MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 31 January 2015

PICHA MBALIMBALI AJALI MAYA YA MEYA NA WAANDISHI HABARI MOROGORO

Wasamalia wakimuwahisha Hospital,Mmoja wa majeruhi mara baada ya kupata ajali eneo la Mzambarauni Darajani -Msamvu barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Rajab Rutengwe akionesha eneo ambalo gari la namba SM 4151 Nissan iliyokuwa ikitumiwa na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo , ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam .Meya huyo na watu wengine watatu walijeruhiwa na kupimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kulazwa wakindelea kupatiwa matibabu.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo ,(45) akiwa amelazwa wodi namba tano ya daraja la kwanza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari yake SM 4151 ilipogongwa Januari 30, mwaka huu saa 9: 30 alasiri eneo la Mzambarauni Darajani , Msamvu Barabara kuu ya Moro- Dar na Basi la Abiria aina ya Scania yenye namba za usajili T 831 CEH (Happy Africa ),iliyokuwa ikitokea mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam ,mbali na Meya huyo na watu wengine watatu ,Dereva Mwambala Ally (55), na waandishi wa habari , Anita Chali (30) pamoja na HUSSEIN Nuha (28) pia walijeruhiwa na kulazwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu. ( Picha na John Nditi).
Mwandishi wa habari,Anita Chali akiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kujeruhiwa kufuatia gari waliyoipata,walipokuwa kwenye kazi na Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Basi lililogongana na Gari ya Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo.
Na Mwanaharakati.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 31 JAN 2015


Na Mwanaharakati.

SOMA TAARIFA YA KUPOTEA KWA DC KIPUYO AKIELEKEA KISIWANI GOZIBA WILAYANI MULEBA

Taarifa tuliyopokea inasema  kuwa mkuu wa wilaya ya Muleba Lembris Kipuyo aliondoka jana asubuhi na timu yake ya ukaguzi kuelekea kisiwani Goziba kwaajili ya kujionea hali ya wananchi na mazingira kutokana na dhoruba iliyowakumba.

Safari ya kutoka Muleba hadi Goziba ni kwa muda wa saa 6 tu, lakini wenyeji walishangaa kuona hawafiki walau saa 5 za asubuhi kwasababu walikuwa Boat yenye kasi kubwa, ikabidi waaanze kufuatilia taarifa zao,

Walifanya mawasiliano wilayani wakasema mkuu huyo wa wilaya ameondoka asubuhi lakini wakadai kuwa hawana taarifa nyingine kama amerudi bila kufika kisiwani humo, ndipo uongozi wa kisiwa ukaanza kuwatafuta ziwani, na kufanikiwa kuwapata wakiwa wamekwama ndani ya ziwa Victoria.

Kilichofuatia ni kuwavuta kutumia mtumbwi mwingine baada ya kukuta wameharibikiwa na waliokuwa nao, ambapo walifanikiwa kufika kisiwani Goziba saa 4 usiku wa kuamkia leo.

Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi, lakini mpaka sasa wakaazi ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo kisiwani humo wanaishi kwenye jengo la zahanati na wengine kadhaa wamelazwa hospitali ya mkoa Kagera baada ya kujeruhiwa na mabati yalioezuka juzi alhamisi.
Na Mwanaharakati.

Friday, 30 January 2015

HATARI KWA WAFANYAKAZI WA KITANZANIA VIWANDANI PWANI





Ni kutokana na baadhi ya wamiliki wa viwanda mkoani humo kukiuka sheria za usalama mahali pa kazi kwa kuwafanyisha kazi kinyume na taratibu.

Hali hiyo ya kuhofia kukamatwa imekuwa ikiwafanya kufunga Geit za viwanda vyao ili wakaguzi wa serikali wasiwafikie kama inavyoonekana katika kiwanda cha BLANKETS & TEKTILE cha Mkuranga, huku Tanzania Gyp sum waliofungua wamebainika kuwanyanyasa wafanyakazi kwa kuwanyima vitendea kazi huku wakifanyika katika eneo lenye hali mbaya ya hewa.

Kiwanda hicho kinajihusisha na utengenezaji wa GYPSUM ambazo hutumika kwenye ujenzi ambapo utengenezaji wake unahitaji vifaa kama boots, groves na vifaa vya kuvaa usoni, lakini wao wanakiuka kama picha moja inavyoonesha mfanyakazi akiendelea kuteseka kazini hapo juu, huku weneyewe wachina wakijifungia kwenye vibanda vidogo vya vioo wanavyotengeneza na kuwekea vioyozi ili waendelee kusimamia utendaji kazi.
 

Na Mwanaharakati.

TPA KEMONDO YATAJWA KWA UNYANYASAJI WA ABIRIA WA VISIWANI, WAANDISHI WASHUUDIA KAGERA








Inatokana na kero ya kutozwa sh 600 kwenye eneo la kupandia Boat ziendazo visiwani, kwa kila anayepanda na kushuka, jambo ambalo kwao wameona ni kero ilhali eneo lenyewe ni bovu na kuwafanya wakati mwingine kudonoka kwenye maji kama unavyoona kwenye picha.

Wanasema kuwa wakihoji wanaambiwa hizo ni kwa ajili ya matengenezo ya eneo, jambo ambalo linawashangaza kwani hadi sasa hakuna matengenezo yoyote, huku wakisema kuwa mia sita kwa kupanda na kushuka ni kiasi kikubwa hata kama ni matengenezo haifai, huku wakiomba SUMATRA kuingilia kati.
 

Na Mwanaharakati.

MAGAZETI YA LEO 30 JAN 2015

Na Mwanaharakati.

MSAADA WA HARAKA KWA WAATHIRIKA WA DHORUBA KISIWANI GOZIBA ZIWA VICTORIA



Ni baada ya dhoruba iliyowakumba jana na kusababisha kifo cha mtu mmoja huku wengine zaidi ya 30 wakifikishwa usiku katika hospitali ya mkoa kwa matibabu baada ya kujeruhiwa na mabati ya nyumba zilizoezuka.

Taarifa ya mtendaji wa kata Goziba Bw Nason Bahemuka, inasema kuwa mtumbwi uliosadikiwa kuzama haukuzama japo ulipoteza mawasiliano baada ya kupotea njia na wataitolea taarifa baadaye.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Bw John Mongera, anataraji kufika kisiwani humo wakati wowote kutoka sasa, kutokana na umbali uliopo kuwa usafiri wa fiber boat spa 40 unatumika muda wa saa6 kutokea Muleba mjini Muleba kufika Goziba kisiwani.
 

Na Mwanaharakati.

Thursday, 29 January 2015

BREAKING NEWS!!! BOAT YASADIKIWA KUZAMA NA WATU WANAOSADIKIWA KUFIKIA 30 HUKU NYUMBA KADHAA ZIKIEZULIWA KWA UPEPO MKALI KAGERA

Ni katika kata ya Goziba kiwani Goziba wilayani Muleba, ambapo taarifa za awali zinasema kuwa umezuka upepo mkalisaa nne leoasubuhi, na kuezua nyumba za wafanyabiashara, makaazi, kituo cha polisi na hema la shirika ICAP la kutolea huduma za kiafya kwa kina mama.

Mtendaji wa kata hiyo Bwana Nason Bahemka aliyezungumza na mtandao huu hivi punde amesema kuwa kulikuwa na Boat inayofanya safari zake kutoka Goziba kwenda Ukerewe, inasadikiwa kuzama huku ikiwa na watu zaidi ya 30 ambao hakuna ambaye ameonekana mpaka sasa hivi, huku wakiendelea kufanya mawasiliano.

Amesema kuwa kisiwa hicho chenye wakaazi zaidi ya elfu 7 wengiwao wamejeruhiwa kwa kukatwa na mabati ya nyumba zilizoezuliwa ikiwamo ofisi ya kijiji na mtoto mmoja yuko mahututi.

Mtendaji wa kijiji ametajwa kuwa anaumwa na amelazwa hospitali ya Rubya. tunaendelea kufanya nmawasiliano zaidi kutuletee undani. 
Na Mwanaharakati.

MADAKTARI WASIO NA MIPAKA KUONDOLEWA SUDAN HUKU MAMIA WAKIPOTEZA MAISHA

Shirika la misaada la madaktari wasio na mipaka MSF linasema kuwa linajiandaa kuwaondoa wafanyakazi wake wa kutoa misaada nchini Sudan kwa sababu maafisa wa serikali wanatatiza juhudi zao katika eneo hilo linalokabiliwa na mizozo.

MSF linasema kuwa serikali inafanya maksudi kutatiza shughuli za wafanyakazi hao na pia kuwazuia kufika katika majimbo ya Darfur na Blue Nile ambako maelfu ya watu wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Jeshi la Sudan linakabiliwa na kibarua kigumu kupambana na waasi katika mpaka wa Kusini mwa nchi.
Wiki jana shirika la MSF lilituhumu jeshi la nchi hio kwa kushambulia hospitali katika milima ya Nuba eneo lengine linalozozaniwa.

Na Mwanaharakati.

TAMKO LA WIZARA YA MAMBOYA NDANI KUHUSU KUPIGWA VIONGOZI NAWANANCHI CUF, NA MJADALA UNAENDELEA BUNGENI

Akitoa taarifa ya serikali muda mfupi bungeni Dodoma, waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh Mathias Chikawe, amesema kuwa polisi walijibu barua ya CUF iliyoandikwa tarehe 25 Jan 2015, na kujibiwa siku hiyo kwa kukaa kufanya mazungumzokuwa mkutanohautafanyika, makubaliano ambayo LIpumba na wafuasi wakewalikiuka,jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Amesisitiza kuwa haiwezekani polisiisifanye kaziyake kwasababu ya wananchi wanaokiuka ilhali wamebaini kutokea kwa maafaambayo yangetokana na silaha zilizoibiwa, pamoja na huwepo wamatukioyakigaididuniani.

Hatahivyomwanasheriamkuuwaserikali George Masaju, amekataa wasijadili hoja hiyo, kwa sababu sualahilolimefikishwa jana mahakamani, jamboambalo wabunge wamekataa na sasa wanaendelea kujadili,ilhali Tundu Lisu akikata maelezo waziri  na m,bunge Habibu Mnyaa akisema kuwa maelezo ya waziri ni uwongo, barua ya CUF iliandikwa januari 22 na haikujibiwa mpaka siku ya tukio tarehe 27 ambapo taratibu zote zilikuwa zinaendelea.

Ameongeza kuwa Lipumba alikubali na kuwasihiwananchiwaondoke lakini cha ajabu polisiilimfuata na kusababisha msongamno ambao hatahivyo  ulisababisha adha na yeye kupigwa.

Tunaendelea kukuletea undanina maazimio
Na Mwanaharakati.

Wednesday, 28 January 2015

MATOKEO YA SIMBA NA MBEYA CITY YANASIKITISHA

Ni baada ya Mbeya City kumtandika Simba bao 2-0 baada ya Mbeya City kusawazisha bao lililotanguliwa kufungwa na Simba, na katika dakika ya 90 Mbeya City waliongeza bao kwa njia ya Penart huku Simba wakipata penart na kugonga mwaba katika sekunde za mwisho za mpira.
Na Mwanaharakati.

BREAKING NEWS!!! WANANCHI WAVAMIA GARI LA ZIMAMOTO KWA KUCHELEWA KUFIKA ENEO LA TUKIO, TUKIO LINGINE CLUB YAUNGUA DAR TAZAMA PICHA MBALIMBALI

CLUB Olympia iliyoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam, imeungua na kuteketea kwa moto majira ya saa kumi na nusu usiku wa kuamkia leo ambapo chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika mapema.

Mlinzi wa club hiyo inayomilikiwa na Samuel Mwaisumbe, na ambaye hakuweza kujitambulisha jina lake, alisema moto huo ulianza mishale ya saa kumi usiku ambapo waliweza kutoa taarifa kwa vyombo vya zima moto.

Aliongeza kwamba zima moto hawakufika kwa muda mwafaka na badala yake walifika kunako saa 12 asubuhi wakiwa na maji kidogo ambayo yaliisha wakati moto ukiendelea.


Vyumba zaidi ya kumi na nne vimeteketea kwa moto maeneo ya Mwananyamala Manjunju kufuatia kile kilichoelezwa kuwa ni hitalifu ya umeme ambapo licha ya jitihada za wananchi za kuuzima moto na kuokoa vitu kutokuzaa matunda mamia ya wakazi wa eneo hilo wamelivamia gari la zima moto kwa madai kuwa limechelewa kufika katika eneo hilo.Fuatilia Taarifa zetu Kufahamu zaidi.
Na Mwanaharakati.