MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 23 August 2015

MAZITO KATIKA UZINDUZI KAMPEINI ZA CCM JANGWANI DAR ES SALAAM.

Viongozi na waasisi wa CCM wameudhuria na kuongea mazito, pamoja na mwenyekiti wa sasa Mh Jakaya Kikwete, marais wastaafu Ali Assan Mwinyi, na Benjamin Mkapa , makamu wa rais Gharib Bilali na waasisi wengine wa chama hicho kama Jaj Warioba, Yusuph Makamba na mtoto wa Mwl Makongoro Nyerere na wengineo.

Makundi mbalimbali yamejitokeza na kueleza mapendekezo yao ambapo miongoni mwa waliowakilisha ni mwenyekiti msaidizi wa machinga mkoa wa Dar es salaam , mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu Tz na mwenyekiti wa bodaboda.
Jaji Joseph Sinde Warioba; amewaeleza watanzania kuhusu sifa za wagombea wa CCM kuwa chama kimetazama sifa tatu, uchapa kazi, uadilifu na uzalendo.

Amesema kuwa ukizungumzia uchapakazi wa magufuli ni lazima uutazame katika vipindi vitatu alivyoudumu katika wizara kadhaa hasa ya ujenzi ambayo imeiunganisha Dar es salaam na mikoa yote Tanzania kwa barabara, akifanya kazi ndani na nje ya serikali.
Jaji huyo mstaafu, amesema kuwa alipewa kazi na rais mkapa katika awamu ya tatu, ambapo alikuwa akichunguza rushwa na kugundua ufisadi mkuu ulikuwa katika ujenzi ambapo katika kipindi cha miaka 20 tangu kuchunguza, Magufuli ameingia katika wizara hiyo kwa miaka 15 sasa na hakuna tena taarifa za ufisadi katika ujenzi kama ilivyokuwa awali.
Chanzo kikuu cha ufisadi, amekitaja kuwa ni kukaa karibu kwa viongozi na mafisadi, kwani taifa lina matatizo ya kuporomoka kwa maadili ambapo kiongozi bora anatakiwa kuwa mzalendo bila kuwa na makundi ila kundi moja ambalo ni watanzania.

Ameongeza kuwa mabadiliko yanayotajwa na baadhi ya watu tayari yamefanywa na CCM kwa kiasi kikubwa kwa mara ya kwanza baada ya kuweka wagombea wenye sifa hizo tatu na kubwa zaidi kumweka mwanamke kama makamu wa Tanzania.

Rais wa Zanzibar na mwakilishi wa baraza la mapinduzi;  Dr.Ali Mohamed Shein
amesema kuwa ni wakati wa watanzania kuenzi kazi kubwa iliyofanywa na Magufuli, na wazanzibar wanayatambua, wakatuma salamu zao ili kudhiilisha ukweli wao, akisisitiza kuwa uongozi siyo wa kujaribu hiyo watanzania wawe makini.






Rais mstaafu wa awamu ya pili; Ali Assan Mwinyi amesema kuwa upinzani ni muhimu na upo siku nyingi lakini siku imefika wao kuazima viongozi na dhamira ya waliokwenda wameenda kuongeza nguvu ili kuishinda CCM lakini yawezekana ikawepo CCM mbili A na B.

Rais wa awamu ya tatu; Benjamin Willaim Mkapa, amesema katika hao nane walioteuliwa na tume ya uchaguzi, watanzania watazame timu bora kwasababu ndiyo itasukuma maendeleo yao lakini watambue kuwa hapa nchini kuna chama kimo tu cha ukombozi, huku akikumbusha sifa za viongozi madhubuti kuwa ni wale wanaotekeleza imani za wananchi kwa vitendo, kushiriki na wenzao, kuwa mstari wa mbele kutekeleza mambo ya umma kupitia ccm, wakati wote mfano kauli zao na mtazamo wao kwa kutokuwa wazululaji.

Haitoshi kusema tu kuwa unachukia umaskini bali masharti na taratibu za kuondoa umaskini.

Saturday, 22 August 2015

YANGA AMTANDIKA AZAM

Matokeo ya Dar Young Africans na Azam fc yamemalizika kwa yanga kumtandika azam kwa penart 8-7 na mtanange umemalizika kwa yangu kumbana azam kushindwa kupata ushindi mara tatu tangu ashiriki mashindano hayo.
Na Mwanaharakati.

WAGOMBEA UBUNGE WALIORUDISHA FORM MANISPAA YA BUKOBA


Ni Balozi Kagasheki ambaye amerudisha form hizo tayari kuanza kampein katika jimbo la Bukoba mjini, ambapo ahadi yake ni kueleza sera kupitia Ilani ya chama alichopitia cha CCM.
Mkurugenzi manispaa Aron Kagurumjuli kulia akipokea form za Mh Kagasheki.
Mwingine ni mgombea kupitia ACT Wazalendo, ambaye amesema kuwa chama chake kina mwongozo bora na tofauti na vyama vingine nchini hivyo wanajua jinsi ya kusogeza karibu maendeleo ya wananchi.

Mwingine ni kutoka TLP ambaye pia amesema wamejipanga vizuri kuchukua nafasi ya ubunge katika manispaa ya Bukoba ingawaje wanatambua kuwa hawana wananchama wengi Bukoba mjini.

Wilfred Muganyizi Lwakatare, yeye amerudisha form kupitia CHADEMA, akisema kuwa sasa ni wakati wake kurudia nafasi ya ubunge katika jimbo husika. 

Na Mwanaharakati.

VIDEO; SUMAYE AIHAMA CCM CHAMA ALICHOJIUNGA NACHO SIRI YAKE



. Asema lazima akina Mbatia wafundishwe,
. Aungana na wanaotafuta mabadiliko.

Ni aliyekuwa waziri mkuu katika awamu ya tatu chini rais Benjamin Mkapa, Frederick Sumaye, amesema amepata Baraka za familia yake ambayo ni ya kaskazini, kwa lengo la kuungana na wanaotafuta maendeleo ndani ya CCM.
Itakumbukwa kuwa ni waliokuwa mawaziri wawili  kuondoka ndani ya CCM, yeye pamoja na Mh Edward Lowasa, baada ya kutochaguliwa kugombea urais kupitia CCM, kwani walikuwa miongoni mwa watia nia 42 kupitia chama hicho, ambapo John Mgufuli aliteuliwa na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho. 

Na Mwanaharakati.

Tuesday, 18 August 2015

MELI ILIYONUSURIKA KUZAMA BUKOBA


Ni meli iliyoanza safari zake mwezi    baada ya kufanyiwa marekebisho na kupelekwa ziwani kama mbadala wa Mv Victoria inayoendelea na marekebisho hadi mwezi september 2015 kwa mujibu wa  taarifa zilizopo.



 





Taarifa za jana jumatatu 17 agost 2015, zinasema kuwa Mv Serengeti, iliyokuwa ikitokea Mwanza kwenda Bukoba, ilishindwa kutia naga katika bandari ya Bukoba, na kulazimika kurudhiswa kwa umbali wa maili kadhaa karibu na kisiwa cha Musira na baadaye muda wa saa tano, naodha aliyekuwa akiendesha meli hiyo Bempele Samsoni alifanikiwa kuirudisha na kutia nanga 

Na Mwanaharakati.

Monday, 17 August 2015

MALERIA YASHUKA MAAMBUKIZO KAGERA, RTI YAMALIZA KAZI



Kiwango cha maambukizi ya malaria mkoani Kagera umetajwa kushuka tofauti na ilivyokuwa kabla ya unyunyiziaji wa dawa ya ukoko majumbani.
Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela, amesema kuwa taarifa ya utafiti wa UKIMWI na malaria mwaka 2007, inaonesha kuwa kiwango cha maambukizi ya malaria kwa watoto chini ya miaka mitano kilikuwa asilimia 41, ambapo utafiti 2011 kilishuka hadi asilimia 9 na 2015 utafiti  umeonesha maambukizi yameshuka kutoka 41% hadi 9.5%.

Pamoja na kuipongeza taasisi ya utafiti wa malaria RTI, mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa mikoa tafiti zinaonesha kuwa mikoa mingine ambayo haikuwa na utaratibu wa unyunyiziaji dawa ya mbu majumbani, kiwango cha malaria kimeendelea kuwa juu, akitolea mfano mkoa wa Lindi 35.7 kwa kupunguza kiwango kidogo hadi asilimia 29 kwa mwaka, huku Kigoma maambukizi yakipanda kutoka asilimia 19.6 mwaka 2007 hadi asilimia 26 mwaka 2011
Mkuu wa mkakati wa unyunyiziaji dawa majumbani nchini Stephen Magesa, ameiomba


ofisi ya mganga mkuu kuongeza nguvu katika vijiji vya kando ya ziwa wilayani Muleba  kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya malaria, ingawa tathmini yake bado inafanyika.








Mratibu wa RTI uhamasishaji mkoani Kagera Deodart Ngaiza, amesema unyunyiziaji wa


dawa ya kuua mbu majumbani ulianza mwaka 2007 kwa kushirikisha jamii husika ili kuondoa dhana ya imani potofu iliyokuwa imetawala kuwa zinapunguza nguvu za kiume. 
 

Amewashauri wananchi kuzingatia maelekezo ya wataalamu katika matumizi ya nyumba zilizopuliziwa kutumika sambamba na vyandarua wanavyopewa
Mkutano wa wadau wa utekelezaji huduma za afya mkoani Kagera, umefanyika kwa kuwashirikisha wakurugenzi wa halmashauri za mkoa, watendaji wa huduma za afya na waratibu

BREAKING NEWS!!! RED CROSS WAJIONDOA KUTOA HUDUMA KAGERA

. Mkoa wajipanga,
. Damu hatarini kukosekana.


Kutokana na hali hiyo, serikali ya mkoa inaangalia namna ya kukabiliana na damu kwa matumizi ya wagonjwa katika hospitali, baada ya RED CROSS ukijitoa.

Akizungumza na mwandishi wa kituo hiki, mkuu wa mkoa wa Kagera Bwana John Mongela, amesema kuwa kujiondoa kwao kunatokana na kumalizika kwa mkataba kati ya serikali na shirika la msalaba mwekundu(RED CROSS), ambayo ameelezea kuwa ni jambo zito na linahitaji nguvu za pamoja kwasababu ya unyeti wake hivyo inapaswa kufanyiwa haraka
Amesema kuwa wamefanya kazi hiyo kwa kipindi kirefu katika program mbalimbali tofauti na suala la damu salama, hivyo viongozi na wananchi, ni wakati kukaa pamoja katika kukabiliana na hali hii.

Taarifa ya shirika la msabalaba mwekundu Tanzania kwa ufadhili wa serikali ya Marekani CDC, ambao umekuwa ukikusanya damu kutoka wilaya zote na kupelkwa mwanza kwa upimaji na kuhakikisha inavifikia vituo vyote vya usambazaji, limetoa taarifa kuwa  ufadhili wake kwa TRCS umefikia ukomo October mwaka huu na RED CROSS kusitisha huduma zake mkoani Kagera.

Kuondoka kwa red cross kunaipa jukumu serikali kujipanga na kuratibu huduma hiyo bila ufadhili, na inashauriwa kuwatumia watalaamu ambao wamekuwa wakifanya kazi hiyo kupitia ufadhili ili wasaidie kwa utalamu wao kupitia bajeti ya serikali kila mwaka.

Na Mwanaharakati.