridhaa 6 wamesimama kujinadi kila mmoja kwa nafasi yake kueleza watafanya nini, ingawa imeonesha kila anayeulizwa kuhusu uliwahi kufanya nini, imekuwa ngumu kupata swali la moja kwa moja na kuwaridhisha wajumbe kama walivyo tarajia majibu.

Kwa upande wake Mjuni Kataraiya, aliyewahi kuwa mbunge katika jimbo hili 1995- 2000, amejittetea kuwa hakuuza jimbo bali alishindwa tu katika uchaguzi, hivyo anawaomba wananchi ili alete maendeeo kwa kipindi alichokaa bila nafasi hiyo amejifunza mengi. 

Na Mwanaharakati.

UJIO WA OBAMA HALI YA TAHARUKI KENYA TAZAMA HAPA



Na Mwanaharakati.

Wednesday, 22 July 2015

HII NDIYO AJALI YA BUS DODOMA WATU 20 WAFARIKI

Ni katika ajali iliyohusisha bus LA SIMIYU EXPRESS iliyokuwa ikitokea Mwanza kwenda Dar es salaam, ambayo imepasuka tairi na kupinduka na watu 20 kufariki papo hapo huku wengine40 wakijeruhiwa.

Taarifa za awali zinasema kuwa bado baadhi ya miili ya marehemu imenasa kwenye gari hilo kwani imeharibika vibaya.

Endelea kufuatilia hapa
Na Mwanaharakati.

Tuesday, 21 July 2015

WAGOMBEA UBUNGE MANISPAA BUKOBA KUUNGANA

. Ni CCM katika kampeini katika kata,
. Mikutano kuanza 23 hadi 30 julai 2015.
Wakati wa kuelekea katika uchaguzi mkuu, mchakato wa kupata wagombea katika majimbo na kata unaendelea ambapo walioomba nafasi ya ubunge katika manispaa ya Bukoba, wanaanza mchakato wa kutembelea kata zote 14 kuomba kura kwa wajumbe kwa kujielezea na jinsi gani watatekeleza ilani ya CCM kwa atakayechaguliwa.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu ofisi kwake, katibu wa CCM wilaya ndugu Abdul Kambuga, amesema kuwa kwa mujibu wa utaratibu wa chama, inabidi watangaza nia wote waongozane kufanya mikutano kila kata, ambapo kama kuna mgombea anayetaka kwenda na gari yake binafsi anaomba kufanya hivyo ingawa ni lazima awe kwenye msafara mmoja.
Jumla ya wabunge waliotangaza nia ya kugombea jimbo la Bukoba mjini ni 8 baada ya mmoja kushindwa kurejesha fomu, na kufanya idadi ya watu 9 waliochukua fomu kutotimia.

Na Mwanaharakati.

MBUNGE NA DIWANI WAVURUGANA UCHAGUZI MWENYEKITI BUKOBA VIJIJINI

. Wananchi watahabika na barabara,
. Akana kupewa hela mbunge,
. Wasema apewe nafasi nyingine.



Ni katika kata ya Nyakibimbili wilayani Bukoba vijijini kaskazini magaharibi mwa mkoa wa Kagera, katika jimbo analogombea Jasson Rweikiza, huku wananchi wakimuuliza ataomba vipi kura zao ilhali alishindwa kukamilisha barabara inayowafanya kukosa huduma muhimu za matibabu na kusafirisha bidhaa zao za kilimo kupata masoko.

Hatahivyo inadaiwa kuwa mbunge huyo amesikika akisema kuwa barabara hiyo imeshindwa kukamilika baada ya diwani wa kata hiyo SYLVAND LUGALAMULA kukataa pesa za ukarabati wake.

Katika mahojiano maalumu na kandayaziwa blog, diwani wa kata hiyo aliyemaliza muda wake Bwana Sylivand Lugalamula amefafanua kuwa anahisi mbunge huyo amechukia baada ya kushiriki kampeini za kumchagua mwenyekiti wa halmashauri.





Sambamba na tatizo la barabara, wakaazi wa vijiji vya Nyakibimbili, Kitahya Bugengere na Bundaza, wanakabiliwa na huduma ya matibabu huku wakijengewa kliniki na shirika la kiraia WORLDVISION, ambayo hatahivyo haina wahudumua.

Kandayaziwa blog, bado inaendelea kumtafuta mbunge wa jimbo anayemaliza muda wake katika jimbo la Bukoba mjini kupata maelezo yake kuhusu hilo.
Na Mwanaharakati.