MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 4 February 2014

WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI DODOMA WAMETAKIWA KUTENDA HAKI ILI KUTIMIZA MAJUKUMU YAO KWA JAMII.






Hayo yamesemwa na  Jaji mfawidhi Mkoani Dodoma  Crecencia  Makuru wakati akitoa ufafanuzi katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini  yaliyo fanyika katika viwanja vya mahakama kuu mkoani Dodoma.Akizungumza katika maadhimisho hayo Jaji   Makuru amesema maudhui ya sheria ya mwaka huu ni utendaji haki kwa wakati .Sanjari na hayo  amesema kuna vitu vikuu vitatu vinavyo weza kusababisha mahakama kutoaminika ikiwemo ucheleweshwaji wa kesi.

Maadhimisho  hayo  ni ya kumi na nane tangu  kuanziswa kwa  maadhimisho hayo mwaka  1996.
 

MWANA HARAKATI

Monday, 3 February 2014

WANANCHI WAMETAKIWA KUTUMIA MASHIRIKA KATIKA MASUALA YA KISHERIA


Rai hiyo imetolewa mapema leo, na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, mheshimiwa GADDY MJEMMAS, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania.
Jaji MJEMMAS amesema kuwa baadhi ya Watu wamekuwa wakipoteza haki zao kwa kukosa uelewa kuhusu masuala ya sheria, huku baadhi yao wakipoteza muda kwa kufungua mashauri mahakamani  yasiyostahili.

Akitolea mfano, Jaji MJEMMAS amesema kuwa mwananchi mmoja, ambaye hakumtaja jina, alifika mahakamani kwa nia ya kumfungulia kesi  ya madai baba yake mzazi ambaye bado yuko  hai, akimdai Mirathi.

Amesema kuwa Mirathi hutolewa kwa kuzingatia  matakwa ya mtoa Wosia, hivyo endapo mwananchi huyo angekuwa na uelewa wa  sheria, asingepoteza muda wake kufika mahakamani.

Jaji MJEMMAS pia amewataka Wananchi mkoani KAGERA kushirikiana na Polisi pale unapofanyika upelelezi kwa makosa ya jinai, na pia wajitokeze kutoa ushahidi mahakamani pale kesi inapoanza kusikilizwa.

Maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania huashiria kuanza kwa Mwaka wa  shughuli za  Mahakama nchini.

Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni : ‘UTENDAJI HAKI KWA WAKATI: UMUHIMU WA USHIRIKI WA WADAU’.
MWANA HARAKATI

SIKU YA MAHAKAMA YA ADHIMIDHWA MKOANI KAGERA

Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Bukoba mkoani Kagera GAD MJEMAS amewataka mawakili kutotoa mapingamizi yasiyo ya lazima ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati.

Hatahivyo viongozi wa magereza wametakiwa kutoa ushirikiano kwa kufikisha faili za kesi za watuhumiwa kwa wakati ili haki itolewe kwa wakati.

Wakati huo huo Jaj MJEMAS amesema kuwa ni muhimu kuajiri mawakili wa kutosha ili kupunguza malimbikizo ya mashauri mahakamani huku akisema kuwa wadau muhimu kwenye sheria ni mashirika binafsi kama MUHOLA na mawakili binafsi pamoja na wananchi wenyewe.

Ni maadhimisho yanayoendelea sasa hivyo tutakuletea habari zaidi.

MWANA HARAKATI

BINTI AUMBULIWA NA MPEZIE



MWANA HARAKATI

MAZISHI YA ASKARI 5 WALIOKUFA KWA AJALI

  
 Mami ya raia wakishuudia miili ya askari hao wakati wakiagwa kwa ajili ya kufanyiwa maziko.
MWANA HARAKATI

MATOKEO YA UDIWANI



Mgombea wa Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameibuka Kidedea kwa ushindi alioupata katika uchaguzi huo mdogo wa Jimbo hilo baada ya kukaa wazi kwa muda mrefu kutokana na kutenguliwa kwa aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo hilo Mhe. Mansoor Yussuf Himid.

Masimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kiembesamaki Ndg. Suluhu Rashid , akitangaza matokeo hayo baada ya kumalizika kwa kazi ya uhesabuji wa Kura na kuzijumlisha kura zote zilizopingwa na Wananchi wa Jimbo hilo.

Akitangazo matokea hayo ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki  yalioshirikisha Vyama Sita vya Siasa vilivyosimamisha wagombea wake.

Msimamizi wa Uchaguzi Ndg. Suluhu akitoa matokeo hayo Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameshinda kwa  Kura 1856, sawa na asilimia 75.1 na kutangazwa mshindi wa Uchanguzi huo Mdogo wa jimbo hilo kuchukuwa nafasi ilioachwa wazi na Mhe. Mansoor Yussuf Himid, aliyevuliwa Uwanachama na CCM na nafasi hiyo kuwa wazi kwa muda hadi kufanyika kwa uchaguzi mdogo leo na kumpata mrithi wa kiti hicho.


Mgombea wa Chama cha CUF Mhe. Abdulmalik Juma Jecha, amepata kura 445, sawa na asilimia 18.3, Mgombea wa Chama cha ADC Mhe. Amani Ismail Rashid  amepata kura 84, sawa na asilimia 3.5, Chama hichi ni kipya kimeungwa na Viongozi walioondoka CUF, na hii ni mara ya pili kushiriki Uchanguza tangu kuazishwa kilishiriki uchaguzi wa kwanza kisiwani Pemba katika jimbo la Chambani,Pemba.

Nae Mgombea wa Chama cha  CHADEMA Mhe. Hashim Juma Issa,amepata kura 34 sawa na asilimia 1.5, katika uchaguzi huo mdogo wa jimbo la kiembesamaki.Mgombea wa TADEA Ali Mohammed Ali (Mbongo) amepata kura 6 sawa na asilimia 0.3. Nae Mgombea wa Chama cha SAU Mhe. Ramadhani Simai Mwita amepata kura 1 sawa na asilimia 0.1

Kwa matokeo hayo Tume ya Uchaguzi Zanzibar imemtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kuwa ni Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki na anakuwa Mwakilishi halali baada ya ushindi huo.
 


MWANA HARAKATI

Sunday, 2 February 2014

ARSENAL YAILAZA CRYSTAL PALACE 2-0

Ni kazi iliyofanywa na CHAMBERLAIN dk 56 kuandika bao la kwanza na katika dk za 70 yuleyule kuandika bao la pili.

Mtanange umemalizika na umeudhuriwa na mashabiki 60,005, kesho ni CHELSEA na MAN CITY jioni.

MWANA HARAKATI

BREAKING NEWS!!! AJALI MBAYA BUKOBA

 Picha juu ni gari iliyopata hitilafu na kupoteza mwelekeo ikiwa na mzigo unaoonekana hapo nyuma, ambapo kichwa cha gari hilo ndicho kimesambaratika kama picha inavyoonesha na chini mzigo unaonekana ukiwa umefunikwa, mbele ikiwa ni sehemu iliyoharibika vibaya.



 Gari linaloonekana juu lilipisha gari iliyopata ajali mara baada ya dereva wa gari ili la chini kumwona mwenye scania ilianguka akija kwa kasi nyuma yake, ambapo pamoja na kumpisha, bado gari hilo limekwanguliwa kutokana na juhudi za kupishana wakati yote yakielekea sehemu moja.

 Picha juu ni Trafic akiangalia hali ya gari iliyokwanguliwa na chini ni taswira ya barabara ilivyokuwa baada gari hiyo kukwanguliwa na baadhi ya molamu nyeusi zilizokuwa kwenye gari hiyo kumwagika.
Taarifa rasmi kuhusu hali za waliokuwa ndani ya gari hiyo tutakuletea kwani kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa  WILIAM MKONDA amesema bado wanashughulikia ajali hiyo.
MWANA HARAKATI

MJI WA SIBUT WAKOMBOLEWA, RAIA WAFA NJAA S KUSINI HUKU UCHAGUZI WAGHUBIGWA NA VURUGU THAILAND

Kamanda wa kikosi cha amani cha Umoja wa Afrika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati anasema askari wake wameukomboa mji wa Sibut, kutoka kwa wapiganaji wa zamani wa Seleka.

Kamanda huyo, Jenerali Tumenta Chomud, alisema askari kutoka Gabon sasa wako mjini Sibut, na watawanyang'anya silaha wapiganaji waliouteka mji huo Alkhamisi.

Wapiganaji wa zamani wa Seleka - wengi wao Waislamu - wamekuwa wakiondoka mji mkuu, Bangui, ambao uko kama kilomita 200 kusini ya Sibut.
Kuondoka kwa Seleka kumezusha mauaji ya kulipiza kisasi, na watu zaidi ya 40 wameuwawa mjini Bangui katika siku chache zilizopita.
Uchaguzi mkuu ncini Thailand umeanza leo huku ilinzi ukiwa umedhibitiwa, na kukiwa na taarifa za vurugu katika baadhi ya maeneo.
Umoja wa mataifa unakadiria kwamba takriban watu millioni 3.7 nchini Sudan kusini wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi walio watiifu kwa aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar.

Mratibu wa maswala ya kibinaadamu katika umoja huo Toby Lanzer amewaambia waandishi habari kuwa mzozo huo ulioanza mwezi Disemba mwaka jana umeharibu masoko pamoja na maisha ya kawaida ya watu, mbali na kusababisha hali mbaya ya kibinaadamu kwa thuluthi moja ya idadi ya raia.
MWANA HARAKATI

MAGAZETI LEO 02 JAN 2014





MWANA HARAKATI

MAN U JAMANI!!!!!!!!!!

Katikati Charlie Adam akishangilia na Mark Hughes baada ya kufunga mabao mawili yaliyoifanya Stoke imalize ukame wa ushindi ndani ya mechi sita.

MABAO mawili ya Charlie Adam yameipa Stoke City ushindi wa kwanza kabisa kihistoria dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Britannia.

Adam alifunga mabao hayo dakika ya 38 na 52, wakati bao pekee la United lililofungwa dakika ya 47 na Robin van Persie.

Kiungo mpya wa United, Juan Mata alicheza kwa dakika zote 90 na hakuweza kuwaepusha Mashetani hao Wekundu na kipigo. United sasa inabaki na pointi 40 baada ya kucheza mechi 24 na inaporomoka hadi nafasi ya saba kutoka ya sita.
MWANA HARAKATI

Saturday, 1 February 2014

BINTI MDOGO AMEISHI KWA KUWEKEWA VIDOLE SEHEMU ZA SIRI NA BOS WAKE

Ni mtoto mwenye miaka 13 baada ya kuwa anafanya kazi za ndani wilayani Muleba alipoajiriwa kwenye familia moja yenye baba na mama lkn kutokana na mama kuondoka mara kwa mara nyumbani hapo kitokana na masuala ya kazi, baba mwenye nyumba amekuwa akimwita mtoto huyo chumbani kila anaporejeakutoka kazini.

Kwa mujibu wa mtoto huyo ambaye jina limehifadhiwa, baba huyo amekuwa akimtegeshea mke hayupo ana mwita binti chumbani na kumwingizia vidole sehemu za siri huku akisema kuwa anamwangalia kama ameoga.

Ameeleza kuwa mwanzoni amekuwa akiumia lakini badaye akazoea na hana maumivu tena kwani limekuwa jambo la kila siku na la kawaida.

Baada ya ufuatiliaji wa dawati la jinsi polisi mkoani Kagera, bwana huyoamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi na mtoto amechukuliwa na mmoja wa wasamaliawema lakini bado wanatafutwa wazazi wake ili kujua wamelichukuliaje na kwanini wamtafutie mtoto ajira akiwa ns umri huo

MWANA HARAKATI

WANAFUNZI 1400 KUKOSA SEHEMU YA KUKAA

Wanafunzi hao ni wa shule ya msingi Mizani katika kata Nyakahula wilayani Biharamulo kutokana na ongezeko ktk shule hiyo yenye chekechea hadi la 3.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa kijiji YUSUPH SEIF amepanga kuitisha kikao cha wazazi tarehe 6 mwezi  huu kuangalia uwezekano wa kujenga shule nyingine ili kupunguza ongezeko hilo

Shule iliyopo sasa ina madarasa manne na chumba kimoja kinatumiwa na walimu kama ofc ambapo wanataka kujenga shule mpya kutokana na uwingi wa watoto ktk kijiji hicho.

MWANA HARAKATI