Nicolaus Mac (None Association Movement) KWA MATANGAZO YA REDIO NA TV WASILIANA NASI KWA +255767814844- nicolausngaiza@gmail.com.
Sunday, 19 February 2012
Thursday, 16 February 2012
Kwanza hizi ni pikipiki kwa ajili ya kubebea mama wajawazito lakini kwa sasa hazijatumika na tayari ziko katika hali mbaya, yaani zimeanza kuhujumiwa kabla ya kazi.
Hii ndiyo sura ya mbele ya Hospitali hii ya mkoa ikionekana safi kimazingira, lakini ndani kwenye WARD za wagonjwa kunatisha make mashuka ni machafu hasa katika vyumba vya waliojeruhiwa.
Mgonjwa huyu hapa chini amekaa hospitali zaidi ya wiki akisubiri upasuaji wa jicho baada ya kutoka chumba cha upasuaji amelazwa katika mashuka machafu yenye Damu.
Shule ya Kata Bugandika Kiziba inatumika kufundishia wanafunzi lakini bado haijakamilika, na hii ni kwasababu ya kuendeleza elimu hivyo wadau wa elimu jitokezeni kusaidia hali hii.
Pamoja na ujenzi huo kuendelea kwa kusuasua, kuna sintofahamu inayowapa wasiwasi waliowengi ususani katika baadhi ya maeneo kwa walipoanzia upanuzi huu.
Ajabu ni pale wanapofikia kwa wale waliojenga kuingia barabareni wapanuzi hawa wanaweka kona kwa lengo la kuwakwepa kushhindwa kuwaondoa.
Huu ni mfano tosha katika eneo la Victorias ambapo packing ya magari iko kabisa barabarani sasa wajenzi hawa wameongeza kona upande wa pili kukwepa packing hiyo.
Baada ya kuona Daraja au CARAVAT ya pale Annex kwa inakuwaje limefanywa finyu na kwanini upanuzi huu unaoneka sehemu zingine zimepanuliwa na zingine wanaziacha hivyohivyo? Kaimu meneja TANROADS Kagera Mhandisi Nasri Chakindo, alisema hayo ni mambo ya kiufundi ila nilipotaka kujua mambo gani hayo alisita kunena.
Upanuzi huu umenzia hospitali ya mkoa hadi Upendo ila zoezi litaendelea hadi kastamu na kule Rwamishenye kwani saizi hakuna fedha ya kutosha, hayo ni maneno ya TANROADS.
Tuesday, 14 February 2012
Ikiwa ni siku mwafaka ya wapendanao (VALENTINE DAY) mimi nimemzawadia ua maalum ndiyo maana kwa furaha naye kaamua kuniunga mkono kwa kulibusu.
Jah Bless you my Kid Bertha Lucky.
Monday, 13 February 2012
Baadhi ya wachezaji wa Kagera Sugar wakitoka uwanjani Kaitaba vichwa chini, baada ya kulazwa Bao 2-0, ndoto zao kupanda Ligi kuu Tanzania Bara zinafutika kwani mechi iliyopita katika uwanja wao wa nyumbani walipigwa bao 1-0 na JKT Ruvu.
Tuesday, 7 February 2012
NI mwalimu mkuu wa shule ya Kangabusharo Bw. PILIUS EMMANUEL akiwa ofisini kwake shuleni hapo. Analalamikia kuwa na walimu wa kiume pekee katika shule hiyo ambapo wanashindwa kulifundisha darasa la saba kwasababu wanafunzi wa kike katika darasa hilo wengi wanabalehe hivyo kulifanya darasa hilo kuwa katika hali mbaya ya hewa na uchafu kwani wengi wanaingia katika siku zao EDHI bila kujijua hivyo kuwafanya walimu kuona aibu katika darasa hilo.
Hawa ni wanafunzi katika darasa la tano wanaonekana wadogowadogo lakini baadhi ya mabinti nao wakianza kubalehe inakuwa ni chnagamoto kwa walimu hao wakiume waliopo shuleni hapo.
Mwalimu PILIUS alipohojiwa nami amesema ameshapeleka maombi katika ofisi ya afisa elimu wa wilaya ya Bukoba kupatiwa walimu wa kike ila anashangaa kuona kimya.
Subscribe to:
Posts (Atom)