MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 30 August 2015

UPEPO WA SIASA WABADILIKA UKAWA NA CCM WAWA SUMU, MAZITO YAKO HAPA.



. Ni baada ya maneno mazito ya ACT,
. Yasema kazi ya rais inataka mtu imara,
. Chataja mambo matatu ya uchaguzi.

ACT- imefanya uzinduzi wake katika viwanja tofauti na CCM na UKAWA, baada kuzindulia viwanja vya ZAKHEM Mbagala, ambapo mshauri mkuu wa chama hicho Prof Kitila Mkumbo, ametumia dakika 10, kutaja kazi za rais, sifa na kuwasihi wananchi wapime na kuchagua October 25/2015.


Meneja wa kampeini za rais kupitia chama hicho Bw. Habib Mdunga, amesema kuwa watanzania wasidanganyike na vyama vya CCM na UKAWA, isipokuwa wakitaka ulaghai kuna vyama vitawalaghai, wakitaka mbwembwe kuna vyama vitawaonesha mbwembwe, lakini wakitaka sera waende ACT itawapa sera na utekelezaji wake.

Mgombea urais wa chama hicho ambaye ni mwanamke pekee kugombea urais katika vyama vyote Tanzania Bi. Anna Mgwila, ameeleza ilani ya ACT uku akisema mambo matatu ya utu, uzalendo na uadilifu na kuwa wamchague kuongoza taifa kwani mabadiliko yanayotakiwa kwa sifa ya kwanza ni mabadiliko ya kumpata kiongozi mwanamke Tanzania.


Na Mwanaharakati.

Saturday, 29 August 2015

MCHAKATO WA VALERIAN JIMBONI NKENGE WAENDELA

Ni katika kusaka kura za wananchi wilayani Misenyi, akigombea ubunge kupitia CHADEMA huku akitajwa kuwa na sera nzuri aikilinganishwa na wagombea wengine wa chama hicho.
Na Mwanaharakati.

SLAA KUIBUKA UZINDUZI UKAWA JANGWANI LEO?

Picha ya maktaba.
Yapo mazungumzo ya chini kwa chini na sitofahamu kuhusu Wilbroad Slaa kuibuka katika mkutano wa uzinduzi wa kampeini za UKAWA kitaifa chini ya wenyeviti wenza, huku mgombea urais na mwenza wake wakitangaza ilani ya CHADEMA.

Itakumbukwa tangu Edward Lowasa kuingia CHADEMA baada ya kukatwa na CCM kugombea urais 2015, makatibu wa CHADEMA na CUF na ambao ni waasisi wakuu wa UKAWA, waliamua kukaa kando, huku Ibrahim Lipumba akitangaza adharani kuwa anaachia ngazi na kusalia mwananchama wa kawaida, ilhali Slaa hajawahi kujitokeza popote.

Maandalizi ya UKAWA leo yameshakamilika tayari kwa mkutano wao Jangwani jijini Dar es salaam.
Na Mwanaharakati.

TAARIFA YA HIJA NYAKIJOGA HII HAPA

Baba Askofu msaidizi jimbo katoliki la Bukoba Dr Method Kilaini, anakukumbusha hija ya Nyakijoga tarehe 6 septemba, kama alivyoeleza kupitia ukurasa wake wa mtandao.
HIJA NYAKIJOGA MUGANA BUKOBA 06 SEPT. 2015
Wapendwa,
Tunawaalika katika hija ya kila mwaka ya Nyakijoga Mugana Bukoba; Lurdi ya Bukoba. Itakuwa tarehe 06 Septemba 2015. Mwaka huu hija itaobgozwa na Balozi wa Baba Mtakatifu Tanzania, Mha. Askofu Mkuu Francisco Padilla.

Karibu tumshukuru na tumwombe Mama Yetu Bikira Maria. Kwa namna ya pekee tuombee amani nchi yetu katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Mama maria Mama wa Mungu utuombee.

Na Mwanaharakati.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 29 AGOST 2015


MAAMUZI MAGUMU YA TCRA JUU YA TBC HAYA HAPA



MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA) imetoa  onyo kali  kwa television ya Taifa  TBC kwa kitendo chake cha kubagua kusoma taarifa zinazohusiana na vyama tofauti na CCM .

Hukumu hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Walter Bugoya wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Bugoya amesema kamati hiyo imebaini TBC one imekiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005  pamoja na sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 baada ya kufanya upendeleo wa vyama katika taarifa zake kwenye vipindi.

Amedai katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa tarehe 15 mwezi huu majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu,katika kipingele cha uchambuzi wa magazeti ambapo mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa anayasoma magazeti huku akiruka kusoma habari kuu husika.

Amesema Mtangazaji huyo alipokuwa anachambua gazeti la Majira na Nipashe alidanya umma jambo ambalo amedai ni kosa.

Bugoya ametaja makosa hayo ni wakati  mtangazaji huyo alipokuwa anasoma Gazati la Majira  ukurasa wake wa mbele alisema habari kubwa ni “CCM yazidi waumbua wanaomfuata lowassa” wakati habari  kubwa ilikuwa inasomeka hapo ni ile inayosema “Mbeya kwafurika”huku picha ya gazeti hilo likionyesha picha ya umati watu pamoja na mgombea wa Urais wa chadema Edward lowassa akihutubia.

Amesema mtangazaji huyo pia alifanya kosa jengine kama hilo pia wakati akisoma Gazeti la Nipashe ambapo alisema Habari iliyopewa uzito wa kipekee ni  “Mbalawa atoa sheria ya mitandao”  ambapo habari iliyopewa uzito ilikuwa ni ile ilikuwa “Mafuriko Mbeya” na sio aliyokuwa anaisoma yeye.

Amesema baada ya Kamati yake kubaini makosa hayo waliwasiliana na mkurugenzi wa TBC one Bwana Mshana ambao mkurugenzi huyo alitoa utetezi wake kwenye kamati hiyo akisema mtangazaji huyo ajafanya kosa kwakuwa alikuwa ajaridhika na taarifa zilizokuwa zimeandikwa kwenye magazeti hayo.

Sanjari na hayo Mshana alizidi jitetea akidai kuwa hata mtangazaji huyo  hata asingesoma habari ile lakini picha iliyokuwa inaonekana kwenye magazeti hayo teyari mtazamaji alikuwa ashajua kwahiyo amedai haikuwa na ulazima wa kusomwa.

Bugoya amesema baada ya kusikiliza upande wa TBC one ndio wakabaini kituo hicho kilikiukaka sheria ya utangazaji ya Mwaka 2005 ambayo inavitaka vituo vyote vya utangazaji nchini kuripoti taarifa kwa kutokuwa na upendeleo wowote.

Amesema Kamati imefikia uamuzi wa kuipa onyo kali TBC one na endapo wakiendelea basi Mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali zaidi.
 

Na Mwanaharakati.

Thursday, 27 August 2015

BREAKING NEWS; NAFASI ZA KAZI WAHITIMU FORM IV, SIX NA JKT KATIKA JESHI LA POLISI MWISHO NI MWEZI HUU

Jeshi la polisi Tanzania linawajulisha kwamba litaendesha mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi kwa miezi tisa katika shule ya Polisi Tanzania “Moshi” kuanzia taerehe 29/08/2015.

Mafunzo hayo yatahusisha wahitimu wa vyuo vikuu, kidato cha sita kidatocha nne wote wa mwaka 2014. Aidha wahitimu wa Jeshi la kujenga Taifa wa mwaka 2015 watahusika pia.
BOFYA KUSOMA MAJINA YOTE HAPA
Na Mwanaharakati.

Wednesday, 26 August 2015

HUU NDIYO UZINDUZI NA UTAMBULISHO WAGOMBEA UKAWA MANISPAA BUKOBA


Add Madiwani wanaogombea kata 14 na viti maalumu wakitambulishwa na mh. Lwakatare mbele ya mkutano wa hadhara.
Ni katika uwanja wa Uhuru (Mayunga) manispaa ya Bukoba, ambapo mgombea ubunge kupitia CHADEMA, ameongoza wagombea wenzake 14 ambao wanagombea ngazi ya udiwani. 
Mgombea ubunge wa CHADEMA Wilfred Lwakatare, ametangaza ILANI kuwa wana mipango ya kuleta maendeleo, hivyo wananchi wawape nafasi ya kuchukua uongozi.

Amesisitiza kuwa suala la mikataba ambayo imekuwa ikifanyika kwa siri yeye ataisimamia ili ijulikane kwa jamii.
Add Mgombea udiwani kupitia CHADEMA wilayani Misenyi Valerian Lugarabamu akisalimia umati baada ya kukaribishwa atoe salamu.
Ni mkutano wa kwanza wa katika UKAWA manispaa ya Bukoba, ambapo mikutano mingine ya mchakato wao utaendelea kuiona kupitia mtandao huu.
Na Mwanaharakati.

TASAF KUTOHUSIKA KUWATAMBUA MASKINI, SOMA NA SIKILIZA HAPA



Katika awamu ya tatu ya mfuko wa kaya maskini nchini, mkoani Kagera wameendelea na utaratibu wa ugawaji fedha katika kaya husika, ambapo jumla ya mil 319,060,000/= zinazotolewa kwa   walengwa 8753 Bukoba vijijini, na kiwango cha chini ni sh 20,000/= ilhali cha juu kikiwa ni sh 86,000/= kulingana na ukubwa wa familia.

Mtandao huu umeshuudia mchakato wa utoaji fedha kwa baadhi ya kaya kwenye kata za Bujugo na Karabaige, kando na hiyo kumekuwa na malalamiko juu ya mfuko huo, ikitajwa kuwa wanaopewa siyo wahusika yaani ni wale wanaojiweza na wasio jiweza kuwekwa kando.
Ismail Hamidu ambaye ni afisamratibu wa TASAF halmashauri ya Bukoba vijijini Bw Ismail, amesema kuwa wao hawahusiki  kufanya mchakato wa utambuzi kuhusu maskini, badala yake ni viongozi wa vitongoji na mitaa ambao wanaishi karibu na wahusika, ambapo taarifa zao ndizo zinawezesha kuwapa mgawo sawa kulingana na ukubwa wa kaya. 
Amesisitiza kuwa TASAF haihusiki kutambua kaya maskini bali ni kazi ya wanavijiji au mitaa husika na wao hupewa taarifa baada ya kukidhi vigezo vinavyotolewa na TASAF, hivyo malalamiko yanayojitokeza siyo ya msingi.

Amesema kuwa awali kulikuwa na wakati mgumu kuwapata wahusika, kwasababu kulikuwa na uvumi kuwa fedha hizo ni za FREEMASON lakini baada ya kugundua siyo kweli, wamejikuta wakitaka kuingizwa kwenye mchakato ilhali hawakuudhuria mikutano ya utambuzi, ndiyo maana kuna baadhi ya malalamiko kuwa wamebaguliwa.


Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Bukoba Bi Jenista Lugakingira, amesema kuwa serikali inaendelea kutekeleza mipango yake kwa wananchi, kwani inatambua umuhimu na mahitaji katika kusukuma mbele maisha yao, huku akiwasihi kujitokeza kupiga kura kumchagua kiongozi wanayemtaka, ifikapo oktoba 25 mwaka huu.

Na Mwanaharakati.

Tuesday, 25 August 2015

MRATIBU UCHAGUZI AELEZA WALIOENGULIWA KUGOMBEA BUKOBA; FUNGUA SAUTI HAPA


Akuzingumza na mtandao huu, mratibu uchaguzi manispaa ya Bukoba amepokea mapingamizi 10 kutoka kata mbalimbali katika ngazi ya udiwani.

Mapingamizi hayo yamewekwa na wagombea udiwani katika vyama mbalimbali vya siasa, ambapo mratibu wa huyo wa uchaguzi Bw Elick Bazombopora, amesema kuwa mgombea wa kata Kahororo Bw Chief Abdronicas Kalumuna amewawekea mapingamizi wagombea  Venant Lugemalila Salapion wa CCM na Bnyenza Saimon wa  ACT, hatahivyo Bw Banyeza amepeleka pingamizi ambalo haliokutaja linampinga nani.

Mratibu huyo amesema kuwa katika kata Miembeni Pingamizi limewekwa na Baganda Gyeshumba Richard wa CHADEMA akimwekea Richard Gasper, ambapo katika kata Kashai,  mgombea wa CCM Bw Samora Agaptus Lyakurwa, amewekea pingamizi ndugu Kabaju Abdukad, ilhali katika kata Kagondo kuna mapingamizi  matano na mapigamizi matatu yakiwekwa na Anatory Aman kwa wagombea watatu.

Amesema kuwa amewawekea Simart Peter Baitan wa CCM, Joram Ifunya wa CHADEMA, na tatu kwa mgombea wa ACT Benson George Bitegeko, ambapo Joram wa CHADEMA amemwekea Baitan wa CCM, ilhali  Benson George Bitegeko akimwekea Anatory Amani.


Katika barua yake yenye kumbukumbu namba BMC/KT/KAG/A.2/49, amabaye ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata Kagondo, amesema kuwa ametengua uteuzi wa Dr Anatory Amani kugombea udiwani, kutokana na pingamizi la Bw Benson George Bitegeko wa ACT kuhusu kudanganya eneo alilozaliwa, ambapo katika barua yake Amani alionesha kuzaliwa wilayani Karagwe, ilhali taarifa za mamlaka zinaonesha amezaliwa katika eneo la Kanoni Ruanda, kwenye wilaya ya Rakai nchini Uganda, hivyo hakutoa taarifa sahihi za kuzaliwa kwake.

Kupitia baraua yenye kumbukumbu KSH/UCH/VEO.1/05, iliyoandikwa na msimamizi kata Kashai, imetengua uteuzi wa ndugu Kabaju Nuruhuda Abdukadir kugombea udiwani kwenye kata hiyo kwasababu ya pingamizi alilowekewwa na mgombea wa CCM ndugu Samora Agapmtus Lyakurwa.
 
Na Mwanaharakati.