MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 30 November 2015

SERIKALI YAKEMEA JUU YA KAULI ZA RAIS,UTARATIBU WA USAFI SIKU YA UHURU KUTOLEWA

Mkurugenzi wa habari maelezo Bw Assah Mwambene, amesema kuwa kauli inayotolewa na badhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii hazifai na rais hakukosea alipoagiza ununuzi wa vitanda Muhimbili.
Wakati huo huo, amesema kuwa utaratibu wa usafi siku ya uhuru tarehe tisa desemba, utafanyika chini ya utaratibu wa serikali za mitaa, ingawa unaandaliwa rasmi kwa wananchi na wafanyakazi.





Na Mwanaharakati.

Wednesday, 25 November 2015

MPYA:SERIKALI YAZUIA MATUMIZI YA FEDHA KUANDAA VIKAO NCHINI


Serikali kupitia ofisi ya rais utumishi wa umma, imesitisha utaratibu wa kuandaa mikutano ya serikali kwaajili ya kubana matumizi, na badala yake imeanzisha utaratibu wa kufanya mikutano kwa njia ya TEHAMA
Na Mwanaharakati.

Friday, 20 November 2015

HII KALI; TAMISEMI YAONDOA WAKUSANYA KODI MAOFISINI



Ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, imeanza utarartibu wa ukusanyaji
kodi kupitia mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji mapato ya mamlaka za serikali za mitaa, kuondoa mianya ya rushwa na wakwepa kodi ilhali Tanzania ikikabiliwa na ujenzi holela katika halmashauri mbalimbali nchini.

Na Mwanaharakati.

MAGUFULI ATAJA MAZITO BUNGENI, UKAWA WAONDOKA

Akihutubia bunge la 11 katika serikali ya awamu ya tano, rais wa tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli, ametaja mambo makuu na mazito hasa yale aliyokutana nayo katika kipindi kifupi, ambayo anataka yafanyiwe kazi katika kuyapatia majibu ya haraka.
 Ametaja ;- Rushwa; kuwa lazima iondolewe kwa namna yoyote ndipo atakubali na kukubalika,
                  Bandari; kwa kusema kuwa wizi na ubadhilifu uliokuwapo lazima uondoke,
                  Miundombinu; amegusia kuwa ni lazima wananchi wapate maji,barabara na umeme wa uhakika,
                  TRA; Hapo akasisitiza kupatikana kwa kodi halali na kuondoa wakwepaji,
                  Tanesco; amesema atakomesha tabia ya kukatika hovyo na mgawo usio wa lazima,
                  Ujangili; Hili linahusu kuzuia uvushaji malisili kwa wizi na kuweka mipaka na makaazi ya watu,
                  Uduma za afya; vituo vya tiba, dawa, na vifaa vya tiba.
                  Uhamiaji; Kudhibiti ajira kwa wageni na utoaji hovyo wa vibali vya ukaazi,
                  Polisi; Kuondoa kubambika kesi, madai ya askari na makaazi,
                  Kilimo;  Hapa lazima yaende sambamba na uvuvi, viwanda na mazao,
                  Reli; inakwenda sambamba na uboreshaji wa bandari kavu,hakuna kusafirisha mizigo bure,
                  Makundi maalumu; Kuwezesha wazee, watoto, wasanii, wafanyakazi na walemavu. 
Na Mwanaharakati.

Thursday, 19 November 2015

HUYU NDIYE NAIBU SPIKA TANZANIA-TULIA ACKSON



Na Mwanaharakati.

CV YA KASSIM MAJALIWA IKOHAPA

Vijalizo vya JinaMhe.
Jina la Ukoo:Majaliwa
Jina la Kwanza:Kassim
Jina la Kati:Majaliwa
Tarehe ya Kuzaliwa:1960-12-22
Mahali Alipozaliwa:
Hali ya Ndoa:Nimeoa
Kundi:Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
Jinsia:M
Simu ya Ofisi:-
Simu ya mkononi:785205910
Barua pepe:majaliwa.kasimu@yahoo.com
Anuani:P.O.Box 51,
Ruangwa

Elimu
TokaHadiJina la Shule/ChuoCheti

19701976Mnacho Primary Schoolcheti cha Elimu ya Msingi
19771980Kigonsera Secondary SchoolCSEE
19911993Mtwara Teachers College-
19941998University of Dar es SalaamBachelor Degree
19991999Storckolm UniversityPGDP

Mafunzo Mengineyo
-

Uzoefu
TokaHadiJina la MwajiriNgazi/Wazifa

20102014-MB
20062010PMMkuu wa Wilaya
20012006PS-CWJKatibu Mkoa
20012001PS-CWJKatibu Wilaya
19882000PS-MoecMkufunzi
19841986TD-Lindi CouncilMwalimu

Na Mwanaharakati.

KAULI YA WAZIRI MKUU BAADA YA KUPIGIWA KURA

Anatarajiwa kuhapishwa kesho saa4 katika ofisi ndogo za ikulu CHAMWINO mjini Dodoma, ambapo mchakato umekamilika kuhusu kuidhinishwa kwake baada ya wabunge kumpitisha kwa asilimia 73.5% ya kura za wabunge wote walioshiriki.
Na Mwanaharakati.

HUYU NDIYE WAZIRI MKUU MTEULE

Baasha iliyowasilishwa bungeni imeonesha jina la Kassim Majaliwa kuwa ndiye waziri mkuu mteule.
Na Mwanaharakati.

Wednesday, 18 November 2015

WIZARA YAPIGA MARUFUKU KULIPIA UMEME; SOMA UNDANI



. Imewataka wananchi kutokubali kuchangia fedha ili kuunganishiwa huduma ya umeme.


Msemaji wa wizara ya nishati na madini  Badra Masoud, amesema kuwa serikali haijaweka mpango wa kuchangisha watu hela kwa ajili ya huduma, afisa wa wizara wala kulipa fundi wa Tanesco, akiongeza kuwa fedha elekezi inaweza kuhitajika katika maeneo ambayo hayako kwenye mpango wa wizara kufikisha umeme kwa wakati huo.
Amesema kuwa nchi inakua kwa kasi na serikali imejipanga kufikisha umeme kila eneo kulingana fedha zinavyopatikana kwa kusisitiza kuwa kuna lawama kuhusu mgawo wa umeme, ambao amefafanua kuwa saizi haukuna mgawo ingawaje ubovu wa miundombinu ndiyo husababisha kukosekana kwa umeme kwa wakati Fulani.
Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi duniani na uharibifu wa vyanzo vya maji,  Tanzania inakosa mvua za kutosha  na kusababisha gharama za umeme kupanda baada ya mabwawa ya Mtera kukauka ambayo huzalisha umeme wa wa bei nafuu kuliko umeme wa aina yoyote mpaka sasa.

Tanzania ina megawati 1500 za umeme ambazo hutumika kati ya megawati 800 na 900 nchi nzima kutoka vyanzo vya  Ubungo one, Tegeta, Nyakato Mwanza megawati 60, Ubungo two ya gesi na kampuni ya Symbion pamoja na IPTL na AGRECO zinazotumia mafuta, ingawa serikali inaendelea kuongeza kiasi cha umeme huo kwa kuwekeza katika gesi na makaa ya mawe.
 
Na Mwanaharakati.

Monday, 16 November 2015

JOB NDUGAI APITISHWA NA CCM- SOMA UNDANI

Chama cha mapinduz ccm kimempitisha Job Ndugai kugombea nafasi ya spika kwa kupigiwa kura hiyo kesho.

Wagombea watatu walioteuliwa pamoja naye hiyo jana wameamua kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho, taarifa inaendelea...
Na Mwanaharakati.

Friday, 13 November 2015

ANNA MAKINDA ATANGAZA KUTOGOMBEA USPIKA-UJUMBE MZITO UKOHAPA

In baada ya uvumi wa muda mrefu kuhusu spika anayemaliza muda wake kuwa anagombea nafasi hiyo akiwa nje ya ubunge, amezungumza na waandishi habari kuwa hatagombea na kutaja sababu kuu mbili.

1. Nimekaa sana uongizini kwa miaka40 sasa.
2. Ni vema kumuacha rais wetu mpya akatengeneza safu mpya nasie tukiwa kama washauri.

Mh. Makinda amesisitiza kuwa ili serikali ifanye kazi yake vizuri, ni vema jamii ikaacha maneno ya ushabiki wa kisiasa.

Picha na habari zaidi vinafuata.

Na Mwanaharakati.

Monday, 9 November 2015

RAIS MAGUFULI AVUNJA BODI YA MUHIMBILI. UONGOZI KUSIMAMISHWA

Maamuzi mengine ya rais huyo nikumsimamisha na kumuamishia wizarani kaimu mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo.

Rais Magufuli ametoa uamuzi huo muda mfupi baada ya kutembelea hospitalini hapo na kukuta baadhi ya vifaa havifanyi kazi, ilhali baadhi ya kina mama wagonjwa wakiwa wamelala chini.

Maamuzi hayo yameanza maramoja baada ya taarifa hiyo kutolewa na balozi Ombeni Sefue katibu mkuu kiongozi.
Na Mwanaharakati.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA RAMANI YA ZAMANI


.Haioneshi marekebisho ya mikoa mipya,
.Wachapishaji wauzaji kukamatwa,
.Yasema hakuna mgogoro na Malawi.


katika baadhi ya maeneo.
Mkurugenzi wa habari maelezo ambaye ni msemaji wa serikali ASSAH MWAMBENE, amesema kuwa serikali ilizindua ramani mpya na sahihi, ambayo inaonesha uwepo wa mikoa mipya ya SIMIYU, GEITA na MANYARA, pamoja na kuonesha mipaka ya eneo la ziwa Nyasa na Tanganyika.
Amesema kuwa siku za karibuni baadhi ya vyombo vya habari yakiwamo magazeti ya Mzalendo, Citizen, Mwananchi na Wajibika yalitumia ramani isiyosahihi katika taarifa zake, na serikali inaweza kuvichukulia hatua kwa mujibu wa sheria wakati wowote.
Wakati huo huo, amezungumzia mgogoro wa ziwa Nyasa  kati ya Tanzania na Malawi, kuwa ukubwa wa Tanzania ni pamoja na eneo la ziwa Nyasa, kwani  Malawi ina eneo lake katika ziwa hilo na hakuna mkanganyiko tena kwani Tanzania inahudumia eneo lake na Malawi la kwake kwasababu nchi zilikwisha kaa pamoja na kutoa maelezo na shughuli zinaendelea kawaida.
Itakumbukwa kuwa ramani ya Tanzania, afrika na dunia imekuwa ikiuzwa kiholela na wafanyabaisha mbalimbali nchini, jambo ambalo serikali imewataka kufuata taratibu za upatikanaji wa ramani iliyo sahihi kwenye mamlaka husika, kama wanataka kuendelea na biashara hiyo.

Na Mwanaharakati.