Nicolaus Mac (None Association Movement) KWA MATANGAZO YA REDIO NA TV WASILIANA NASI KWA +255767814844- nicolausngaiza@gmail.com.
Sunday, 29 April 2012
SHULE YA MSINGI YAKUMBWA NA UJENZI HOLELA;-
BAR YATIA KINYAA KWA NZI
Ni baa ya pombe ambayo kwa kiasi kikubwa imeonesha kutojali afya za watu kutokana na kujaa nzi kila kona kutokana na mazingira yake kuwa na majani na takataka. Juu ya meza ni kinywaji cha mtu kimezungukwa na nzi nje ya uwanja wa mpira wa miguu Kaitaba mjini Bukoba.
JENGO LA CCM MKOA WA KAGERA LIMESHINDIKANA KUMALIZIKA KWA MIAKA MINGI SASA;-
Thursday, 26 April 2012
SAMAHANI KWA KUTOWEKA HABARI MPYA KWA MUDA WA WIKI NZIMA;
BAADA YA KUWA KIMYA KATIKA BLOG YETU, SASA TUMEREJEA KUANZIA KESHO SAA TANO TUTAKUWA NA HABARI MPYA KADRI ZINAVYOPATIKANA.
Monday, 16 April 2012
RAIS KIKWETE AWASILI BRASILIA NA MAMA SALMA KIKWETE;
Rais Jakaya Mrisho kikwete amewasili Brazil
jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tano.
Katika ziara
hiyo Rais Kikwete anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake
Rais Dilma Varna Rousseff wa Brazil na Rais mstasafu wa nchi hiyo
Mheshimiwa Inacio Lula da Silva na viongozi waandamizi wa nchi hiyo.
Rais Kikwete
anatarajiwa kuhutubia mkutano huo tarehe 17 Aprili, mara tu baada ya hotuba
ya ufunguzi itakayotolewa na Mwenyekiti wa mkutano huo Rais Dilma
Rousseff wa Brazil, ambapo ataelezea maendeleo iliyofikia katika kuandaa mpango
kazi wa kutekeleza ahadi ya kuongeza uwazi kama
ilivyokubaliwa katika kikao kilichofanyika Disemba 2011.
Rais Kikwete
anatarajiwa kurejea nchini Aprili 20, 2012.
Sunday, 15 April 2012
RAIS KIKWETE AMEONDOKA NCHINI KWENDA BRAZIL
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho
kikwete anatarajia kuondoka leo tarehe 14 April, 2012, jioni kuelekea Brazil kwa
ajili ya ziara ya kikazi ya siku tano.
Katika ziara hiyo
Rais Kikwete anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais
Dilma Varna Rousseff wa Brazil na Rais
mstasafu wa nchi hiyo Mheshimiwa Inacio da Silva Lula na viongozi waandamizi wa
nchi hiyo.
Katika ziara hiyo,
Rais Kikwete atahudhuria mkutano wa mwaka wa wakuu wa nchi zinazoshiriki katika
Mpango wa Ubia wa Uwazi Serikalini (Open Government Partnership-OGP)
utakaofanyika mjini Brasilia chini ya Uenyekiti wa Rais Rousseff na kuhudhuriwa
na wajumbe wapatao mia nne (400) kutoka serikalini, Asasi zisizo za kiserikali,
Sekta binafsi pamoja na Mashirika ya Kimataifa.
Ubia wa Uwazi Serikalini au kwa kifupi OGP, ni mpango uliozinduliwa Septemba 2011 mjini New York, Marekani kwa lengo la kuwapa wananchi nafasi
ya kushiriki katika kuamua mambo
yanayowahusu, kupitia vyama visivyo vya Kiserikali na vya Kijamii.
Ubia huu
unashirikisha kwa usawa wawakilishi wa serikali kwa upande mmoja na wawakilishi
wa Asasi zisizo za Kiserikali za Kijamii kwa upande mwingine. Nchi ya Brazil
kwa kushirikiana na Marekani imekuwa mstari wa mbele katika kusukuma ubia huu.
Rais Kikwete
anatarajiwa kuhutubia mkutano huo tarehe 17 Aprili, asubuhi mara tu baada ya
hotuba ya ufunguzi itakayotolewa na
Mwenyekiti wa mkutano huo Rais Dilma Rousseff ambapo ataelezea maendeleo
iliyofikia katika kuandaa mpango kazi wa kutekeleza ahadi ya kuongeza uwazi
kama ilivyokubaliwa katika kikao kilichofanyika Disemba 2011.
Rais Kikwete
anatarajiwa kurejea nchini tarehe 20 Aprili, 2012.
…………Mwisho……………
Imetolewa na Premi
Kibanga,
Mwandishi wa Habari
wa Rais, Msaidizi
Ikulu
Dar-Es-Salaam
14 April, 2012
MVUA MANISPAA YA BUKOBA ZAASHIRIA MAFURIKO KUTOKANA NA UJENZI HOLELA;-
CHINI ni picha iliyochukuliwa wakti wa mvua asubuhi leo katika moja ya daraja la Brabara ya Kashozi eneo la machinjioni katika manipaa ya Bukoba.
Katika eneo la makaazi ya watu kumekuwa na uwingi wa maji unaotokana na miundombinu mibovu inayoharibiwa na wananchi kwa kuje holela, hata kama serikali ya mkoa inajitahidi kuboresha miundombinu hiyo.
Awali mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu FABIAEN MASSAWE aliwataka viongozi wa miundombinu kwa kushirikiana na afisa afya kuhakikisha wanasafisha mitaro ukiwemo mto mkubwa katika manispaa hiyo.
CHINI ni mtaro mmojawapo wa maji ambao unalemewa kupitisha maji kipindi cha mvua kutokana na udogo wake.
Saturday, 14 April 2012
KAGERA SUGAR YATOSHANA NGUVU NA AFRICAN LYON, HUKU MMILIKI WA AFRICAN LYON AKIWALAUMU WAAMUZI;
Picha juu ni wachezaji wa Kagera Sugar wakitoka uwanjani kwa masikitiko baada ya kutoka sare na wachezaji wa African Lyon ambao nao hapa chini wanaonekana kusikitika sare hiyo.
Baada ya mchezo huo mmiliki wa African Lyon amelaumu waamuzi na kudai kuwa huo ni ubabaishaji huku akishindwa kutanabaisha tatizo analolalamikia lakini amedai TFF ina fanya upuuzi kwa kuwatumia waamuzi wasiyo na viwango.
Ndani ya mchezo huo mwamuzi ametoa kadi 3 za njano na nyekundu 1 kwa wachezaji wa African Lyon.
Uwanjani Kaitaba jumatato wiki ijayo kutakuwa na mtanange mwingine kati ya Kagera suga na Yanga Afrika.
Friday, 13 April 2012
JESHI LA GUINEA BISAU LIMEMKAMATA WAZIRI MKUU WA NCHI HIYO;
BISSAU- Soldiers have arrested the prime minister of Guinea-Bissau,
a military spokesman said Friday, hours after the leader's home was
attacked with grenades in what former colonial ruler Portugal described
as a military coup.
The attacks that rocked the capital of this tiny country known for cocaine trafficking late Thursday came just two weeks before Prime Minister Carlos Gomes Jr. was to take part in a presidential runoff election as the frontrunner.
Military
press attache Francelino Cunha told The Associated Press that Gomes had
been detained by the military. The whereabouts of the country's interim
president remained unknown.
The
Portuguese Foreign Ministry said it "urges the masterminds of the
military coup to respect the well-being of the Guinean democratic
authorities and free those who have been detained."
However,
a communique from an unidentified military commander that was released
Friday claims the soldiers don't want to seize power, but instead were
trying to halt an invasion from Angolan troops.
Prime Minister Gomes
had been favored to win the April 29 runoff after his challenger Kumba
Yala, a former president who was overthrown in a 2003 coup, said he
would boycott the vote because of irregularities in the first round of
balloting.
Hilo ni tukio la pili katika kipindi kifupi katika mataifa ya Afrika viongozi kupinduliwa na majeshi baada ya kubainika kuleglega katika utendaji.Wiki iliyopita Jeshi nchini Mali lilikubaliana na ECOWAS kurudisha madaraka ya kiraia baada kuhakikisha kuwa mpango wa kuwaondoa waasi wa kikulima waliokuwa wakiteka maeneo ikiwemo mji muhimu wa TIMBUKTU.
RAIS KIKWETE AZINDUA TUME YA KURATIBU MAONI YA KATIBA MPYA;
Katika uzinduzi uliofanyika Ikulu ya Dar es salaam, rais Kikwete amewaapisha pia wajumbe 30 wa tume hiyo wakiongozwa na waziri mkuu wa mstaafu JOFEPH SINDE WALIOBA.
Amewataadharisha kuhakikisha wanaongoza tume hiyo vizuri na kujitahidi kutokwama pindi wakienda katika baadhi ya maeneo na kukuta gharama za malazi ziko juu.
Tume hiyo itafanya kazi wa kuratibu maoni kuhusu mabadiliko ya katiba kwa kupatikana mpya au kufanya marekebisho ya hii iliyopo tangu 1977.
Amewataadharisha kuhakikisha wanaongoza tume hiyo vizuri na kujitahidi kutokwama pindi wakienda katika baadhi ya maeneo na kukuta gharama za malazi ziko juu.
Tume hiyo itafanya kazi wa kuratibu maoni kuhusu mabadiliko ya katiba kwa kupatikana mpya au kufanya marekebisho ya hii iliyopo tangu 1977.
Thursday, 12 April 2012
MAREHEMU JENERALI MWITA KIARO AAGWA MWANZA;
Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro
alizaliwa mnamo tarehe 1/01/1923 nakufariki dunia 10/04/2012.
Huyu ni mke wa kwanza wa marehemu Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro aitwaye Penina Kiaro, akiwa katika hali ya majonzi.
Chini ni baadhi ya makamabanda wakifuatilia misa ya kumwaga marehemu katika eneo la kilima kwenye nyumba mojawapo ya marehemu hapo Kapripoit Mwanza.
Mwali wa marehemu Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro unasafirishwa kwenda kwao Mara tayari kwa mazishi.
WALEMAVU KARAGWE WALILIA HAKI ZAO;
Mwenyekiti huyu (PICHANI CHINI) anadai kuwa wamebaini asilimia 92 ni unyanyapaa kati ya viongozi na walemavu wilayani karagwe.
Pamoja na hiyo mwenyekiti huyo amesema kuwa wamekuta baadhi ya wanafunzi wanaotakiwa kulipiwa gharama za shule halipiwi na badala yake wanalipiwa watoto waviongozi, kama watoto wa diwani ndiyo wanaolipiwa.
Amesisitiza kuwa wanaofanya ubadhilifu huo ni wenyeviti wa vitongoji, watendaji wa kata na vijiji kwa kushirikiana na madiawani wa maeneo husika.
Chini ni Kizito malinzi aliyekuwa dereva lakini alipata ulemavu mwaka 2010 baada ya kuwa alikuwa akirekebisha gari na gafra mwenye nalo akaliondoa na kumgonga na kumsaga mguu, kwa mujibu wake kesi inaendelea lakini haisikilizwi kwa umakini kwani kila akifika anapewa tarehe na anafamilia ya watoto 6 lakini anaishi kwa kuomba omba kutokana na kukosa mtaji, lakini anaomba wa kumsaidia nyenzo za kushona viatu na zingine za mkono anaweza kuzifanya hivyo mwenye uwezo amsaidie.
Akizungumza nami mwenyekiti wa halmashauri ya Karagwe Bw Ishuju Lunyogoto, amesema hakuna ruzuku ya serikali lakini wao kama viongozi wameweka mpango wa kujenga shule tano zenye miundombinu ya kuwapokea walemavu.
Tuesday, 10 April 2012
WAZIRI NCHIMBI AMESEMA SERIKALI IMETOA MILIONI KUMI KUGHAN MSIBA WA KANUMBA;
Wakizungumza katika kuuaga mwili wa Kanumba waziri Nchimbi amesema kazi za wasanii sasa imefika ukomo kwani kutokana na maombi ya wasanii walioogozana na Kanumba mwaka jana waliomba kuwa na shirikisho litakalosimamia kazi zao na rais pamoja na viongozi wengine wamesema hii nafasi inatumika kusisitiza kuendeleza fani hii ambayo ilikuwa ikifanywa kwa makini na msanii STEVEN CHARLES KANUMBA.
Naye katibu wa kamati ya mazishi na msiba JB amesema kuwa Kanumba atakumbukwa sana katika fani hii si kwa tanzania pekee bali afrika mashariki na kati na dunia nzima. Bofya Video ili kusikia waziri Nchimbi na baadaye JB kwa walichokisema hivi punde.
KANUBA ANAAGWA HUKU RIPOTI KUHUSU KIFO CHAKE ZIMEANZA KUTOLEWA, DOKTA NCHIMBI ASEMA SERIKALI IMTOA MILIONI KUMI;
Katika kuaga huku mwili wa marehemu ndugu ndiyo wameruhusiwa kuaga mwili na gari inayobeba mwili huo inapita katikati ya watu waliojipanga barabarani ila watu ni wengi sana,
Waziri wa habari na michezo Dokta EMMANUEL NCHIMBI amesema kuwa wasanii waliobaki waendeleze fani hiyo lakini kutokana na kazi aliyoifanya kanumba serikali imetoa shilingi milioni 10 kughani msiba.
The Citizen Reporter
Dar es Salaam. Tanzania’s premier film star, Steven Kanumba, died of a brain injury caused by a sudden blow to the head. One of the doctors who examined Kanumba’s body at Muhimbili National Hospital hinted that the actor died on the spot after suffering such severe brain damage that he collapsed and stopped breathing.
Kanumba died on Saturday in his room in a dramatic turn of events that many of his fans have yet to come to terms with.
On the night he died, the 28-year-old actor was reportedly with 18-year-old Elizabeth Michael, popularly known as Lulu, who is being interrogated at Kinondoni regional police headquarters at Oysterbay in Dar es Salaam.
Monday, 9 April 2012
KIVUKO KILICHOAHIDIWA NA SERIKALI HAKIONEKANI;
Akizungumza na Blog hii Afisa tawala msaidizi miundombinu mkoani Kagera Bwana SEIF USSEIN, amesema kuwa utaratibu wa kujenga kivuko katika eneo la Rubafu kilomita 42 kutoka Bukoba mjini, katika eneo la Bugabo Bukoba vijijini, uliwekwa na serikali ya mkoa kwa mpango wa kurahisisha mawasiliano zaidi ya miaka miwili iliyopita.
Nilipomhoji bwana Ussein kuhusu taarifa za mkandarasi kukatisha mkataba, alijibu kuwa ni kweli alikatisha baada ya serikali kumcheleweshea malipo lakini alilipwa kiasi flan cha pesa na bado anadai milioni 60 ambazo nilimuuliza kama amekatisha mkataba inakuwa serikali iendelee kumlipa badala ya yeye kuilipa serikali kwani ndiye aliyekatisha mkataba, alinijbu kuwa serikali haina hasara na hata hivyo hizo pesa mkandarasi huyo hajaja kuzidai.
Mapema nikizungumza na baadhi ya wafanyakazi waliokuwa kwenye kampuni ya mkandarasi kutoka kampuni ya JESCO ya jijini Mwanza iliyokuwa ikifanya kazi hiyo ikiwemo kujenga nyumba za wafanyakazi na TRA na Uhamiaji, walisema kuwa mkandarasi huyo ameshafariki lakini aliacha amekabidhi kila kitu.
Awali wakti nikichunguza uwepo wa kivuko hicho, nilifanikiwa kuelekea katika maeneo ya Kabindi na Kasensero nchini Uganda, nikakuta hakuna shughuli zozote za uwepo wa kivuko na nilipomhuliza afisa huyo alisema kuwa hata wao mapema walipata wasiwasi, lakini walishatuma barua kwa waziri wa uchukuzi ambaye alifanikiwa kukagua maeneo hayo alipofanya ziara mkoani Kagera na aliahidi kuliwasilisha kwa viongozi wa jumuiya ya afrika mashariki EAC kwani ni wazo zuri.
Hadi sasa ni miaka 2 tangua kuahidiwa kivuko hicho jambo lililozua maswali mengi kwa jamii ya wanakagera na baadhi ya wavuvi kutoka Uganda kwani hawaoni kinachoendelea, kwasasa majibu ndiyo hayo.
MABONDIA HAWA WANAMENYANA USIKU WA LEO MWANZA;
Bondia Tomasi Mashari akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa
ubingwa na Selemani Galile utakaofanyika usiku wa leo.
Bondia Tomasi Mashari kushoto na Selemani Galile, watafanya mbambano huo chini ya promota wa mpambano huo Prospa Rweyemamu.
Bondia Tomasi Mashari kushoto na Selemani Galile, watafanya mbambano huo chini ya promota wa mpambano huo Prospa Rweyemamu.
Sunday, 8 April 2012
TASWA YAZUNGUMZIA MAMBO MATATU;
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
A.MSIBA
WA KANUMBA
CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinaungana na wasanii wote
nchini na Watanzania kwa ujumla kuombeleza kifo cha msanii mahiri Steven
Kanumba kilichotokea usiku wa kuamkia Jumamosi jijini Dar es Salaam.
B.PONGEZI KWA SIMBA
KUINGIA 16 BORA
TASWA
inatoa pongezi za dhati kwa timu ya Simba ya Dar es Salaam baada ya kufanikiwa
kuingia hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika
(CAF) kwa kuitoa ES Setif ya Algeria Ijumaa iliyopita.
Tunawasihi wachezaji wa Simba
na viongozi pamoja na mashabiki wa klabu hiyo, wasibweteke na mafanikio hayo
badala yake waunganishe nguvu ili waingie hatua inayofuata hatimaye watwae
ubingwa maana hakuna lisilowezekana chini ya jua.
C. WAANDISHI WALIOSHINDA
TUZO
Kamati ya Utendaji ya
TASWA inatoa pongezi za dhati kwa waandishi wa habari za michezo walioshinda
Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) zilizofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam.
Waandishi hao ni Imani
Mani aliyeshinda upande wa magazeti, Anwar Mkama upande wa televisheni na
Abdallah Majura upande wa redio, ambao tunaamini juhudi za kazi zao
zimefanikisha kupata tuzo hizo.
Nawasilisha.
Amir
Mhando
Katibu
Mkuu TASWA
08/04/2012
UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa
Shirikisho la Filamu Tanzania
–TAFF- kuomboleza kifo cha msanii maarufu nchini Steven Charles Kanumba,
aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Aprili 7, 2012.
Katika
salamu hizo, Rais Kikwete amemwomba kiongozi huyo wa TAFF kufikisha salamu za
rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wana-familia ya Kanumba na kwa wasaani
wote nchini ambao wamepotelewa na mdau na mwenzi wao.
Rais
Kikwete amesema kuwa ameshtushwa na kuzunishwa na kifo cha msanii huyo ambaye
amemwelezea kuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye katika uhai wa
maisha yake mafupi na akiwa bado kijana sana amechangia kwa kiwango kikubwa
maendeleo ya sanaa ya filamu nchini na kupitia sanaa hiyo kuitangaza Tanzania
kimataifa.
Amesema
Rais: ”Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Ndugu Steven
Charles Kanumba. Kupitia filamu zake, ameburudisha na kuelimisha jamii yetu kwa
namna ambayo haiwezi kupimika. Alikuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa
ambaye mchango wake mkubwa katika kuanzisha, kukuza na kuimarisha sanaa ya
filamu nchini hautasahaulika.”
Ameongeza
Rais Kikwete: “Ndugu Kanumba pia ametoa mchango mkubwa katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania mbele
ya mataifa mengine kupitia sanaa ya filamu na uwezo mkubwa wa kisanii. Tutaendelea
kumkumbuka kwa mchango wake huo kwa nchi yetu.”
“Nakutumia
wewe Rais wa TAFF salamu zangu za rambirambi na kupitia kwako kwa wasanii wote
wa filamu na sanaa nyingine kufuatia msiba huu mkubwa kwa fani yetu ya sanaa.
Aidha, naomba unifikishie salamu za dhati ya moyo wangu kwa wanafamilia wote.
Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa. Waambie naelewa machungu yao
katika kipindi hiki kigumu cha msiba,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Namwomba
Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu za kuweza kuhimili kipindi hiki kigumu kwa
sababu yote mapenzi yake. Aidha, naungana na wana-familia na wasanii wote
nchini kuwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya
Marehemu Steven Charles Kanumba. Amen.”
Mwisho.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
07 Aprili, 2012
RAIS KIKWETE ATAZINDUA TUME YA KURATIBU MAONI IJUMAA APRIL 13 WIKI HII
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atazindua
rasmi Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Mabadiliko ya Katiba na kuapisha
wajumbe wa Tume hiyo Ijumaa ijayo, Aprili 13, mwaka huu, 2012.
Tume hiyo itazinduliwa na wajumbe wake kuapishwa kulingana na matakwa ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 iliyounda Tume hiyo. Aidha, Tume hiyo itazinduliwa rasmi wiki moja baada ya kuwa imetangazwa rasmi. Rais Kikwete alitangaza Tume hiyo jana, Ijumaa, Aprili 6, 2012, kwenye mkutano wa wahariri uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Tume
hiyo itakayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Joseph Sinde Warioba akisaidiwa na
Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustino Ramadhan ina wajumbe 30,
ikiwa ni wajumbe 15 kutoka kila moja ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Wajumbe wa Tume hiyo kutoka Tanzania Bara ni Profesa Mwesiga L Baregu, Ndugu Riziki Shahari Mngwali, Dkt. Edmund Adrian Sengodo Mvungi, Ndugu Richard Shadrack Lyimo, Ndugu John J Nkolo, Alhaji Saidi El Maamry na Ndugu Jesca Sydney Mkuchu.
Wajumbe wengine wa Tume hiyo kutoka Bara ni Profesa Palamagamba Kabudi, Ndugu Humphrey Polepole, Ndugu Yahya Msulwa, Ndugu Esther Mkwizu, Ndugu Maria Malingumu Kashonda, Mheshimiwa Al-Shaymaa J Kwegyir, Ndugu Mwantumu Jasmine Malale na Ndugu Joseph Butiku.
Wajumbe
wa Tume hiyo kutoka Tanzania Visiwani ni Dkt. Salim Ahmed Salim, Ndugu Fatma
Saidi Ali, Ndugu Omar Sheha Mussa, Ndugu Raya Suleiman Hamad, Ndugu Awadh Ali
Saidi, Ndugu Ussi Khamis Haji na Ndugu Salma Maoulidi.
Wengine kutoka Visiwani ni Ndugu Nassor Khamis Mohammed, Ndugu Simai Mohammed Said, Ndugu Muhammed Yussuf Mshamba, Ndugu Kibibi Mwinyi Hassan, Ndugu Suleiman Omar Ali, Ndugu Salama Kombo Ahmed, Ndugu Abubakar Mohammed Ali na Ndugu Ally Abdullah Ally Saleh.
Shughuli za Tume hiyo zitaratibiwa na Sekretarieti ambayo Katibu wake atakuwa Ndugu Assaa Ahmad Rashid na Naibu Katibu atakuwa Ndugu Casmir Sumba Kyuki.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
07 Aprili,
2012
Saturday, 7 April 2012
MAMA KANUMBA AANZA SAFARI KUTOKA BUKOBA;
Aethibitisha kupokea taarifa za kifo hicho na akasema kuwa jana alipigiwa simu na marehemu akimwambia kuwa amemtumia nauli aende Dar ili waagane ili Kanuba aende Marekan.
Ni ndugu wa karibu katika familia ya Kanumba wanaitana kama kaka na dada.
Baadhi ya wasafiri waliosubiri kuondoka katika ndege moja na mama Kanumba.
Ni ndugu wa karibu katika familia ya Kanumba wanaitana kama kaka na dada.
Baadhi ya wasafiri waliosubiri kuondoka katika ndege moja na mama Kanumba.
-STEVEN KANUMBA - “MWAKA HUU SITOSEMA KITU,NI KAZI TU”
Soko limetanuka kiasi
kwamba tunatambulika kimataifa. Pia hivi sasa makampuni ya kusambaza kazi zetu
yameongezea ikiwemo na pesa kwa kiasi fulani tofauti na hapo mwanzo.Safari bado
ni ndefu lakini angalau inatia moyo.
Nimejifunza mengi
lakini zaidi nimejua zaidi juu ya thamani kama msanii.
Kazi ambazo mimi naona zitoa vituko ni kama hiyo Uncle JJ, Je wewe? Kumbuka hatuko naye tena.
Subscribe to:
Posts (Atom)