MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Friday, 26 July 2013

RAIS KIKWETE AZINDUA BARABARA YA KAGOMA RUSAUNGA MKOANI KAGERA

 Pamoja na uzinduzi huo, mh rais amesema kuwa serikali ina mpango wa kuanza msako mkali kwa majambazi yanayoteka magari na uvamizi mbalimbali, kuwa wanaomiliki silaha wazisalimishe ndani ya wiki mbili baada ya hapo majeshi yote nchini yanaanza msako na wanawahusika hawatakamatwa mateka.
 Juu ndiyo barabara iliyofunguliwa,

 Rais pia amepanda mti katika eneo la uzinduzi huliofanyika kwenye njia panda wilayani biharamulo.

 Mawaziri walioongoza na rais pia wameshiriki kupanda mti
 Kamanda wa polisi mkoanNI Kagera PHILIP KALANGI, akifuatilia ulinzi na usalama wakati wa uzinduzi na hotuba ya rais wilayani Biharamulo, na chini ni waziri wa ujenzi Dk Pombe magufuli akipinga ngoma ya Nyamigogo.
MWANA HARAKATI

Thursday, 25 July 2013

RAIS KIKWETE AMEWAAHIDI WANANCHI WILAYANI MULEBA KUPIMA ARDHI NA KUONDOA MGOGORO KWA WANAOPAKANA NA KAMBI YA KABOYA.

 Mheshimiwa Mwijage, amesema kuwa mgogoro wa wananchi na kambi ya Kaboya, aueleweki kutokana na kutokuwapo mipaka ya kambi hiyo, kitendo kinachosababisha wananchi washindwe kutumia ardhi kutokana na masuala ya ulinzi na usalama, ilhali jeshi nalo linatakiwa kuheshimia.
 Katika hatua nyingine, mbunge huyo amesema kuwa wananchi wakabiliwa na ukosefu wa huduma ya umeme, ambapo walishapewa ahadi ya kupatiwa huduma hiyo kupitia REA, lakini hadi sasa hakuna kilichoishatekelezwa na kusababisha lawama kwa viongozi wa jimbo hilo.


 Rais Kikwete amesisitiza kuwa ulinzi na usalama umeimarika katika mkoa na nchi ya tanzania, kutokana na kauli ya mkuu wa majeshi Jenerali DAVIS MWAMUNYANGE, kuwahahikishia wananchi kuwa jeshi liko imara na linazingatia ulinzi kwa wananchi wake.
 Wananchi wakifuatilia hotuba fupi ya rais wa jamhuri ya muungano Tanzania baada ya kuweka dhana za asili kwenye mwenge wa kudumu ktk makaburi ya mashujaa.

Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi HAMIS KAGASHEKI, akisalimiana na viongozi wengine wa kitaifa katika maadhimisho ya siku ya mashujaa kambini Kaboya.

Rais Kikwete ameendelea na ziara yake mkoani Kagera, ambapo sasa yupo wilayani Muleba ambapo atahutubia wananchi baada ya kuzindua mradi wa maji katika eneo la IYAKO, na bada ya hapo anapumzika na kuelekea Biharamulo.
MWANA HARAKATI

Wednesday, 24 July 2013

RAIS KIKWETE AMEWEKA JIWE LA MSINGI KWEYE UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA.

 Ris akivishwa bendera ya skauti
 Hii ni sehemu ya uwanja wa ndege wa Bukoba.
 Rais Kikwete akihutubia wananchi uwanjani hapo
 Mheshimiwa Kikwete akipewa taarifa na kusomewa ramani na mtaalamu wa ujenzi wa uwanja wa ndege
 Rais Kikwete akielekea kufungua pazia ya jiwe la msingi baada ya kukata utepe.
 Mheshimiwa Rais akisalimiana na baba Askofu Kilaini alipowasili uwanjani hapo
 Waziri wa maliasili na utalii Balozi Kagasheki, akibadilishana mawazo na waziri wa uchukuzi Arison Mwakeyembe na chini rais akihutubia wananchi baada ya kuzindua jengo la cha acha ushirika Kagera KCU.
 Chini ni picha ya pamoja na viongozi wa ushirika nyuma jengo hilo lililozinduliwa linaonekana kwa mbali.
MWANA HARAKATI

Tuesday, 23 July 2013

UGANDA IMEWEKA UTARATIBU WA MACHINGA KUVAA SARE

 Ni kwa wafanyabiashara ndogondogo wanaouza vitu vidogovidogo kwa abiria kwenye stendi mbalimbali za magari.

 Hapa ni katikati ya jiji la KAMPALA, lilipomulikwa na kamera ya kandayaziwaleo ilipotembelea maeneo hayo.
 Wakati waganda wanaoonekana wakiuza ndizi, mishikaki na soda wakiwa na sare zao kwa mujibu wa utaratibu, Tanzania wao wanauza maziwa, karanga nk bila hata kuwa katika hali ya kuvutia wateja.



MWANA HARAKATI

MAANDALIZI YA SIKU YA MASHUJAA YAMEKAMILIKA VIWANJA VYA MASHUJAA KAMBINI KABOYA MKOANI KAGERA.

 Ni kikosi cha askari wa JWTZ kikitoka uwanjani baada ya kuigiza mapokezi na salamu ya rais ili kujiweka sawa.

 Makaburi ya walipolala makamanda waliopigania nchi na hapa chini ni upande wa makamanda wa Kikristo kama kibao kinavyoeleza.

 Ukaguzi wa rais ukiigizwa na viongozi waliokuwa katika viwanja hivyo kama wanavyotembezwa na uongozi kwa kutoa ufafanuzi kwa kiongozi.

 Baadhi ya magari yaliyofanya kazi wakati huo na sasa yamesalia kama magofu ila ni kionesho tosha.
 China unaona masalia ya magari, vifaru na bomu vilivyotumika enzi hizo.

 Ni viongozi mbalimbali wa kijeshi na dini akionekana kamanda wa polisi mkoa PHILP KALANGI.
MWANA HARAKATI

Monday, 22 July 2013

JE RAIS KIKWETE ATAJIBU AU KUTEGUA KITENDAWILI CHA VIFO VISIVYOJULIKANA WILAYANI MULEBA?

 Mahojiano yangu mbalimbali usiku na mchana kujua hali hiyo ikoje, yamenifanya kugundua kuwa katika kata ya muhutwe wananchi wameshaamua kujifungia mapema kabla ya saa moja jioni wakihofia kutekwa.
 Kuhusu walichozungumza wananchi, wenyeviti wa kata na vijiji, kamanda wa polisi na mkuu wa wilaya ikibidi na mkuu wa mkoa wa Kagera, fuatailia vipindi vya redio Kasibante 88.5 MHz kupitia mboni ya jicho kila ijumaa 21:30 ni muda wa usiku na marudio jumapili saa 1 kamili jioni.
Pichani ni baadhi ya wananchi wakiwamo wenyeviti wa vijiji mbalimbali kwenye kata ua Muhutwe wilayani Muleba wakizungumza nami.
MWANA HARAKATI

SHULE YA SEMINARI YA KIISLAMU QDUS MJINI BUKOBA, YAFANYA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA BWENI NA MIUNDOMBINU MINGINE.

 Mbuh. Kagasheki amechangia sh milioni 5 na zingine 5 amewapa siku mbili lakini zilizosalia ili kukamilisha mil 23 za bweni, ambapo harambe imechangisha trip za mawe na sementi kutoka kwa wadau mbalimbali kutokana Kasibnte fm kurusha harambee hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na waziri live. 
 Mgeni rasmi akisaini kitabu cha maudhurio.
 Mezani ni mil 5 alizotoa mbunge, huku akiendelea kuwata wadau mbalimbali walichangia kwa ahadi na cash.
 Haya ni baadhi ya majengo ya shule hiyo yenye wanafunzi 307 na walimu 26 ambao ni awali hadi drs la saba.

 Ni baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakisikiliza kwa makini mazungumzo ya waziri Kagasheki.
MWANA HARAKATI

Friday, 19 July 2013

SHIRIKA LINALOJISHUGHULISHA NA ELIMU YA UPATIKANAJI WA MAJI SALAMA SNV, LIMEPOKEA RIPOT YA WAANDISHI HABARI KUTOKA REDIO ZA KANDA YA ZIWA KUHUSU MRADI WA ELIMU YA MAJI KWA MWAKA MMOJA.

 Picha juu wa kwanza kushoto ni Mwanafunzi kutoka SAUT yupo SNV kwa field ya miezi3, wapili nyuma ni CONSOLATA TEM, cordinator SNV, wa tatu ni mwanahabari Mac Ngaiza kutoka Kasibante fm redio Bukoba, wa nne ni AYETA ambaye ni cordinator pia katika miradi ya SNV na amejikita katika ushauri kihabari, na mwisho ni mwanahabari kutoka redio FARAJA Shinyanga.
 Aliyesimama ni Projestus Binamungu wa Kasibante fm, akiwasilisha mada kwenye kikao cha wanahabari na SNV.
Mwanaharakati Nicolaus Mac Ngaiza ambaye pia ni mmiliki wa Blog hii, akiwa kwenye kivuko kimoja Busisi kwenye safari kuelekea Mwanza.
MWANA HARAKATI

WANAJAMII KUPITIA BLOG YENU HII, NIMEREJEA BAADA YA MICHAKATO MIREFU ILIYONIBANA KUWAPA HABARI, MSILAUHUMU BALI MNIOMBEE NIENDELEE NA KAZI YANGU HII YA KUHABARISHA.

Ni baada ya kutoonekana katika safu hii muhimu, katika kuweka habari, siyo kwamba nilifungwa, nilizuiliwa au niliacha kazi ya habari, bali nilikuwa na majukumu mengine muhimu ya kuongeza uelewa kichwani na kushidnwa kupata nafasi, leo nimerejea kwa nguvu mpya karibuni wadau.

MWANA HARAKATI

Saturday, 15 June 2013

WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO WAKATI AKIZINDUA RASMI MTANDAO WA MAWASILIANO YA SIMU WA KUSAIDIA WATOTO HAPA NCHINI (TZ CHILD HELPLINE) TAREHE 14 JUNI, 2013


HOTUBA YA MHE. SOPHIA M. SIMBA (MB),

Kwanza, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru mwenyezi mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha sote kukutana hapa ili kuweza kushuhudia tukio hili muhimu katika kuwezesha watoto kupata mojawapo ya haki yao ya msingi.

Ndugu Wageni Waalikwa
Mnamo mwaka 2009 Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya watoto hapa nchini ilifanya utafiti wa kina ili kufahamu ukubwa na sura ya ukatili wa kijinsia, kimwili na kiakili yanayowasibu wasichana na wavulana hapa nchini.  Utafiti huu ulifanywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Afya ya Sayansi na Tiba cha Muhimbili (Muhimbili University of Health and Allied Sciences – MUHAS) kwa kushirikiana na UNICEF na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Center for Diseases Control – CDC). Ripoti ya Utafiti huu ilizinduliwa rasmi mnamo tarehe 09 Agosti, 2011 na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa bibi Asha-Rose Migiro.

Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa kuna kiwango kikubwa cha ukatili dhidi ya watoto na matukio mengi ya ukatili kwa watoto yamekuwa yakifanyika ama shuleni na au nyumbani.  Hali hii ilipelekea wadau wa masuala ya watoto (Taasisi za serikali na zile zisizokuwa za serikali) kuandaa Mpango Mkakati wa mwaka mmoja wa Kushughulikia Tatizo la Ukatili Dhidi ya Watoto (2012 – 2013) na hatimaye kuandaa Mpango wa miaka mitatu wa kushughulikia tatizo hilo (2013 – 2016) ambao ulizinduliwa mwezi April mwaka huu.

Ndugu Wageni Waalikwa
Mnamo tarehe 3 Januari, 2013 Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto iliingia makubaliano na Asasi Isiyokuwa ya Kiserikali ya C-Sema kuhusu uendeshaji wa mtandao huu katika maeneo ya majaribio (Pilot Areas). Uendeshaji wa mtandao huu katika maeneo haya utasaidia kutoa picha halisi ya namna nzuri ya uendeshaji wa mtandao wa namna hii hapa nchini.  Mtandao huu utafanya kazi katika Wilaya/ Manispaa za Temeke, Magu, Bukoba Vijijini, Musoma Mjini, Kasulu na Hai ambapo muda si mrefu utaanza kufanya kazi katika Manispaa za Ilala na Kinondoni. Lengo kuu la Serikali kwa kushirikiana na wadau wake wa maendeleo ya watoto ni kuhakikisha kuwa mtandao huu unafanya kazi katika maeneo yote ya Tanzania Bara.

Ndugu Wageni Waalikwa
Uanzishaji wa Mtandao wa Mawasiliano wa Kusaidia Watoto ni moja wapo ya shughuli ambazo zilipangwa kutekelezwa na Wizara yangu katika Mpango wa Miaka Mitatu wa  Kushughulikia Ukatili Dhidi ya Watoto uliozinduliwa hivi karibuni. Kadhalika, ni moja wapo ya utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa  Haki za Watoto (The UN Convention on the Rights of the Child – UN CRC) ambao nchi yetu iliusaini na kuuridhia mara baada ya kupitishwa kwake. Mtandao huu utatoa fursa kwa watoto na au watu wazima kwa niaba ya watoto kutoa taarifa za ukatili unaofanywa kwa watoto katika eneo fulani ili kuwezesha wahusika kufuatilia kwa karibu na urahisi kwa ajili ya kutoa msaada kwa mtoto/watoto waliofanyiwa vitendo vya ukatili na kumchukulia/kuwachukulia hatua mhusika/wahusika wa vitendo hivyo vya ukatili. Kwa kiasi kikubwa kama mtandao utatumiwa kwa malengo haya, ni imani yangu kuwa itasaidia kupunguza ukatili dhidi ya watoto na vile vile kuhakikisha kuwa watoto wanapata msaada stahiki kwa wakati.

Ndugu Wageni Waalikwa
Ni matumaini ya Wizara yangu kuwa wadau mbalimbali watajitokeza kushirikiana nasi katika kuhakikisha kuwa huduma hii inapatikana katika maeneo yote hapa nchini katika muda muafaka ili kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata ulinzi wa kutosha. Kadhalika, ni matumaini yangu kuwa jamii na wahusika wote watawezeshwa kupata uelewa wa kutosha kuhusu matumizi sahihi ya mtandao huu.

Mwisho, napenda pia kuchukua fursa hii rasmi kutamka kuwa nimezindua rasmi mtandao wa mawasiliano ya simu wa kusaidia watoto katika maeneo ya majaribio niliyoyataja hapo mwanzo.

Tuungane kwa Pamoja Kuijenga Tanzania Imfaayo Mtoto.
MWANA HARAKATI