MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 20 May 2017

VIDEO;WALIMU 28 WAMALIZA SEMINA YAO CHINI YA UDHAMINI WA JAMBO BUKOBA


By Lameck Richard


Walimu 28 kutoka shule za msingi kumi na nne za halmashauri ya wilaya Bukoba  wamekabidhiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya semina fupi iliyoanza may 15 mwaka huu ambayo ilikuwa inaendeshwa chini ya ufadhili wa shirika la JAMBO BUKOBA.

Akikabidhi vyeti hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Bukoba,Afisa Michezo wilaya hiyo Bw,Gosbert Kamuntu amelipongeza shirika la Jambo Bukoba linaloendeshwa kwa ufadhili wa Clemens Mulokozi kwa kazi nzuri wanayoifanya huku akiwasihi wazazi na walezi kuruhusu watoto wao kushiriki michezo kwani michezo ni ajira na ni sehemu mojawapo ya kuendeleza vipaji vyao.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa shirika la jambo Bukoba Iman Paul amesema kuwa mwaka 2008 walianza rasmi kutoa semina kwa walimu wa shule za msingi mbalimbali ndani ya manispaa ya Bukoba na halmashauri ya wilaya Bukoba ambapo kufikia may 19 mwaka huu wamekamilisha zoezi hilo kwa wilaya hizo mbili,na semina zinaendelea kutolewa kwa wilaya nyingine zote za mkoa wa Kagera .

Aidha amesema kuwa malengo ya shirika la Jambo Bukoba ni kuendeleza vipaji vya watoto kupitia michezo ndani ya mkoa wa Kagera kwa kujali usawa wa kijinsia,kutoa elimu ya ukimwi na elimu kwa ujumla.

Bi,Paul ameongeza kuwa pamoja na kuendesha michezo hiyo wamejikita pia katika kuboresha miundombinu katika shule za msingi mbalimbali ndani ya mkoa wa Kagera kujipatia kiasi cha shilingi milioni nne ambazo huzitoa kwa kila timu inayoshiriki bonanza la mkoa na ufanyika mara moja kwa mwaka.

Kwa upande wa wakufunzi katika semina hiyo mwl William Magesa na Bi,Macleth Joseph{Mrs Kamuntu}wamewasihi wahitimu wote kuhakikisha wanakuwa balozi wazuri kwa kuwafundisha wanafunzi wao  michezo yote waliyojifunza  kupitia semina hiyo .

Sanjali na hayo,wahitimu wamelipongeza shirika la jambo Bukoba kwa kuanzisha mafunzo hayo huku wakisema awali walikuwa na changamoto kubwa kimichezo lakini kuanzia sasa wanahaidi watafanya vizuri zaidi kwa wanafunzi wao kwa kuwafundisha kile walichokipata ndani ya semina hiyo.

UNAWEZA KUTAZAMA FULL VIDEO HAPA  YA MENEJA MRADI Iman Paul………….....


Na Mwanaharakati.

Thursday, 18 May 2017

VIDEO; KUMALIZIKA MITIHANI YA KIDATO CHA SITA KAGERA.



Mitihani ya kidato cha sita imekamilika leo kitaifa ambapo mkoa wa kagera umethibisha kuwa mtihani huo umemalizika  salama bila kuwepo udanganyifu wa aina yoyote.

Afisa Elimu mkoa wa Kagera Aloyce Kamamba amesema kuwa kwa mujibu wa taratibu, mitihani yote imefanyika salama na mpaka sasa kamati ya mtihani ya mkoa imesema hakuna tukio lolote ambalo limepokelewa kwamba kuna udanganyifu wowote ambao umefanyika katika kituo chochote mkoani humo.



VIDEO YA AFISA ELIMU MKOA KAGERA


Na Mwanaharakati.

KAULI NZITO ZA MADEREVA BUKOBA BAADA YA BARABARA ILIYOKUWA IMEKATIKA KUANZA KUTUMIKA.


Mnamo may 12 mwaka huu barabara ya kemondo iliyopo halmashauli ya wilaya Bukoba ilikatika kutokana na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia siku hiyo na kukatisha mawasiliano kwa wanaotegemea barabara hiyo hususani magari ya kutoka Bukoba mjini kuelekea mikoani na wilaya jirani kama Muleba ambao walilazimika kupitia barabara ya Katerero,Kyetema na Kanyinya.



Barabara hiyo iliyokuwa ikiendelea na ukarabati leo imeanza kutumika kwa magari yote,ambapo baadhi ya madereva wameipongeza serikali kwa jitihada ilizozionyesha kwan awali walikuwa wanapata changamoto kubwa kutokana na msongamano wa magari katika barabara waliyokuwa wakitumia huku wakisubili ukarabati ukamilike.

Aidha wameishauri serikali kukarabati barabara ya Katerero-Kyetema-Kanyinya maana imeharibika sana kwa kipindi ilichotumika na inaweza kusababisha changamoto nyingine kwa wakazi wanaoendelea kutumia barabara hiyo.

Kwa upande wake meneja wa TANROAD mkoa wa Kagera mhandisi Andrew Kasamwa amesema kuwa barabara hiyo ya Kyetema-Kanyinya imekuwa ikiendelea kutumika katika kipindi hiki cha mpito, ingawa, tayari wameshaanza ukarabati wa maeneo yaliyoharibika.

VIDEO YA BAADHI YA MADEREVA  …………………......


Na Mwanaharakati.

Friday, 12 May 2017

SAFARI ZIMEKWAMA BUKOBA BAADA YA BARABARA YA BUKOBA DAR ES SALAAM KUMEGUKA



Wakala wa barabara nchini TANROADS mkoani Kagera, umepeleka mkandarasi katika barabara kuu ya Bukoba kwenda Muleba iliyomeguka na kushindwa kupitika, ili kuanza kazi ya ujenzi maramoja.

Akizungumza na mwandishi wa kituo hiki katika eneo la Bulila kijiji Kanazi kata Kemondo Bukoba vijijini, meneja wa TANROADS mkoani humo mhandisi Andrew Kasamwa, amesema kuwa wamechukua hatua za awali kuwaelekeza watumiaji kupitia  barabara ya Kanazi kutokea Kanyinya, huku mkandarasi akianza kazi ya ukarabati kwa kuweka daraja kwenye eneo lililoharibika.

Amemtaja mkandarasi aliyekabidhiwa kazi hiyo kuwa wa kampuni ya ABEMULO, na kuwa wamemtaka akamilishe kazi hiyo haraka, kutokana na umuhimu wa barabara hiyo kuu kama kiunganishi cha mkoa wa Kagera na mikoa mingine nchini.

Badhi ya wananchi wa eneo hilo, wamesema kuwa Calvat iliyosombwa na maji ya mvua iliyonyesha kuanzia usiku wa kumakia leo, ilikuwa imeanza kuwa na nyufa, huku mtendaji wa kata hiyo Silianus Sostenes akisema kuwa tatizo kubwa limetokana na uchafu uliokuwa umeziba na kusababisha maji yaanze kupita pembeni.

Gharama za matengenezo ya eneo hilo zitatolewa baada ya tathmini kamili kufanywa na kamati ya ujenzi na vikosi vya ulinzi na usalama.
 

Na Mwanaharakati.

Wednesday, 10 May 2017

HAWA NDIYO WABUNGE WA CHADEMA AFARIKA MASHARIKI EALA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepiga kura leo na kuyapitisha majina mawili ya wanawake pekee Bi. Josephine na Maasah kati ya sita waliojitokeza kugombea nafasi hiyo.

Kati ya wagombea hao alikuwamo Laurence Masha, Ezekia Wenje ambao waliokuwa wamegombea na kukataliwa kwa kutokidhi taratibu, Prof Abdallah Safari, na Salum Mwalimu.
Na Mwanaharakati.

MWALIMU ALIYEFARIKI KATI YA 36 WA LUCKY VICENT AZIKWA KAGERA .









Mwili wa aliyekuwa mwalimu wa St. Lucky Vicent,Innocent Papian miaka 25 ambaye ni miongoni mwa watu 35 waliopata ajali may 6 huko Arusha na kupoteza maisha jana mwili wake umefikishwa wilayani kwao Kyerwa mkoani Kagera na kuzikwa.

Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey Mheruka akiwakilisha serikali ameongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Kagera na nje ya mkoa katika mazishi ya mwalimu huyo,huku akisema kuwa mwalimu Innocent enzi za uhai wake alikuwa anaiwakilisha vyema wilaya ya Kyerwa pamoja na Taifa kupitia taaluma yake ya uwalimu kwani alikuwa mtumishi ambaye hatiliwi shaka lolote kwenye vyeti vyake.
SAUTI YA MKUU WA WILAYA KARAGWE   

Kwa upande wake afisa elimu taaluma mkoa wa Kagera mwl,Fides Munyogwa amesema kuwa mkoa umepata pengo kubwa maana ni kijana ambaye ndo alikuwa ameingia kwenye taaluma lakini malengo yake yameishia njiani.

Pia Mwl,Munyogwa amewasihi wananchi kutoingiza imani yoyote juu ya kifo hicho kwani ni mapenzi ya Mungu badala yake wamuombee apumzike kwa amani.
"Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe".

MWISHO.

 

Na Mwanaharakati.

Tuesday, 2 August 2016

SAMAHANI KWA KUTOKUWA HEWANI

Hii ni baada ya kuwa kwenye marekebisho na utafiti wa masuala kadhaa ya kijamii, tunarejea sasa kwenye majukumu.