KUTEULIWA KUWA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja
Jenerali Samwel Albert Ndomba kuwa
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia tarehe 14 March 2012.
Meja Jenerali Samwel Albert Ndomba alizaliwa tarehe 22 Apr
1954 wilaya ya Mbinga, mkoa wa Ruvuma. Meja
Jenerali Ndomba aliandikishwa Jeshi mwaka 1976 na kutunukiwa kamisheni 1977.
Katika Utumishi wake amewahi kushika madarakayafuatayo,
Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Jeshi, Mkuu wa Wilaya Ngara, Mkuu wa Mkoa Arusha
na Mkuu wa Utumishi wa Jeshi.
Meja Jenerali Ndomba anashika nafasi iliyoachwa wazi na
Meja Jenerali Samweli Kitundu ambae amestaafu kwa mujibu wa sheria.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 92023, Simu:
0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk