MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 31 May 2015

HOTUBA YA MWIGULU NCHEMBA, UKUMBI WA MWL. NYERERE DODOMA

 Anazungumza na watanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari, huku akieleza kuwa ametangazia Dodoma kwasababu anazungumza na watanzania.

Amesema kuwa matatizo yanayowasibu watanzania hajalisoma vitabuni bali ndiyo maisha aliyoishi, kutokana na umaskini wa alipototea kwenye familia ya mzee Materu, ilhali akisema kuwa alishawahi kubeba zege, na mkewe kupika mama lishe huku akipokea matusi mbalimbali ya wabeba zege wenye njaa.

Mambo matatu muhimu anayofikiri ni muhimu kwaq watanzania, ni kujitegemea hasa kwa kulipa kodi, awamu ya matumizi kwa kuziba mianya ya matumizi mabaya, na kukomesha kazi kwa mazoea.

Ameongeza kuwa tumeendelea kulalamikia masoko, kuuza vitu vikiwa ghafi na kuendelea kulalamikia pembejeo, akisema kuwa kazi ya rais wa tano siyo fadhila bali kazi anayokwenda kuifanya.

Endelea kutufatilia hapa

Na Mwanaharakati.

HOTUBA; WASIRA AKITANGAZA NIA KUWANIA URAIS KATIKA UKUMBI WA B.O.T JIJINI MWANZA LEO




HOTUBAYA MHESHIMIWA STEPHEN WASIRA KATIKA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAISWA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  1. Nianze kwa kutoa shukrani kwenu wote mlioacha shughuli zenu ili kuja hapa kunisikiliza. Kuja kwenu hapa kwa wingi ni ishara ya imani mliyonayo kwangu, Nawashukuru sana
  2. Kwa zaidi ya mwaka mzima, kumekuwepo na miningo’no kuhusu uwezekano wangu kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Aidha kutokana na mijadala ya wananchi au kupitia mitandao ya kijamii au vyombo rasmi vya habari, mining’ono hiyo imefanya baadhi ya watu wanifuate ili wanishauri nigombee na wengine wamenipigia simu kwa kunishawishi nisisite kugombea
  3. Leo, nakuja hapa Mwanza kuvunja ukimya na kumaliza minong’ono kwa kutangaza rasmi kwamba nimekata shauri kugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania


KWANINI NAGOMBEA

Zikosababu kadhaa, ambazo zimenisukuma kugombea kufikia uamuzi huo

  • Haki yangu ya kikatiba. Hii ni sababu ya msingi lakini siyo yenye uzito, kwa vile ni haki ya kikatiba na ni kwa ajili ya watanzania wote. Hivyo zinahitajika sababu za ziada licha ya haki ya kikatiba
  • Naifahamu Tanzania, Kwa muda mrefu tangu miaka ya 1970 nimeshirikishwa katika uongozi wa nchi yetu tangu nikiwa na umri wa miaka wa 27


  • 1970 kwa mara ya kwanza nilichaguliwa kuwa mbunge wa Mwibara katika wilaya ya Bunda
  • 1973 niliteuliwa kuwa waziri mdogo (Juniour Minister)
  • 1975 Niliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na katibu wa TANU wa mkoa
  • 1982-1985 Afisa mwandamizi mkuu ubalozi wa Tanzania Marekani
  • 1987-1989 Raisi alniteua kuwa naibu waziri wa serikali za mitaa na mifugo na vyama vya ushirika
  • 1989-1990 Niliteuliwa kuwa Waziri wa kilimo, mifugo
  • 1990-1991 Mkuu wa mkoa wa pwani na katibu wa CCM Mkoa
  • 2005-2015 Waziri wa wizara ya maji , kilimo, ofisi ya Waziri mkuu Kilimo tena Ofisi ya rais mahusiano na uratibu na hatimae kilimo tena hadi sasa

Shughulihizi chini ya Marais wa awamu zote nne umenipa uzoefu mkubwa wamasuala ya kitaifa na kuniwezesha kuifahamu vema Nchi yetu. Mimi nimiongoni mwa Watanzania wachache, wanaoijua Tanzania ya leo nakubashiri Tanzania ya kesho.
Kamamwanafunzi mzuri wa nafasi mbalibali, walioniundisha waliozingatiahazina ya uzoefu, naamini uzoefu niliopata utanisaidia sana katikauongozi wa nchi yetu iwapo chama changu kitanipendekeza na hatimayekuchaguliwa na watanzania kwa Rais wa nchi yetu
Pamojana yote hayo haitakuwa rahisi kwangu kufanya uamuzi wa kugombeanafasi ya urais. Hii ni kwa sababu natambua majukumu na wajibu waRais ulivyo mzito wa kuongoza watanzania karibu million hamsini (50)na zaidi kwa ulinzi wa matumaini na matamanio yao ya nyakati.
Hatahivyo, baada ya tafakuzi nimeridhika kuwa uamuzi wa kugombea nafasihii ya juu kabisa katika nchi yetu ni sahihi na ni wakati mwafaka nahali ya kisiasa ilivyo kwa sasa, najiona kuwa mtu sahihi , kwa kuwaninayo nia ya kuipeleka nchi yetu katika ngazi ya juu zaidi kisiasa,kiuchumu na kijamii.
SERAYA JUMLA ZA NCHI
Baadaya maelekezo hayo ya utangulizi, sasa nizungumzie mambo ya msingi nahazina yanayohusu uongozi wa nchi yetu.
Endaponitateuliwa na chama changu na kupata ridhaa ya watanzania na hivyokuchaguliwa kuwa Rais wa Jamuhuri yaMuungano wa Tanzania nitaelekezanguvu zangu katika kusimamia yafuatayo;-

  1. Tanzania inabaki kuwa nchi imara yenye Umoja, Amani na Mshikamano.
  2. Taasisi nzito hususani mihimili mitatu ya dola ya kitaifa ( Serikali, Mahakama na Bunge) Zinaimaimarishwa na kuwezeshwa ili zitekeleze majukumu yake sahihi kwa mujibuwa katiba
  3. Utumishi wa umma utafanyiwa marekebisho ili utekeleze wajibu wake kwa uadlifu na waladi
  4. Kusimamia na kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kukua kwa viwango vya juu zaidi ( kufikia tarakimu mbili) na utengenezaji wa nafasi za ajira unaoendana na matamanio ya wananchi
  5. Kuhakikisha raia wa Tanzania (wazawa) Wanawezeshwa ili washiriki kikamilifu katika kuendesha uchumi wa nchi yao.


CHANGAMOTOZINAZOIKABILI TANZANIA NA WATAZANZANIA
Haitoshikuifahamu Tanzania kama nchi na historia yake bila kuelewa changamotochangamoto zinazowakabili wananchi. Iwapo Chama change kitaniteuakupeperusha bendere ya CCM, na kupata ridhahaa, yako mambo manneambayo yatashughulikiwa na serikali ya awamu ya tano chini ya uongoziwangu. Mambo hayo ni;-

  1. Umasikini wa kipato

Pamoja na mafanikioya kukua kwa ..................

AFISA WA TUME YA UCHAGUZI AMETOROKA RAIS APATA PIGO, SOMA HAPA



Nia ya rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu imepata pigo baada ya ripoti kutoka nchini humo kudai kuwa mwenyekiti msaidizi wa tume ya uchaguzi ametoroka.

Afisa mmoja tume hiyo ya uchaguzi ameiambia redio moja ya Ufaransa kuwa Spes Caritas Ndironkeye aliabiri ndege ijumaa na haijulikani kama alijiuzulu au la.
Tume hiyo ya uchaguzi ina maafisa wakuu watano na inaweza kuendelea kuhudumu hata baada ya kuondoka kwa mmoja wao.

Hata hivyo duru zinaelezea kuwa huenda afisa wa pili wa tume hiyo akajiondoa na hivyo kulemaza shughuli za tume hiyo.

Juma lililopita kanisa katoliki nchini Burundi lilijiondoa kutoka kwa harakati zozote za uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata siku moja tu kabla ya umoja wa Ulaya kuondoa maafisa wake katika shughuli hizo za uchaguzi.

Umoja wa ulaya ulikuwa umetuma maafisa wa kucimamia na kuhakikisha kuwa uchaguzi huo ni wa huru na haki.

Taarifa hiyo imetokea wakati ikisalia wiki moja tu uchaguzi wa wabunge na madiwani ufanyike nchini humo.

Kanisa katoliki ni kiungo muhimu katika suala la amani na demokrasia nchini Burundi tokea kuanzishwa mazungumzo ya amani ya Arusha mnamo miaka ya tisini.

Haya yamearifiwa wakati maandamano dhidi muhula wa tatu wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza yanaendelea kufanyika katika mitaa kadhaa ya mji mkuu Bujumbura kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Makundi ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa zaidi ya watu 20 wamefariki wakati wa ghasia za maandamano,

Tangu rais Pierre Nkurunziza alipotangaza mwezi uliopita kuwa anapania kuwania tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu, kinyume na katiba ya Burundi.
Uchaguzi wa urais umepangiwa kufanyika Juni tarehe tano, huku ule wa urais ukiwa mwishoni mwa mwezi huo wa Juni.
 

Na Mwanaharakati.

Saturday, 30 May 2015

VIDEO; KANGELUGOLA MBUNGE WA MWIBALA AMUITA LOWASA, NABII- TAZAMA HAPA

Ni katika mkutano ambao mh Lowasa ametaja sababu za msingi kumsukuma agombee nafasi hiyo, huku akisema kuwa ni makubaliano yao kati yake na rais Kikwete wakati wa kugombea miula miwili iliyopita.
Na Mwanaharakati.

VIDEO; HOTUBA YA LOWASA NA KINGUNGE MKUTANO WA KUTANGAZA NIA ARUSHA

Katika mkutano huo ulioudhuriwa na maelfu ya watu kutoka mikoa mbalimbali, hasa viongozi wa CCM, Kingunge amesema kwa mara ya kwanza ameshuudia umati mkubwa kumkubali kiongozi katika hatua ya kwanza kama hii.


Na Mwanaharakati.

MBUNGE AZUIA UANDIKISHAJI BVR KAGERA?



. Ni baada ya kutowaletea maendeleo,
. Mradi wa umeme waelekezwa kwa wachache,
. Barabara mbovu wajasriamali, na wagonjwa walalama.
Ni kutokana na wananchi kubainika kiasi kidogo kujitokeza katika halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera, kwenye uandikishaji BVR kanda B kama zilivyotengwa na halmashauri husika, ambapo mtandao huu umejionea wananchi kiduchu katika  kata Karabagaine kilomita 18 kutoka Bukoba mjini.

Katika vituo vya kijiji Kitwe, na Kangabusharo, mtandao huu umetaka kujua sababu ya kuwafanya wananchi waendelee na shughuli zao ili kwenye vituo umeandikishwa watu 8 tangu saa2 asubuhi hadi saa 7 mchana, ikabainika kuwa wanaamini kujiandikisha ni kunufaisha viongozi hasa wakisiasa, hasa kwa kumtaja mbunge.
KANDAYAZIWA BLOG, imejionea ubovu wa barabara yenye urefu wa kilomita 2.5 kutoka Kiziru kuelekea gereza Rwamulumba, ambapo wakaazi wanaamini kuwa wametupiliwa mbali na viongozi wao.
Wameomba TANROADS kuwapa ruksa ya kukarabati barabara hiyo, ili wajinusuru na baadaye gharama yao irudishwe na wakala hao wa barabara mkoani Kagera, kama mwenyekiti wa kijiji na mtendaji Kagabusharo wanavyoeleza.
Mimi mtendaji wa kijiji Kangabusharo Bi Joyce Kayoza, barabara hiyo imekuwa kero kwetu, lakini pia tutafanya mkutano wa kujadili kjinsi ya kupata pesa za kujenga barabara hiyo, fedha ambayo baadaye wataomba TANROAD iwarudhie kwani itakuwa imetokana na nguvu za wananchi.

Mwishoni mwa mwaka jana, aliyekuwa meneja wa TANROADS mkoani Kagera John Kalupare, alieleza kuwa barabara hiyo iko chini ya mamlaka ya chai Bukoba Tea Company Rwabikanshe, ambao waliomba kwa makubaliano na wakala huo taifa, kuwa watakuwa wakiifanyia marekebisho, kwa kigezo kuwa TANROADS ikikarabati unafanyika uharibifu wa majani chai yaliyo pembezoni mwa barabara hiyo.
Hatahivyo muhandisi John Kalupare, aliongeza kuwa baada ya BTC kushindwa kufanya ukarabati huo, wakala huo umeandika barua kwao ili wakubali kubatilisha makubaliano ya zamani ili TANROADS ikarabati barabara yake, ingawaje kwa sasa, wakala huo Kagera umesema unafuatilia jambo hilo kwa karibu. 

Na Mwanaharakati.

UPDATES; MKUTANO WA EDWARD LOWASA ARUSHA LEO JUMAMOSI


. Magari matangazo PA yazunguka mtaani kukumbusha wananchi,
. Mitambo ya matangazo na live yatisha,
. Wadau waamkia uwanjani tangu asubuhi.


Ni mkutano unaofanyika leo katika uwanja wa Shehk Amri Abeid mjini Arusha, ambapo saa 8;00 kamili mchana matangazo ya moja kwa moja yataanza kurushwa na vyombo vya habari vya IPP MEDIA, Chanel Ten na CLOUDS, pamoja na redio kadhaa za kijamii, zitaanza kurusha matangazo ya moja kwa moja.
Mtandao huu utaendelea kukuletea live updates za mkutano huo, ambao mbunge wa Monduli na aliyekuwa waziri mkuu katika awamu ya nne, mh Edward Lowasa, anatarajiwa kutangaza nia ya kuwania urais wa awamu ya tano, huku akisisitiza kueleza machache kuhusu tuhuma anazotajwa kuhusika.
Na Mwanaharakati.

Wednesday, 27 May 2015

HAYA NDIYO MAUAJI MAPYA YA KUTISHA BUKOBA, WENGINE WACHINJWA LEO

. Waliochinjwa leo watolewa pua,
. Kwa mara ya kwanza auawa mwanamke,
. Tukio moja lafanyika vijijini.
Watu wawili wameuawa kwa kuchinjwa, na hatimaye kutolewa pua, huku wakikatwa na kitu chenye ncha kazi kisogoni, mauaji ambayo yanafanana, ambapo mtandao huu umetembelea maeneo ya kata Karabagaine  katika kijiji cha Kitwe, na kukuta Joseph Gabriel, aliyekuwa akifanya vibarua mbalimbali kukutwa amekatwa na kitu chenye ncha kali, huku akiondolewa sehemu ya pua na shavu la kushoto, huku kukiwa na kipande cha sabuni inayoonesha kuwa aidha alitoka au akienda kukitumia.
Mtandao huu umezungumza na mwenyekiti wa kijiji Kitwe, muda mfupi kabla ya kuwasili poilisi, ambao hatahivyo walichelewa kufika kutokana na kuwa katika tukio lingine lililotokea siku moja na hilo la Kitwe.
 
Mashuuda waliozungumza na KANDAYAZIWA, wamesema kuwa aina hii ya mauaji na kuondoa pua za marehemu ilikuwa haijawahi kutokea, ukiachilia mbali mauaji yale alipouawa kijana katika barabara ya Kagondo Rwamishenye wiki chache zilizopita.

Mauaji mengine yaliyofanyika leo, inasemekana mwanamke ambaye jina lake halikufahamika maramoja, ameuawa kwa kuchinjwa na pua yake kuokotwa katika maeneo ya karibu na tukio, katika mtaa wa Kibeta kata Kibeta.
Mtandao huu umefika katika eneo la tukio na kukuta mwili wa marehemu umeshaondolewa na polisi, kama picha inavyoonesha chini, lakini taarifa aliyotupa mmoja wa askari waliofika kwenye tukio hilo, amesema kuwa pua ya mama huyo umeokotwa maeneo jirani huku katika eneo hilo kutokutikana kiasi cha damu ya kumwagika ispokuwa matone tu ya damu.

Mwezi uliopita, polisi Kagera ilitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mauaji ya manispaa ya Bukoba, ikieleza kuwashikilia watu kadhaa na kinara wa mauaji hayo, ambao majina yamehifadhiwa kwasababu za kiusalama, huku ikisema kuwa watu wawili waliuawa na polisi kwa kupigwa risasi, wakati wakiwapelka kwenye maeneo wanakopangia uhalifu huko Bugabo halmashauri ya Bukoba.
Na Mwanaharakati.

Tuesday, 26 May 2015

SIKILIZA KAULI YA MWISHO YA RWANGISA, TANGAZO LA KIFO CHAKE HAPA

Siku chache kabla ya kifo chake alizungumza nasi kwa njia ya simu kutokea New York Marekani, akisisitiza yafuatayo kwa wana Bukoba.

Baada ya kifo chake saa 5;00 asubuhi saa za huko, ambazo ni 12;00 jioni kwa afrika mashariki, baada ya kufanya mawasiliano na familia ya marehemu, mbunge Kagasheki alipewa taarifa kuwa taratibu za kusafirisha mwili zinafanyika tayari kuletwa Bukoba kwa maziko.
Bw. Samuel N. Luangisa ni nani?
Ni mzaliwa wa Bukoba mmoja kati ya waasisi wa TANU na hatimaye CCM, ambaye alipata kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza wa baada ya uhuru (1961–1964), ambaye hatahivyo alikuwa miongoni mwa waliopendekeza mkoa huo kuitwa Kagera badala ya jina la awali la mkoa wa Ziwa magaharibi.
Jina hilo lilibadilishwa na kuwa “Kagera” mwaka 1979, mara baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda, ambapo mkoa, chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa, aliyekuwepo wakati huo, Capt. Peter Kafanabo, ulipendekeza uitwe “Kagera”chini ya ushauriano wa mzee Luangisa.
 
SAMWEL RUANGISA alipata kuwa mbunge wa jamuhuri ya muungano kupitia jimbo la Bukoba mjini kwa tiketi ya CCM kati ya 1985-1990, na baada ya hapo ameendelea kuwa diwani wa kata Kitendaguro anakozaliwa hadi 2014 alipovuliwa udiwani na mahakama kutokana na mgogoro uliojitokeza na kushindwa kuudhulia baadhi ya vikao vya baraza la madiwani, akiwa miongoni mwa madiwani sita waliovuliwa kati ya madiwani 24 wa manispaa hiyo.  


Na Mwanaharakati.

Monday, 25 May 2015

MZEE SAMUELI NTAMBALA LUANGISA AMEFARIKI DUNIA, SOMA HAPA

Taarifa za awali zinasema kuwa mzee Ruangisa ameaga dunia huko nyumbani kwake New York Marekani, ambapo alikuwa chini ya uangalizi wa daktari nyumbani kwake, akisumbuliwa na maradhi.
 matibabu ya afya yake takribani miezi mitano sasa.
 Kushoto ni Mzee Rwangisa, Murungi kichwabuta na Balozi Kagasheki, walipokuwa  nyumbani kwa mzee Rwangisa New york Marekani, siku chache zilizopita.
Endelea kufuatilia upate kusikia sauti yake siku chache zilizopita.
Na Mwanaharakati.

TARIFA ZA KIFO CHA MZEE SAMWELI RWANGISA

Itakumbukwa kuwa amekuwa akisumbuliwa na maradhi huko New York nyumbani kwake akitibiwa hivyo taarifa zaidi tutakuletea hapa.
Na Mwanaharakati.

RAIS ABADILISHA WAKUU WA WILAYA 10, DARRY RWEGASIRA AONDOLEWA KARAGWE, KYERWA YAPATA MPYA KUTOKA MKALAMA.



Rais Kikwete amemteua Bw Antony Mavunde kuwa mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, kuanzia leo jumatatu 25 may 2015, huku akifanya uhamisho wa wakuu wa wilaya 10 kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa wilaya mbalimbali nchini.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa mkuu wa wilaya Karagwe Darry Rwegasira, amepelekwa wilaya ya Biharamulo, huku Dc Misenyi  Fadhil Nkulu, akipelekwa wilaya ya Mkalama.

Elias Choro John Tarimo, ametolewa Biharamulo kwenda Chunya mkoani Mbeya, huku Deodartus Kinawiro kutoka Chunya kwenda Karagwe mkoani Kagera.
 

Na Mwanaharakati.