MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 5 October 2014

BREAKING NEWS!!!SIKU YA WALIMU DUNIANI WALIMU WAITUMIA KUPELEKA UJUMBE KATIKA BUNGE LA KATIBA

Katika maadhimisho hayo yanayoendelea kitaifa mjini Bukoba mkoani Kagera mgeni rasmi akiwa waziri mkuu Pinda, walimu wameandamana wakiwa na mabango mnalimbali.
 
 
 
Katika mabango hayo kuna ujumne mbalimbali kuwa mishaara yao 370000/= ilhali serikali imetumia fedha nyingi kulipa wabunge wa katiba kwa siku moja laki3 kuwa hili halikubaliki.
Na Mwanaharakati.

Saturday, 4 October 2014

BALOZI KAGASHEKI ATOA NYUMBA KWA SHIRIKA

Kulia na mh Kagasheki na kushoto anayeonekana mgongo ni mkurugenzi wa COSAD Bw Smart Baitan wakati wa chai ya pamoja nyumba kwa mbunge huyo, alipotembelewa na ujumbe wa COSAD.



Baba askofu Kilaini kushoto akiteta jambo na mmh mbunge Kagasheki muda mfupi kabla hawajazindua ofisi ya COSAD.

 Balozi Kagasheki ambaye ndiyo mbunge wa jimbo la Bukoba mjini, amesema kuwa amevutiwa sana na uwekezaji wa shirika hilo, hasa katika kuweka Kliniki ya kisasa ambayo itapunguza matatizo mengi ya wananchi anaowaongoza, huku akiahidi kushiriki nao na kusema kuwa nyumba aliyoitoa itasaidia kutumiwa na madaktari watakaokuwa wakitoa huduma katika hospitali hiyo yenye vifaa vya kisasa.
Ni balozi Kagasheki akikata utepe wa ofisi kuu ya COSAD Kagera iliyoko Kashura manispaa ya Bukoba.

Na Mwanaharakati.

NEWS ALERT!!! UNDANI WA MKUTANO WA MAAFISA MIPANGO

Mkutano wa kitaalamu ambao unawakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka tasnia za mipango, uchumi, takwimu na maendeleo, wenye wajibu wa kusimamia uchumi na mipango umefunguliwa rasmi na kuwakutanisha kwa pamoja wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba wakati wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Washiriki wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani).


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Balozi (Mstaafu) Dkt. Lumbanga alisema kuwa wachumi na maafisa mipango wana wajibu mkubwa katika kuishauri serikali juu ya njia bora na madhubuti za kupambana na umaskini na kuharakisha maendeleo kwa jamii ya Watanzania.

“Muna dhima kubwa katika kushauri kitaalamu juu ya namna nzuri za kupunguza tatizo sugu la umaskini miongoni mwa Watanzania,” alisema.

Balozi (Mstaafu) Dkt. Lumbanga aliwasihi washiriki kutumia fursa hiyo kujadili kwa kina na kubadilishana uzoefu juu ya sera, mipango na kujenga mtandao wa masuala ya maendeleo ya kitaaluma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kutoa fursa ya kuwakutanisha kwa pamoja wataalamu hao na kujenga uelewa wa pamoja juu ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. 

Aliongeza kuwa Mkutano huo, unatoa fursa za kujadiliana kwa pamoja juu ya mafanikio na njia za kukabiliana na changamoto kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi kwenye masuala hayo. 

“Mkutano huu ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi wa kada hizi kwa minajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini,” alisema Dkt. Mpango.

Kwa mujibu wa ratiba ya mkutano huo, Mada mbalimbali zinawasilishwa kwa kutilia mkazo masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayojitokeza hivi sasa, ambapo mkutano huo unajadili masuala ya Maendeleo ya Tasnia ya Wapanga Mipango (wachumi, maafisa mipango na watakwimu) na Maandalizi ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/16 – 2020/2021).

Mada nyingine ni pamoja na Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma ambao una lengo likiwa kuimarisha utendaji, ufanisi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya miradi na program za maendeleo. Pamoja na mada ya Namna bora ya kujiandaa na Uchumi wa Gesi. 

Washiriki wa mkutano huu ni pamoja na wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.
 

Na Mwanaharakati.

BREAKING NEWS!!! POLISI YATUMIA MAJI YA KUWASHA KUTAWANYA WAANDAMANAJI DAR

 Taarifa inasema kuwa katika maandamano hayo, polisi imemkamata mbunge wa Kawe Bi Halima Mdee, aliyekuwa akiongoza maandamano hayo ya wanawake chadema.
Tutakuletea undani wa taarifa hiyo.
Na Mwanaharakati.

Friday, 3 October 2014

NEWS ALERT!!! BALOZI KAGASHEKI UMUHIMU WA SHULE YA VIZIWI MUGEZA

Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki akihutubia katika sherehe za kuhitimu darasa la saba kwa walemavu wa kutosikia( viziwi) Mugeza mjini Bukoba.

 Katika sherehe hiyo Kagasheki amempongeza mwalimu mkuu mstaafu Bwana Rutabingwa, huku akiwasihi walimu wengine kuiga mfano wake wa kuomba kufundisha katika shule hiyo kutokana na kuwa na kazi ngumu ya kufundisha watu wenye ulemavu wa namna hiyo.
Kutoka kushoto ni mwalimu mkuu mstaafumzee Rutabingwa, mwl Nicolaus Ishababi aliyeamishiwa Ndolage, Mh Kagasheki na mwalimu mkuu wa sasa.

Balozi Kagasheki kulia akiteta jambo na dokta wa masikio DC Amin

Walimu wa kigeni katika shule hiyo wakifuatilia hotuba ya mh Balozi.

Shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya vitendea kazi, uhaba wa walimu, na miundombinu hafifu kutokana na kuchakaa kwa ile iliyowekwa tangu awali, huku mbunge Kagasheki akisema kuwa yuko pamoja nao na ataendelea kuisaidia shule hiyo kama alivyokuwa akitoa hicho kidogo alichonacho.
Na Mwanaharakati.

Thursday, 2 October 2014

HATARI; NUSURA AUAWE KWA MAPANGA

Kwasasa anaugulia katika hospitali ya mkoa na mmoja wa watuhumiwa yuko mikononi mwa polisi, tutakuletea undani wake.
Na Mwanaharakati.


BREAKING NEWS!!! MIRADI MIKUBWA KUZINDULIWA BUKOBA

Ni eneo la nje ya hospitali hiyo katika kata miembeni eneo la Nyamkazi ambapo vifaa vyote vimeshakamilika tayari kwa kutoa tiba.

Mkurugenzi wa COSAD Smart Baitani akionesha sehemu ya kuhifadhia mashuka ya hospital hiyo.

Machine ya kupimia magonjwa mbalimbali.

Ni machine ya Ultra sound

Huu ni mzani wa kisasa wa kupimia watoto.

Picha ya pamoja katika makao makuu ya ofisi za COSAD Kashura.


Moja ya studio za kurekodia wasanii ambapo pichani ni Mac Ngaiza katika majaribio ya mitambo

Nyumba ya kulala wafanyakazi wa COSAD

Picha juu na chini ni kituo cha huduma na vitabu shule ya msingi Kiteyagwa.


Picha juu na chini ni shamba la mbuzi katika eneo la Kagondo



Na Mwanaharakati.