MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 31 May 2017

AUDIO; KAULI YA CHADEMA BAADA YA KIFO CHA NDESAMBURO



Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, kimetoa ufafanuzi na namna kifo cha mwenyekiti wa chama hicho mkoani Kilimanjaro kilivyotokea.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe, amesema kuwa ni kifo cha ghafla kwasababu juzi marehemu alitokea mkoani Dodoma na asubuhi ya leo alimwita meya wa jiji la Arusha kwa lengo la kujadili naye suala la waliopata ajali katika shule ya Lucky Vicent, ambapo Philimon Ndesamburo alizidiwa ghafla kabla mazungumzo yao kukamilika...SIKILIZA HAPA 

Na Mwanaharakati.

Monday, 29 May 2017

MPANGO WA SERIKALI JUU WANAOINGIZA MIFUGO KWENYE HIFADHI ZA MISTU




Waziri wa maliasili na utalii Prof.Jumanne Magembe leo amefanya ziara yake ya siku moja mkoani Kagera kwa lengo la kueleza msimamo wa serikali juu ya wanaoingiza mifugo katika hifadhi za mistu na mapori ya akiba.

Akiwa wilayani Biharamulo Prof.Magembe amesema kuwa hawataruhusu tena mifugo kurudi ndani ya hifadhi,na watahakikisha ndani ya wiki mbili au tatu wanapitisha ndege zenye rubani na ambazo hazina rubani ili kuhakikisha hakuna mtu anayeingiza mifugo ndani ya hifadhi hizo.

Aidha amesema kuwa wakikuta mtu ameingia kwenye hifadhi,watamuondoa pamoja na msimamizi wa eneo hilo na familia yake yote  ili mbegu mbaya isibaki katika kuhifadhi wanyamapori.
 


Na Mwanaharakati.

VIDEO NA PICHA; WAOKOZI WAKUTANA NA WAKATI MGUMU KUZAMA KWA WATU MANISPAA YA BUKOBA

Mwili wa kijana Renatus Mecksad lieyekuwa na umri wa miaka 14 na alikuwa mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Bugambakamoi umeopolewa, huku mingine miwili ya Shabin Hamad mwenye umri wa miaka 12 na mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Bugambakamoi, pamoja na aliyeogelea kuwatafuta naye kuzama Olvis Frugence aliyekuwa na umri wa miaka 32, miili yao bado haijatafutwa.

Maofisa wa zimamoto wakizunguka kwenye bwawa lililotokana na uchimbaji wa changarawe
Ni umati wa wananchi wakisubiria kuona hatima ya upatikanaji wa miili au wawili hao wakiwa hai

Mama wa mtoto Renatus Mecksad akiondolewa kwenye eneo la tukio akingulia kilio baada ya kuona mwili wa mwanae

Na Mwanaharakati.

MANGU ALIVYOUDHURIA KIAPO CHA IGP MPYA SIMON SIRRO IKULU



Ni katika ukumbi wa Ikulu ambapo Ernest Mangu ambaye uteuzi wake umetenguliwa, yupo katika orodha ya viongozi wa polisi walioudhuria katika hafla hiyo, tayari kushuudia mteule akiwa kiapo...

Kiapo hicho kinajiri siku moja baada ya rais Joseph Magufuli kumteua jana jumapili kushika nafasi hiyo na kueleza kuwa Ernest Magu atapangiwa nafasi nyingine.

Jana mei 28/2017 Rais Magufuli alifanya mabadiliko kwenye jeshi la polisi nchini kwa kutengua uteuzi wa aliyekua mkuu wa jeshi hilo, Ernest Mangu,  nafasi ambayo alitumikia tangau awamu ya nne chini aliyekuwa rais wakati huo Jakaya Mrisho Kikwete.
IGP Sirro alikuwa kamishna wa polisi na kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam, aliwahi kuwa kamanda wa polisi mkoani Mwanza kama alivyo Ernest Mangu aliyewahi kupitia mkoani humo.



Na Mwanaharakati.

HII NDIYO TAARIFA YA WATATU KUZAMA KWENYE SHIMO LA MAJI BUKOBA

Ni tukio la kusikitisha lililotokea jana baada ya watoto wawili kudumbukia kwenye shimo ambalo lilitumika kutoa changarawe katika mtaa wa Bugambakamoi kata Kitendaguro manispaa ya Bukoba.

Watoto hao ni wanafunzi wa shule ya msingi Kitendaguro na mwili wa mtoto mmoja umeshaopolewa huku kijana mwingine mtu mzima na mtoto wa pili haijaopolewa ilhali polisi, zimamoto na wananchi wanaendelea kutafuta miili hiyo au kuwapata wakiwa salama.

Baada ya harakati za baadhi ya wananchi kuwaopoa hapo jana mapema kugonga mwamba, kijana ambaye hajaonekana alilazimika kuzama kuwatafuta huku wenzake wakimzuia kuingia kwy shimo hilo, anasadikiwa kuwa na umri wa miaka 32 na watoto mmoja ana miaka 14 na wa pili miaka 12, picha za tukio hilo na undani zaidi unaletwa kwenu punde....

Na Mwanaharakati.

KITISHO CHA UZALISHAJI MAZIWA KAGERA, KIMEITIBUA SERIKALI NA KUTOA MAAMUZI



 
Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania -TADB kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo nchi nzima ili kuweza kuwakwamua katika changamoto zinazorudisha nyuma juhudi zao za kujiongezea kipato kwa kukosa mitaji ya uhakika katika kuongeza tija ya kilimo nchini.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa inayofanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera.
Mhe. Ole Nasha amesema kuwa dhima ya kuanzishwa kwa TADB ni kutoa suluhisho la ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha na mikopo kwa wakulima wadogo nchini ili kuchagiza maendeleo ya kilimo nchini hivyo Benki ina wajibu wa kuwafikia wakulima wote wadogo wenye uhitaji wa mikopo.
“Nawaomba mujielekeze kutoka mikopo yenu ya gharama nafuu kwa wakulima wadogo ambao hawawezi kupata mikopo kwenye benki za biashara ili kutekeleza lengo la Serikali la kuwainua wakulima kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” Mhe. Ole Nasha alisema.
Aliongeza kuwa anafahamu kuwa Serikali ikishirikiana na TADB ilifanya mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na kupelekea Bodi ya Benki ya Maendeleo Afrika kutoa kibali cha kuipatia TADB fedha za kukopesha kwenye sekta ya kilimo, na kuitaka Benki hiyo kutumia fedha hizo kwa kuwapatia wakulima wadogo ambao ni wahitaji zaidi wa miko hiyo.
“Naomba muwakopeshe wakulima hizo fedha ya zaidi  Bilioni 200 ili kuwaongezea tija katika shughuli zao,” aliongeza.
Kwa mujibu wa mpango kazi wa TADB hadi kufikia miaka mitano ijayo itakuwa imefungua ofisi sita za kikanda zenye lengo la kuwahudumia wakulima wote nchini. Ambapo katika hatua za awali Benki hiyo inaendelea kuwajengea uwezo wakulima wa nchi nzima ili kuwaandaa kupata mikopo kutoka Benki hiyo.
Mpango kazi huo unaweka bayana malengo mengine yanayojumuisha utafutaji wa fedha toka vyanzo mbalimbali zenye gharama nafuu kwa minajili ya kuwakopesha Wakulima katika hatua zote za mnyororo wa ongezeko la thamani kwenye mazao ya Kilimo na kupanua wigo wa utaoji mikopo toka Minyororo Kumi na Minne (14) ya mwanzo na kuhusisha pia mazao mengine ya Kilimo na pia kuwaunganisha wakulima na masoko ya ndani na nje ya nchi.
TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo  na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
 

Na Mwanaharakati.

Sunday, 28 May 2017

PICHA 5;ILIVYOZINDULIWA WIKI YA MAZIWA KITAIFA


 
Akizindua shughuli hiyo Naibu waziri wa Kilimo,mifugo na uvuvi mh.William Ole Nasha amesema kuwa nchi ya Tanzania ina changamoto kubwa kwa upande wa matumizi ya maziwa ambapo kwa mwaka mtanzania mmoja anatumia wastani wa lita 47 ambayo ni chini ya robo ya kiwango kinachopendekezwa na shirika la afya duniani badala ya lita 200,hali aliyosema inasababisha hata kuendelea kwa kiwango kikubwa cha udamavu kwa Watanzania.

Pia amewasihi wananchi kuhudhuria kwa wingi katika kipindi hiki cha wiki ya maziwa ili waweze kupatiwa elimu ya kutosha juu ya matumizi ya maziwa ikiwa ni pamoja na kutambua magonjwa unayoweza kupata usipokunywa maziwa.



Wiki ya maziwa kitaifa  imezinduliwa leo mkoani kagera katika viwanja vya Kyakairabwa vilivyopo ndani ya manispaa ya Bukoba ambayo itafikia kilele  june 1 mwaka huu,ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya maziwa.








Na Mwanaharakati.

Saturday, 27 May 2017

WANAFUNZI WATAHABIKA MASHINDANONI, RAS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KWA HALMASHAURI KUTOA FEDHA.



MULEBA 
                                                                                                                                          

Mashindano ya michezo kwa  shule za sekondari{UMISETA}yamezinduliwa rasmi katika chuo cha uwalimu katoke mkoani Kagera kwa kushirikisha wilaya zote za mkoa wa Kagera zikiwa na jumla ya wanamichezo 469.

Akiongea mbele ya mgeni rasmi,Afisa elimu mkoa Kagera Aloyce Kamamba amesema kuwa wanaoshiriki michezo ni jumla ya wanamichezo 469,walimu na maafisa elimu 40,wanafunzi ni wasichana 192 na wavulana 277 huku akisema kuwa hatua ya kwanza itakamilika may 29 mwaka huu na kupata timu moja ya mkoa itakayokuwa na wanamichezo 91 na walimu 15.

Aidha amesema kuwa may 30 mwaka huu timu hiyo itaanza kambi mpaka june 4 ambapo june 5 itareport chuo cha uwalimu Butimba jijini mwanza kwa ajili ya kushiriki mashindano kitaifa ambayo yanatarajia kukamilika june 17 mwaka huu.

Pia Kamamba amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni pamoja na baadhi ya halmashauri ukitoa ya Bukoba,Karagwe na Kerwa zimeshindwa kukamilisha michango yao kifedha kwa ajili ya kuendesha mashindano hayo hali inayosababisha baadhi ya vitu kukwama.

Akizindua mashindano hayo,Katibu tawala mkoa wa Kagera Kamishina wa polisi Diwan Athuman ametoa siku tatu kwa wakurugenzi wa  halmashauri zote ambazo hazijakamilisha michango hiyo kuhakikisha wanazitoa ndani ya muda huo na apate mrejesho wao.

Sanjali na hayo amewasihi wanamichezo kufanya vizuri katika mashindano yao ili kuhakikisha mkoa wa kagera unafanya vizuri hatua ya kitaifa itakayoanza june 5 mwaka huu.



Na Mwanaharakati.