MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 16 August 2015

JAJ JOSEPH BUTIKU ATOBOA SIRI ZA CCM, ATAJA MTANDAO WA WATU 10



. Kulikuwa na mtandao wa watu 10,
. Asema wanaoondoka ndani yake waondoke,
. Asema utajiri usitumike kukandamiza wanyonge.

Ni mwenyekiti wa taasisi ya mwalimu Nyerere alipozungumza na watanzania kupitia mdahalo ulioandaliwa na taasisi hiyo, kwakusema kuwa mtandao huo uliokuwa umejikita ndani ya CCM, ulikuwa ukiweka masharti ndani ya chama hicho kuwa usizungumziwe kuhusu utajiri wake.
Amesema kuwa utajiri siyo tatizo tatizo ni jinsi utajiri huo unavyotumika, kwa kuwatupia wananchi kama kuku, jambo ambalo Mwalimu Nyerere alisema ni lazima heshima ijengwe kwenye chama na asiyetaka anaweza kuondoka.
Kwaupande wake Profesa Balegu, amesema kuwa hawezi kutoa tuhuma kwa mtu yeyote, huku akisistiza kuwa unaweza kufanya kazi kwenye taasisi yenye uadilifu nawe ukawa mwadilifu au ikawa kinyume chake.

Humphrey Polepole, amesema kuwa Nyerere asitafsriwe vibaya kwa kusema kuwa alitaka mabadiliko
kwani mwenyewe alitaka mageuzi ambayo yanajumuisha mambo mengi na yenye kuwaletea wananchi maendeleo na uwajibikaji bora, wala siyo mabadiliko ya vyama kama wengi wanavyoimba.





Naye Bwana Muhammad Yusuph Mshamba, amesema kuwa sheria ni lazima ifuatwe katika mchakato huu
wa uchaguzi mkuu, kwani wakisea huku ya ICC haitahepukika kwasababu Tanzania ni mwanachama wa mahakama hiyo ya kimataifa ya makosa ya jinai.
 





Katibu wa CCM Tanzania bara Bwana Philip Mangula, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ndogo ya maadili ndani ya chama hicho, amesema kuwa yeye kama mmoja wa wajumbe wa umoja wa vyama 22 vya siasa nchini, walikubaliana kwa pamoja kuhakikisha wanatuza maadili ya vyama vyao hivyo atashangaa kuona ukiukwaji unaendelea katika vyama.

Na Mwanaharakati.

TAARIFA MWANZA MAPOKEZI YA LOWASA

Taarifa zilizotufikia kutoka kwa shuhuda zinasema kuwa polisi wameweka ulinzi mkali na wamefyatua mabomu ya machozi kutawanya wananchi waliojitokeza katika uwanja wa ndege kusubiria mgombea urais kupitia UKAWA Edward Lowasa.

Inasemekana wananchi wanazingira eneo hilo bila utaratibu ikizingatiwa serikali imekwishatoa maelekezo juu ya wagombea wanaozunguka mikoa kutafuta wadhamini kuwa hakuna kufanya maandamano kwa kunajitokeza madhara katika misafara hiyo, na ni uvunjifu wa kanuni za uchaguzi.

Tutakuletea undani...
Picha na jamiiforums mapema leo.

NEWS ALERT!!! WALICHOSEMA WALIOKUWA MAASIMU WA KAGASHEKI HIKI HAPA

. Makundi sasa kwisha,
. Ni katika CCM kutambulisha wagombea,
. Kagasheki asema aliyofanya sasa mtayaona.
Chama hicho kimetangaza na kutambulisha rasmi wagombea wake katika manispaa ya Bukoba, katika ngazi ya ubunge na udiwani, ambapo Balozi Khamis Kagasheki amekabidhiwa bendera ya kugombea ubunge, huku madiwani 14 wa kata za manispaa nao wakitangazwa.

Itakumbukwa katika utiaji nia, walijitokeza wagombea 8,  walioshindwa wamejitokeza jukwaani na kukubali matokeo, lakini wakiahidi kushiriki kumwombea kura mteule, lakini wakaenda mbele Zaidi kuwa.<<<BOFYA SAUTI>>>



Katika mkutno huo wa utambulisho, Mh Kagasheki amesema kuwa yaliyokuwa yakibezwa kuwa hakifanya lolote, sasa yataanza kutajwa kwa vitendo kwani wananchi wanayajua, na kamwe yeye hakulenga kuwaletea maendeleo matajiri wenye uwezo bali wananchi wa kawaida ambao hatahivyo hawapati fursa ya kusikika wakifanya ushabiki.



Na Mwanaharakati.

HATARI; HII NDIYO KAZI YA SHERIA YA MTANDAO NA UTANGAZAJI



Serikali imevitaka vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu kutoa wasemaji wa mwenendo wa siasa katika kipindi chote cha uchaguzi.

Mkurugenzi wa idara ya utangazaji Tanzania, amesema hayo wakati wa kuchambua kanuni za utangazaji katika vyombo vya habari wakati wa uchaguzi wa vyama vya siasa hapa nchini, kwenye semina ya siku moja iliyowashirikisha wakurugenzi, wahariri na waandaaji vipindi wa redio na tv kanda ya ziwa.

Amesema kuwa kutokana na kupitishwa kwa sheria kuhusu vyombo vya habari na utangazaji, ni lazima hata vyama vifuate utaratibu elekezi, ili kutoa fursa pande zote kushiriki kikamilifu huku akisisitiza kuwa hakuna chama cha siasa au chombo cha habari kitakachoonewa kama sheria na taratibu zilizowekwa zitafuatwa.
Kwaupande wake afisa mkuu wa utangazaji Tanzania Andrew Kisaka, amesema kuwa hakuna tatizo la mtangazaji au mwandishi kufanya mawasiliano na chama cha siasa au mwanasiasa kwa lengo la kupata habari, ingawaje mwandishi atakayeshiriki kugombea atatakiwa aombe likizo au kuacha kazi kwa muda wote wa uchaguzi
Amesema kuwa wanasiasa watakaotakiwa kuhojiwa na vyombo vya habari, watatakiwa kukubali ili kusaidia chombo husika kufanya kipindi chenye uwiano sawa, kwani atakapokataa haitaondoa chama kingine au mwanasiasa mwingine kuhojiwa ingawa lazima vyama viwili au zaidi vishiriki kipindi hicho.
 
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, imetoa semina hiyo kwa vyombo vya habari kanda ya ziwa, kwa dhamira ya kudhibiti mawasiliano, kusisitiza kufuata sheria itakayoanza kutumika tarehe 1 mwezi wa 9/2015. 

Na Mwanaharakati.

Sunday, 9 August 2015

MBUNGE AFARIKI KWA AJALI

Taarifa inasema kuwa Mbunge wa viti maalumu CUF aliyejulikana kama Clara Diana Mwatuka, amefariki kwa ajali baada ya gari take iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyetajwa kuwa mwanae, kupinduka katika mteremko wa Malunde Plateau kuelekea Ndanda.

Habari zilizoufikia Mtandao huu zinasema kuwa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospitali ya Ndanda Regional referral.

Mungu amuweke paala anapostail amin.
Na Mwanaharakati.

Saturday, 8 August 2015

TAARIFA YA VIKAO VYA CCM KUHUSU WAGOMBEA

Kwa mujibu wa ratibaya chama hicho, vikao vya mijadala ya watia nia ngazi mbalimbali ni kama ifuatavyo:- Leo tarehe 8 -9 ni sekretariet ya halmashauri kuu taiga inayoweka mikakati na kupitia vikao vya mwongozo wa kujadili watia nia, tarehe 10- 11 itakaa kamati kupokea na kujadili taarifa kutoka majimbo yote, na tarehe 12- 13 halmashauri kuu taifa ambayo ndiyo itachuja na kupitisha wagombea wakupeperusha bendera kupitia chama hicho.

Hatahivyo katibu mwenezi Nape Nnauye amekemea jinsi malalamiko yanavyotolewa.


Tutaendelea kukuletea taarifa kutoka vikao hivyo.
Na Mwanaharakati.

Friday, 7 August 2015

NAFASI ZA KAZI AFISA MASOKO NA AFYA HIZI HAPA MWISHO 31 AUG 2015

  • Job Vacancy > Marketing Executive
    Location > Mwanza
    Position Type > Part Time
    Organization Type > Company

  • Mwanza Dealers Centre Tanzania Limited

Application Deadline: 30 Sep 2015
Marketing Executive POSITION DESCRIPTION:
Mwanza Dealers Centre Tanzania Limited is looking for Marketing Executive who will be responsible for finding markets and receive a commission when he/ she makes sells. The company deals with General HVAC consultancy, Sales, maintenance, HVAC piping layout and air conditioners service provider as well as refrigeration, Furniture, and other electronics and home appliances.
The more you sell the high the commission, no salary under this position.
APPLICATION INSTRUCTIONS:
  • Job Vacancy > Clinical Officer
    Location > Arusha
    Position Type > Full Time
    Organization Type > NGO Website > http://www.fameafrica.org

  • Fame Medical Health Center

Application Deadline: 31 Aug 2015
Clinical Officer POSITION DESCRIPTION:
Position Description Document (download)
APPLICATION INSTRUCTIONS:
Send your updated and relevant CV, Cover letter and copies of your certificates to the following address

FAME MEDICAL
BOX 351 KARATU
Na Mwanaharakati.

MAKUBWA; TAKUKURU KAGERA YACHUNGUZA TAARIFA ZA RUSHWA KURA ZA MAONI.



. Matukio 31 yachunguzwa na TAKUKURU,
. Upotoshaji wahusishwa,
. Wanahabari waaswa kuwa makini.

Akizungumza na mtandao huu juu ya malalamiko ya wananchi kwa kutaja RUSHWA kwa kila jambo mkoani Kagera, mkuu wa TAKUKURU Kagera RBC Joseph Mwaiswelo, amesema kuwa imekuwa ngumu kukomesha rushwa kama hakuna mlalamikaji kati ya mtoaji na mpokeaji.

Matukio 31 kuchunguzwa TAKUKURU;-
Mwaiswelo amesema matukio 31 yamethibitishwa, ambayo hatahivyo bado yanachunguzwa kwa kuwahoji watoa taarifa, lakini bado hakuna lililokwisha muhusisha moja kwa moja anayetajwa kutoa au kupokea rushwa, kwasababu wanaotajwa kutoa hongo ni waliotia nia za kugombea ambao amesema huwezi kuwahoji kabala hujawa na uhakika wa kilichotajwa.

Kuhusishwa upotoshaji;-
Katika kipindi cha kampeini hadi upigaji kura ya maoni kuelekea kupata wagombea wa udiwani na ubunge katika majimbo yote ya mkoa wa Kagera, TAKUKURU imepokea taarifa nyingi za uongo, hasa ambapo mtoa taarifa hasa kwa njia ya simu anapotakiwa kuongozana na afisa na kushindwa kufanya hivyo.

Wanahabari waaswa kuwa makini;-
Kutokana na baadhi ya maswali kwa wanahabari kuonekana kuegemea sehemu au kwa mtu, afisa huyo wa TAKUKURU mkoa amewataka waandishi hao kuwa makini, kutokubali kutumika na baadhi ya watu ili kuwachafua wenzao, ilhali akisisitiza kuwa chombo cha habari kinatangaza au kuandika kupitia sera ya chombo hicho na malengo ya mmiliki kama alivyoruhusiwa na mamlaka, hivyo kuna haki zinazomlinda.
Katika mkutano huo, baadhi ya wanahabari wameonekana kulazimisha kupata majibu ambayo hayawezekani kwa mujibu wa sheria na taratibu, kwani hayaendani na baadhi ya maswali yaliyoulizwa wala hayahusiani na rushwa, hivyo kuwataka kujua kanuni za taasisi husika kabla ya kuwatuhumu wahusika wake.


Na Mwanaharakati.

Wednesday, 5 August 2015

HAWA NDIYO WAGOMBEA WALIOENGULIWA KAGERA KISA HIKI HAPA

Ni Anatory Amani, ambaye amejadiliwa kupitia vikao mbalimbali na kubainika kukigawa CCM kutokana na kusababisha migogoro lkn pia kutanya mambo kinyume na ilani ya chama hicho baada  na kukiuka taratibu za mikutano ya kutia nia kugombea nafasi ya ubunge na udiwani kwani alisikika akitoa kauli zilizokinyume na chama hicho.

Mwingine ni Chief Kalumuna ambaye ameomba kugombea udiwani kata Kahororo  na amejadiliwa na CCM na kubainika na makosa mbalimbali likiwemo LA kuwapeleka mahakamani madiwani wenzake na kukwamisha ilani ya CCM kutekelezeka.

Tutakupa zaidi kupitia hapa.
Na Mwanaharakati.

ULIVYOVUNJIKA MKUTANO WA LIPUMBA SOMA HAPA

Umevunjika na kutofanyika baada ya waze na wanachama wengi kuzingira ofisi ya chama hicho na kumtia hofu Lipumba, baada ya wanachama hao kushinikiza kuwa wanatakja kujua kama atatangaza kujiuzulu ili wajue chakufanya haraka iwezekanavyo.

Baadhi ya wajumbe wamehoji kwanini umehairishwa na alitaka kuzungumza nini, wakajibiwa na ,Magdalena Sakaya mbunge kupitia chama hicho ambaye amesema kuwa kuna wazee wametaka kwanza kujua kauli ya Lipumba kwa wanahabari ndipi aendelee, hali iliyomfanya mwenyekiti huyo CUF Profesa Ibrahim Lipumba kuahirisha hadi siku nyingine.

Na Mwanaharakati.

NAFASI ZA KAZI SERIKALINI NA BINAFSI HIZI HAPA

Nafasi za kazi chuo kkikuu Dar es salaam, mwisho tarehe 19/8/2015 katika kada mbalimbali.
FUNGUA HAPA 1

Nafasi za kazi kutoka EWURA kwa kada na elimu mbalimbali tuma maombi kabla ya Agost 21 2015
FUNGUA HAPA 2

Kwa waandishi wa habari nafasi za kuandaa vipindi kwa muda wa miezi 7 tu, BBC MEDIA ACTION, mwisho tarehe 10 Agost 2015
FUNGUA HAPA 3
Na Mwanaharakati.

MAKUBWA BAADA YA MWENGE WA UHURU KUTUA KAGERA HAYA HAPA



Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 13 mkoani Kagera ambapo Mwenge huo ulipokelewa mkoani hapa Wilayani  Biharamulo Kata ya Kalenge mpakani na Mkoa wa Kigoma tarehe 2/08/2015.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella  akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Issa Machibya alisema kuwa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa mkoani Kagera katika Halmshauri zote za Wilaya saba na Manispaa ya Bukoba na kupitia jumla ya miradi 52.

Katika miradi hiyo 52 Mwenge wa Uhuru utazindua miaradi 25, utakagua miradi 12, utaweka mawe ya msingi katika miradi 13 aidha  Mwenge huo  utapitia miradi mingine miwili ya kijamii ili kuhamasisha maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Kagera.

Mhe. Mongella alitaja mchanganuo wa gharama za miradi hiyo 52 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru kuwa serikali kuu imechangia kiasi cha shilingi 3,257,174,146 sawa asilimia 23.8 Halmashauri za Wilaya zimechangia  kiasi cha shilingi 1,763,070,553 sawa na asilimia 12.9.

Aidha wananchi wamechangia  shilingi 3,086,502,508 sawa na asilimia 22.5  wahisani wamechangia shilingi 5,595,751,962 sawa na asilimia 40.8  ambapo jumla ya gharama yote katika Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba katika mkoa wa Kagera ni shilingi 13,702,499,169 sawa na asilimia 100.
Mwenge wa Uhuru wenye ujumbe  usemao Tumia Haki yako ya Kidemokrasia, Jiandiishe na kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2015, Vijana wa leo na UKIMWI wazazi tuwajibike, Uteja wa Dawa za kulevya unazuilika na kutibika chukua hatua, Wekeza kwa maisha ya baadae tokomeza Malaria, pia Kata mnyororo wa Rushwa  chagua kiongozi mzalendo.
Ujumbe huo unalenga kuwahamasisha wananchi hasa vijana kujikita katika shughuliza uzalishaji badala ya kujihusisha na madawa ya kulevya, uteja, ngono zembe, rushwa  pia na kuchukua hatua dhidi ya malaria pia wananchi kujitokeza kujiandikisha na kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu 2015.
Mwenge waUhuru ulipokelewa Wilayani Biharamulo tarehe 2/08/kuelekea Biharamulo ni Ngara, Kyerwa, Karagwe, Misenyi, Bukoba Vijijini, Manisapaa ya Bukoba na mwisho ni Muleba na Mkoa utakabidhi Mwenge mkoa wa Geita.
Mwenge wa Uhuru uliopokelewa tarehe 2/08/2015 unatarajia kumaliza mbio zake mkoani Kagera tarehe 9/08/2015 na kukabidhiwa mkoani Geita tarehe 10/08/2015 aidha utahitimisha mbio zake kitaifa mkoani Dodoma tarehe 14/10/2015 na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete.
 

Na Afisa habari mkoa.

Sunday, 2 August 2015

MATOKEO YOTE KURA ZA MAONI KAGERA BAADHI KUTOLIPA HELA ZA MIKUTANO

Katika upigaji wa kura mkoani Kagera, wana CCM wamechagua wagombea watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika kampeini za 2015 katika majimbo mbalimbali.

Bukoba mjini wagombea walikuwa nane, ambapo balozi Kagasheki ameshinda kwa kura 6971, akifuatiwa na Amani aliyepata kura 944.
Bukoba vijijini mshindi ni Jacson Rweikiza, Muleba kaskazini Mwijage, Muleba kusini Profesa Anna Tibaijuka, Nkenge Dr Diodorous Kamala kura 8,229 dhidi ya Kyombo 5,429 na Assumpta Mshama 5,273.

Katika manispaa ya Bukoba kabla ya kutangza matokeo, mkurugenzi wa uchaguzi CCM ambaye pia ni katibu wa chama wilaya, amesema kuwa Dr Amani hakujitokeza kusaini lakini alipotafutwa alitoa udhulu, hivyo leo subuhi ametakiwa kusaini kwasababu ndiyo sheria za chama wala siyo ihali.
Mtandao huu bado unafuatilia taarifa za watia nia watatu katika manispaa ya Bukoba walioshindwa kulipa milioni 2 za kampeini kwa mujibu wa kanuni za chama, ambao ni Mjuni Kataraiya, Anatory Amani na George Lubaiyuka.
Na Mwanaharakati.