MWANA HARAKATI
Nicolaus Mac (None Association Movement) KWA MATANGAZO YA REDIO NA TV WASILIANA NASI KWA +255767814844- nicolausngaiza@gmail.com.
Thursday 27 December 2012
ASKOFU KKKT AWAASA WATANZANIA KUTUNZA TAIFA LAO
Akizungumza katika ibaada ya X-mass, Askofu wa kanisa la KKKT dayosisi ya kaskazini magaharibi ELISA BUBERWA, amesema kuwa ni wakati wa wakristo kutambua umuhimu wa taifa lao ambalo limejaa neema, hivyo kulitunza kwa kutotenda maovu ambayo yanaonesha dalili ya kusababisha machafuko. Katika hatua nyingine, Askofu huyo amewataka waumini wote kutopenda kuhama hama madheebu, na hata hivyo kuacha kubatizwa mara kwa mara , kwani kitendo hicho ni hakimpendezi mwenyezi mungu kwani mtu uzaliwa mara moja.
MWANA HARAKATI
MWANA HARAKATI
KOMBE LA MBUNGE LIKO PALEPALE.
Amekiona kitendo hicho kama jambo la biashara na kushindwa kunufaisha wana Jimbo, hivyo amesema amesubiri wampe taarifa za kujipanga kwao ili 2013 kombe liendelee.
Hata hivyo waziri Kagasheki, amesema kuwa katika kipindi cha miezi7 ya uwaziri, alikuwa bado anapunguza changamoto alizokutana nazo pindi ameingia wizarani hapo, hivyo michakato inaendelea kuhakikisha hifadhi za mkoa wa Kagera zinakuwa za taifa ili kusaidia upatikanaji wa ajira kwa wakazi wa mkoa huo.
Friday 21 December 2012
PROFESA TIBAIJUKA AMEITAKA OFISI YA USHURU WA FORODHAS MPAKANI MTUKULA KUHAKIKISHA MAGARI YANAYOEGESHWA MAPAKANI HAPO HAYAKAI KWA MUDA MREFU
Waziri wa ardhi nyumba na makazi Profesa Anna Tibaijuka, ameitaka ofisi ya ushuru
wa forodha mkoa wa Kagera, kuhakikisha inaweka mipango mizuri katika kituo cha
mtukula ili kupunguza usumbufu wa watumiaji
wa mpaka huo.
Akizungumza na ofisa fordha wa kituo cha mtukula bwana PANGANI, Profesa
Tibaijuka amesema kuwa pamoja na kuondoa
usumbufu, mkoa utajipatia faida baada ya kufanya shughuli zake kwa haraka.
Ametoa kauli hiyo baada ya kuona mpaka wa mtukula
umejaa magari makubwa ambayo yantoka
nchini Uganda, na kusababisha foleni kubwa ambayo hata hivyo inaingiza kiasi
kidgogo cha fedha kwani magari hayo yanatozwa shilingi 3000/= tu kwa siku.
Ameongeza kuwa kiasi cha ushuru kikiwa kikubwa
usumbufu utapungua.
Kwa upande wake afisa forodha wa kituo cha mtukula
bwana PRIMUS PANGANI, amesema kuwa magari hayo yanalipiwa shilingi elfu 3, na
kuwa taratibu zote zinakuwa zimekamilishwa kwa upande wa Tanzania, isipokuwa
waganda wanakuwa hawajakamilisha ndiyo maana yanaendelea kuwepo.
MWANA HARAKATI
Thursday 20 December 2012
Wednesday 19 December 2012
ZIMAMOTO YASHINDWA KUFIKA KWENYE TUKIO LA MOTO
Hii ni kutokana na miundombinu mibovu baada ya wananchi kujenga kwenye mlima mjini Bukoba, ambako hakufikiki na chombo chochote cha usafiri jambo ambalo limewafanya kikosi cha zimamoto kushindwa kufika kwenye nyumba moja iliyokuwa ikiwaka moto.
Ni katika eneo la Kashura, na baada ya kuzungumza na askari wa zimamoto waliokuwa kwenye msafara, wamesema kuwa hii hali wanakumbana nayo mara kwa mara katika makaazi tofauti ya mji wa Bukoba, kutokana na ujenzi holela ambao hauzingatii sheria na taratibu za nchi.Picha chini ni njia itumiwayo na wakaazi wa eneo hilo ambapo katika tukio hilo tanesco walifanikiwa kufika na kuzima umeme pamoja na baadhi ya maeneo ambayo tayari yalikuwa yameshika moto, na hakuna aliyejuruhiwa wala kupoteza maisha.
MWANA HARAKATI
BIBI ANAYEISHI KWA TAABU AOMBA MSAADA
Ni baada ya kujikuta kile anachokusanya kwa kuomba kinaondoka bila hata kukitumia, na hii inatikana na kuishi kwenye kibanda au kipande cha nyumba iliyoanguka na kusaza sehemu ya paa huku maeneo mengine yakiwa wazi.
Anasema ulazimika kutembea na mizigo yake akihofia atakapoiacha anakuta imeibiwa na baadhi ya vibaka ambao hata i=hivyo umvizia nyakati za usiku. Je tunamsaidiaje wandugu? YUPO BUKOBA MJINI.MWANA HARAKATI
MWALIMU ALIYETUHUMIWA KWA UCHAWI BUKOBA ASEMA NI MASUALA YA KIFAMILIA
Ni baada ya kupeleka malalamiko katika chama cha waandishi wa habari mkoa, huku akilaumu vyombo vya habari vilivyoandika na kutangaza taarifa zake lakini akiomba msaada wa jinsi gani vyombo hivyo vitumike kutangaza maelezo yake anayodai kuwa ndiyo sahihi.
Mwalimu huyo anafundisha katika shule ya Kashai mjini Bukoba, ambapo anasema yeye hakuwahi kutunza msukule ila siku polisi wanakuja nyumbani kwake kuliwapo na mtoto wa nduguyake aliyemtaja kama GLORY, lakini akasema kuwa alipotea mwaka 2007 na baada ya kupatikana alikutwa aongei hivyo.
Monday 17 December 2012
BAADHI YA WANANCHI WAJIFANYA OMBA OMBA KWA MBUNGE
Ni wananchi wa Bukoba vijijini ambapo mbunge wa jimbo la Bukoba vijijini JASON RWEIKIZA alitembelea wananchi wake, lakini wakati akiwa ndani ya gari lake baadhi ya wananchi walienda kumwomba msaada binafsi, jambo ambalo limeonekana kama ni maozea, Je tutafika?
MWANA HARAKATI
MWANA HARAKATI
COFFI OLOMIDE ALIVYOWASHA MOTO
Ni katika jukwa mwana rumba akichapa kazi, juu akiwa na danser na chini akionesha vitu vyake.
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia show ya kundi zima la Koffi Olomide.
MWANA HARAKATI
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia show ya kundi zima la Koffi Olomide.
MWANA HARAKATI
LOWASA KATIKA HARAMBEE YA KUCHANGIA KANISA
Amesema kuwa tunashuhudia maandamano
katika mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha pamoja na ajira.hali
hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini kwetu.
huko nyuma niliwahi kusema kuwa
makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie juhudi za serikali kutatua suala
hilo''alisema Lowassa.
Lowassa ambaye katika harambee hiyo
aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye na familia yake pamoja na marafiki
zake wamechangia kiasi cha shilingi millioni 33.2.
Zaidi ya shilingi millioni 160
zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana katika harambee hiyo.
Kwa upande wake askofu Akyoo wa
jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa uchapakazi wake popote alipokuwa.''Wakati
ulipokuwa Waziri Mkuu ukimsaidia rais tulishuhudia uwezo wako mkubwa katika
kufuatilia majukumu yako''alisema na kuongeza kuwa Lowassa ni mtu wa ibada
Friday 14 December 2012
HAPPY BIRTHDAY MY KID; MTOTO WA NYOKA NI NYOKA
Mwanangu mpedwa Bertha Bahati Nicolaus, ametimiza miaka miwili leo tarehe 14/12/2012 tangu alipozaliwa rasmi saa tano asubuhi 14/12/2010.
Kutokana na usemi wa mtoto wa nyoka ni nyoka mwanangu anafuata nyayo za baba, kama mtangazaji, tunamlea kwa misingi ya kitangazaji kwasababu Baba mtangazaji mama mtangazaji na mtoto analelewa kitangazaji.Mama Bertha akiwa na Bertha sambamba katika maskani yetu Bukoba mjini usiku wa kuamkia 14/12/2012.
Wednesday 12 December 2012
SIKILIZA MKUU WA WILAYA BUKOBA ZIPORA PANGANI NA DIWANI KATA KASHAI WAKIWASIHI WANANCHI WATAWANAYIKE
Baada ya polisi kulazimisha mama huyo alionesha chumba hicho na watoto wakachukuliwa.
Kamanda wa polisi msaidizi Richard Ngole, amewasihi naye amewasihi wananchi kuwa na subira huku akisema kuwa maelezo yaawali yanasema watoto wanaosadikiwa kuwa mzukule mmoja alizaliwa akiwa na upungufu wa akili, isipokuwa hadi hali hiyo inafikia hatua hiyo, ni baada ya shangazi wa watoto hao na baba mdogo kutoka muleba wakija kuwachukuwa watoto hao ambao hata ivyo ilisemekana walipotea lakini mtuhumiwa alikuwa akiwakatalia huku akiwa amewafungia katika chumba kimoja nyumbani kwake.
MWANA HARAKATI
Kamanda wa polisi msaidizi Richard Ngole, amewasihi naye amewasihi wananchi kuwa na subira huku akisema kuwa maelezo yaawali yanasema watoto wanaosadikiwa kuwa mzukule mmoja alizaliwa akiwa na upungufu wa akili, isipokuwa hadi hali hiyo inafikia hatua hiyo, ni baada ya shangazi wa watoto hao na baba mdogo kutoka muleba wakija kuwachukuwa watoto hao ambao hata ivyo ilisemekana walipotea lakini mtuhumiwa alikuwa akiwakatalia huku akiwa amewafungia katika chumba kimoja nyumbani kwake.
MWANA HARAKATI
TETESI ZA USHIRIKINA ZIMEZUA KIZAAZAA MANISPAA YA BUKOBA
Mkuu wa wilaya ya BUKOBA,
bi ZIPPORAH PANGANI, amewatahadharisha
Wananchi mkoani KAGERA, kutojichukulia
sheria mkononi, pale wanapowatuhumu watu
kwa makosa mbalimbali.
Bi PANGANi, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, ameonya kuwa hakuna mtu yeyote aliye
juu ya sheria, na kuwa yeyote
atakayevunja sheria, atashughulikiwa kwa
mujibu wa sheria.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa
tahadhari hiyo baada ya kutembelea eneo la Majengo Mapya, Kata KASHAI, ambapo kundi kubwa la wananchi walikuwa
wamekusanyika.
Mtuhumiwa huyo, ambaye ni
mwanamke, amelazimika kupelekwa polisi,
baada ya watu wenye hasira kuingia ndani
ya nyumba yake, kufuatia kuwepo uvumi kuwa alikuwa anawahifadhi watoto sita, kwa
lengo la kuwafanyia vitendo vinavyodaiwa kuwa ni vya ushirikina.
Polisi wakipiga mabomu ya machozi ili kutawanya mamia ya raia waliotaka kuvunjwa nyumba ya mtuhumiwa huyo.Wanamgambo na askari polisi wakikusanya baadhi ya raia wanaosadikiwa kusha mawe katika vurugu hizo
Katika vurugu hizo, raia mmoja ambaye picha yake haikuwekwa hapa, ameripukiwa na bomu hilo na kumsababishia maumivu makali usoni na mikononi kupasuliwa vidole.
Subscribe to:
Posts (Atom)