MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 24 July 2017

AUDIO; Mwananchi aliyeomba fedha za shule kwa rais afichua siri Kagera.



Bwana Pastory Kafundi ni mwananchi mkaazi wa kijiji cha Ngalalambi katika halmashauri ya wilaya Biharamaulo, ambaye alitumia nafasi yake kuomba rais awasaidie kuchangia ujenzi wa darasa katika shule ya msingi Mizani, baada ya wanafunzi kusomea chini ya mti tangu januari mwaka huu.

Akizungumza na macmedianews, mwananchi huyo amesema kuwa aliamua kujitoa muhanga kumweleza rais suala hilo, baada ya kuona kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaofikia elfu tatu katika shule hiyo ya msingi, na hata wengine kusomea chini ya mti ilhali wazazi na walezi wakiendelea kujitolea kujenga bila mafanikio kutokana na kukabiliwa na kero za miundombinu ya maji.


.
Mtandao huu umetembelea darasala hilo chini ya mti na kukuta mwalimu wake akiendelea kufundisha, kwa lengo la kujua kero anazokabiliana nazo katika ufundishaji wake huo.

Imebainika kuwa analazimika kutumia nguvu nyingi kuwashawishi watoto hao ambao mara nyingi wanapoteza muda kushangaa magari na wapita njia kutokana na mti huo kuwa karibu na barabara.


Wakati akipita katika kata ya Nyakaula, rais Magufuli alisimamishwa na kundi la wananchi wakitaka asikilize kero zao, ndipo mmoja wa wananchi aliyejieleza hapo juu, alipojitolea kumweleza rais hitaji lao juu ya ujenzi wa madarasa, na kumlazimu rais kutoa ahadi ya shilingi milioni 10 ambazo alizikabidhi kwa mkuu wa mkoa siku akihitimisha ziara yake Kagera kuelekea mkoani Kigoma.
Akikabidhi fedha hizo kwa uongozi wa shule na mbunge wa jimbo la Biharamulo, mkuu wa mkoa wa Kagera meja jenerali mstaafu Salum Kijuu, aliwataka viongozi na wananchi kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, nayeye kuwiwa kuchangia mifuko 10 saruji baada ya kuridhishwa na ujenzi unaoendelea shuleni hapo





Na Mwanaharakati.

AUDIO; Mbunge ashambuliwa na wananchi wake Biharamulo, mjane azuiliwa kuonana na RC.

Wananchi katika halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera, wamemlalamikia mbunge wa jimbo la Biharamulo, kutoonekana jimboni kwa kipindi kirefu mpaka rais alipofanya ziara.

Wakizungumza kwa jazba baada ya kumwona mbunge huyo kwenye mkutano wa rais Magufuli, wananchi hao wamesema kuwa wanazo kero nyingi ambazo kama angekuwa amezichukua kupitia nafasi yake ya mbunge zingeshafanyiwa kazi na serikali, hivyo hakuwa na sababu ya kuja wakati wa mkutano wa rais wala mkuu wa mkoa.
.
Katika maelezo yake kwa wananchi hao mbunge  Oscar Mkasa, amesema kuwa amekuwa akibanwa na shughuli za kibunge, ingawa mara nyingi amejitahidi kushughulikia baadhi ya kero za wananchi wake, akitaja mgogoro wa wafugaji wa Miongora kuwa aliutatua yeye, pamoja na kuomba shilingi milioni 200 za maji, katika mradi utakaotekelezwa na serikali.

Wakizungumza na mwandishi wa kituo hiki, wananchi wa kata ya Nyakaula katika halmashauri ya Biharamulo, wametaja kuwa wanakabiliwa na kero ya ukosefu wa huduma ya maji, uhaba wa vyumba vya madarasa mpaka kuwalazimu kutaja kero hiyo kwenye mkutanio wa rais, na baadhi yao kuchukuliwa maeneo kwa kufanyika uwekezaji wa visima vya maji bila fidia.
Bi. Mastula Hamis yeye ardhi yake ilitwaliwa na uongozi wa kijiji na kujengwa visima vya maji, lakini wakakiuka makubaliano ya kuwa analipwa kila mwisho wa mwezi na kuandikiwa barua kuwa atafidiwa eneo lingine ambalo hatahivyo hakuwahi kupewa, huku akizuiliwa kuwafikia viongozi wa ngazi ya juu mamlakani.

Akiwa ziarani mkoani Kagera, rais wa jamhuri ya muunagno wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, aliwahidi wananchi kuwa atamtuma muhandisi wa maji, ili aweze kushughulikia huduma hiyo, kwani hilo ni jukumu la serikali, na kuchangia shilingi milioni 10 za ujenzi wa darsa katika shule msingi Mizani.
 

Na Mwanaharakati.

Mapacha walioungana wazaliwa tena nchini.

Watoto wawili walioungana kuanzaia kifuani mpaka tumboni wamezaliwa kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Misheni ya Bigwaa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Huku hali ya mama na watoto hao ikiendelea vyema na mapacha hao wakiwekwa kwenye chumba maalumu kwa uangalizi, ingawa wamezaliwa wakiwa wametimiza miezi 9 kama kawaida.

Baba mzazi wa watoto hao Luka Kimole amesema kuwa ni suala la kushangaza kupata watoto kama hao lakini kwakwe katu halichukulii kama mkosi bali neema ambayo imetoka kwa Mungu.

Kaimu Mganga mkuu wa hospitali ya Berega anasema kuwa hali hiyo kujitokezakatika  miaka ya sasa ni kutokana na malezi ya ujauzito.

"Mara nyingi akina mama wanapokuwa wajawazito hushauriwa kutumia baadhi ya huduma za tiba, kwa mfano Ferav na Folic ambazo zinawasaidia kwakiasi kikubwa kuzuia watoto kuzaliwa katika hali kama hizi lakini katika hili hatuwezi kuongea zaidi ni uchunguzi zaidi utafanyika kuona ni kwanini hali kama hzi hujitokeza kwa wingi hasa miaka ya hivi karibuni.

" Kwa nje waweza kuona kama watoto wawili ni vigumu kujua jeh kwa ndani ni miili ya wawili tofauti au kuna kitu kimoja kinawaunganisha, hivyo kuona kama inaweza kufanyika huduma ya kutengenisha.



Na Gsengo

Sunday, 23 July 2017

Mkurugenzi wa halmashauri asimamishwa kazi kwa matumizi mabaya ya fedha.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Bw. Eliseyi Mgoyi pamoja na maofisa wengine watatu kwa  tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma.


Pia amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Songwe, Bw. Damian Sutta kuwakamata na kuanza kuwachunguza haraka maofisa hao na kisha ampelekee taarifa ofisini kwake.


Waziri Mkuu amewasimamisha kazi maofisa hao leo (Jumapili, Julai 23, 2017) wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Vwawa, akiwa katika ziara yake ya kikazi.


Maofisa wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo ni Bw.

BREAKING NEWS: Upinzani wapanga migomo na uvunjaji sheria kumuondoa rais madarakani.



Upande wa upinzani katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, umetangaza mpango wa migomo na kuvunja sheria, kujaribu kumlazimisha Rais Joseph Kabila aondoke madarakani.


Mgomo wa jumla wa siku mbili utaanza tarehe 8 Agosti, na maandamano ya pamoja yamepangwa kufanywa baadaye mwezi ujao, katika kila jimbo la nchi.


Katika taarifa yake, upinzani umesema, ikiwa Rais Kabila hato-taja siku ya uchaguzi ufikapo mwisho wa mwezi wa Septemba, basi watu waache kulipa kodi kwa serikali.


Muhula wa rais ulimalizika mwaka jana, na makubaliano yaliyofikiwa baada ya Kanisa Katoliki kupatanisha, ni kwamba atabaki madarakani hadi Disemba mwaka huu, lakini rais baadae alisema, hakutoa ahadi yoyote.
 

Na Mwanaharakati.

Rais atoa mwezi mmoja kwa waziri wa ujenzi.

Akihutubia wananchi wa jimbo la Kaliua, rais Magufuli amesema kuwa anataka awape raha wananchi wa Kaliua, kwamba serikali anayoisimamia, kukusanya na kutumbua pesa za wabadhilifu haiwezi kushindwa kujenga barabara.



Hatahivyo rais Magufuli amesema kuwa wananchi wote waliojenga kwenye hifadhi ya njia ya reli, wajiandae kisaikolojia kubomolewa na kupisha ujenzi wa reli mpya ya standard gauge, kuwa yeye hapendi kupindisha sheria, na kuagiza kuwa wakati wa kubomoa, waanzie na nyumba za viongozi wa CCM wanaopita na kuwadanganya watanzania kuwa wasiondoke kwenye maeneo hayo.


Amesema kuwa ameamua kutumia barabara kutoka mkoani Kagera hadi atakapofika Dar es salaam, kwa lengo la kuangalia vipande vya barabara ambavyo vimesalia bila kujengwa kwa lami, na kumwagiza waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano, kujenga barabara yenye urefu wa kilomita 28 kwa kiwango cha lami kutoka Kaliua kwenda Urambo.
................BONYEZA CHINI KUSIKILIZA...............

Na Mwanaharakati.

AUDIO; RAIS MAGUFULI ASISIMUA WATANZANIA JUU YA KAFULILA



Rais wa jamhuri ya muhungano wa Tanzania, amezindua mradi wa maji wilayani Uvinza mkoani Kigoma, kabla ya kufanya uzinduzi wa barabara ya Kaliua yenye kilometa 56 mkoani Tabora.


Wakati wa uzinduzi huo wa mradi wa maji wa Nguruka wilayani Uvinza, rais Magufuli amesema kuwa mradi huo unaogharibu shilingi bilioni 2.8, ni muhimu wananchi wautunze kupitia viongozi wao, huku akiwahidi wananchi kuwa kama rais ataanza kufanya mipango ya kufikisha huduma ya umeme.


Pamoja na kufanya uzinduzi huo, amemwagiza waziri wa maji Gerson Lwenge, kuwaondoa watumishi wanaokwamisha miradi ya maji kutelezeka haraka, akisema kuwa yeye kama rais ataondoa walioko ngazi za juu lakini wa ndani ya wizara waziri anao uwezo wa kuwaondoa bila hata kumwomba rais ushauri.

Rais Magufuli amempongeza aliyekuwa mbunge wa Uvinza David Kafulila, juu ya kutetea haki za watanzania wasiendelee kuibiwa juu ya kuibua hoja ya IPTL na kuisimamia, kwamba alisimamia wizi huo wa ajabu, ingawa wapo waliombeza na kumtukana kwamba hata kama walimtukana lakini ukweli wake unaonekana.
..........BONYEZA HAPA CHINI KUSIKILIZA......... 



Amesema kuwa barabara ya kutoka Maragarasi kwenda Uvinza kilomita 50 na nyingine zilizosalia zitatengenezwa kwa kiwango cha lami, na kumpongeza kiongozi mmoja wa kidini aliyejitolea kujenga kituo cha afya na kukikabidhi kwa serikali kwa lengo la kusaidia wananchi wa Uvinza, ambapo rais alichangia shilingi milioni 10 zilizowezesha kununuliwa kwa vitanda na majokofu. 

Na Mwanaharakati.

Saturday, 22 July 2017

BREAKING NEWS;GARI LAPINDUKA HAMGEMBE


Gari aina ya Nissan Hiace lenye namba za
usajili T803 DCJ lmepinduka maeneo ya Hamgembe lakini inasemekana halijaua mtu yeyote

Kwa taarifa za awali ni kwamba dereva alikuwa anatokea barabara ya Mtukula anaingia Bukoba mjini alipofika Kona ya Nyangoye likapinduka, alikuwa amepakia madumu ya maziwa na mahindi.

Picha za ajali hiyo........................






Na Mwanaharakati.